
Siku za hivi karibuni tumeshuhudia kila mtu akija na blog yake,mlundikano wa blog umezagaa kila kona ya .com,kila mmoja ana malengo yake binafsi,wapo waliokuja na blog kama njia ya kujitangaza,kuna waliokuja kwa ajili ya kutafuta umaarufu,wengine kwa kuwa mtu fulani ana blog nami lazima niwe nayo,kuna waliokuja kwa ajili ya kusaidia jamii(kama AfroIT Blog) na kuna walioamua kuja na blog kwa ajili ya kutengeneza pesa. Hivyo madhumuni ya blog ni mengi ambapo hutegemeana na mwana bklog mwenyewe.
Hivyo basi ushindani unakuwa mkubwa mno,kumbuka mazingira ya ushindani siku hizi yanazidi kuwa magumu hivyo unahitajika kuumiza kichwa ili kuibuka kidedea kwenye uwanja wa wanablog.
Kuwa na blog bila ufahamu au maarifa yake kwa undani kuna uwezekano mkubwa sana usifikie lengo lako,ingawa niwengi wetu inatuwia ugumu kupima ufikiwaji wa malengo zaidi ya kuangalia figure ya takwimu za watembeleaji ambazo kwa upande mmoja au mwingine zinaweza kuwa na mapotezo makubwa.
Hapo zamani kuna watu walisema,ukitaka kumnyima kitu mwafrika basi kiweke kwenye maandishi(kitabu),ila kwa dunia ya leo hii,kila kitu kipo kwenye maandishi tena kwa urahisi zaidi vilevile hii imani imepotea kwakuwa tumekuwa na mapenzi makubwa na kusoma vitabu,hii ni kwakuwa kama unataka kufahamu mambo mengi ni lazima uwe msomaji mzuri ma wada na vitabu mbalimbali huku ukijumuika na wataalam ambao watakusaidia kuweza kufikia lengo.Sisi kama nchi tunazoendelea bado tunahitaji kujifunza na kujua mengi zaidi kila kukicha.
Hivyo basi nimeambatanisha kitabu ambacho naamini kitakuwa na msaada mkubwa kwa wanablog wa kitanzania ambapo utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza blog inayolipa na kufanikiwa. Yote haya na mengine meengi yanapatikanika bure ndani ya AfroIT Downloads.
Download kitabu hiki nenda AfroIT Downloads au link ya chini
http://download.afroit.com/?p=1166
Badala ya kusaidia umeanza kwa lugha ya madharau,kejeli na wivu! Hatuna shinda na desa lako. Sie tunaye mwalimu wetu ambaye ni bloga bingwa. Si mwingine bali SUBI wa WAVUTI.
ReplyDeleteSo what! whichever is your problem? maneno ya mkosaji hayo, stop making negative remarks at the expense of other people success.
ReplyDeleteWewe tatizo lako ni nini mtu akiwa na blog yake???..malengo ya blog ni juu ya mtu anayefungua wewe sidhani inakuhusu lolote. Kama ni umaarufu au ni hela wewe inakuhusu nini?
ReplyDeletena wewe hapa unatafuta nini? acha hizo bwana ...tatizo la watanzania hawataki kuona mtu mwingine anacho kitu kama chache...Blog ziko kila mahali nyingi nyingi tu hata watoto wa high shools huku tuliko wanalazimishwa wafungue na kukeep blog. Na blog wanaambiwa waandike topic na kitu chochote wanachopenda sasa sijui wewe ni nani kujadili watu na kuona kuwa na blog ni big deal...
Yaani wewe umeona sijui hao afroit tu ndio wanasaidia jamii. Hapa unafanya nini kwenye blog ya watu kama haikusaidiii kitu. unatuma nini kwa michuzi kama unaona haikusaiidii kupitisha habari zako...Kama hujaanza kufundisha watu juu ya kublog nenda kajifunze communication kwanza ndio urudi hapa....some people geeeeeeer
ReplyDeletehebu potezea wewe mbona wewe mwenyewe umekuja apa kwa nia ya kujitangaza, mdau wa kwanza kasema poa lekebisha kauli kwanza.....wewe kama umekuja na kitabu chako nenda kafungue chuo chako cha kufundisha jinsi ya kupata pesa kupitia blogs...kwanza umeiona web site yako iangalie wewe mwenyewe haina mvuto kabisaaaa.....na hatujui nini malengo yako maaana iko plain tuuu unazungumzia story za IT lakin cha kushangaza tunaona miti tuu apo kana kwamba tuko kwa zoo
ReplyDeletenapenda kukupa ushauli kwamba kabla hujapoda wenzako jiangalie kwanza wewe apo
tumelizika na google wanatufundisha kila kila kitu
hapa kila mtu yuko na mawazo yake
asante
hebu angalieni hii link yake anamfundisha nani sasa?????
ReplyDeletehttp://www.afroit.com/VideoDetails.aspx?eid=628
kwanza sauti mbaya hajui kujieleza kaka apo juu big up sana kwli akajifunze comunication
Duh,Watanzania nimewakubali,Hawasomi habari wao kurukia mada na kuanza kutoa mijungu.Mtoa mada hajamponda yeyote na amekuja kwa nia ya kuelimisha na si lingine.Na ndio maana ametoa kitabu ili watu wajifunze zaidi.Tatizo letu ni kukurupukia kila kitu.Hivi bado tunamtafuta mchawi jamani?
ReplyDelete