
Hapa nakuletea picha ya viboko wapatikanao katika hifadhi ya Katavi Mkoani Rukwa katika wilaya ya Mpanda.
Katika picha hiyo mdau wa blog ya jamii akiangalia viboko wapatao 300 ambao wanapatikana katika eneo hilo. Viboko hao ambao hupenda kuishi majini wakionekana wakigombania kujihifadhi kwenye tope kwani maji yameanza kukauka na kuwapa shida.
Ushauri kwa TANAPA waone uwezekano wa kuweza kuwanususru viboko hao ambao ni hazina kubwa kwa taifa na kivutio kikubwa cha utalii.
Kazi njema bro.
Mdau Ernest
Kama inawezekana ni TANAPA kwenda kuwamwagia maji safi kwenye hilo bwawa hapo ili pasikauke maana itakuwa ngumu sana kwao ku-survive kama pakikauka. Mdau umeleta kitu cha maana sana!
ReplyDeleteHamna la maana aliloleta mdau.Hii mother nature itajirekebisha yenyewe. Mvua itanyesha na viboko watakuwa ok hakuna haja ya kumwaga maji hapo katavi. Ni sawa na kuona simba anakula nyati na kuomba Tanapa iweke fence ya kutenganisha nyati na simba.
ReplyDeleteHuyu jamaa anajiami kwelikweli!! au yuko mbali hapo?
ReplyDeleteWatanzania wenyewe hawana maji sembuse hao Viboko jamani.
ReplyDeleteTANAPA WATATOKEA KAMA KUNA DILI LA KUPATA ULAJI ETC. LAKINI HIVI HIVI KUOKOA KITU AMBACHO HAWAJUI KITAWAINGIZIA MATUMBONI MWAO NIN NA LINI, SAHAU...............NDO BONGO HIYO!!!!!!!!!!
ReplyDeleteWanyama nao wana haki zao hata kama wako porini...na tunapozungumzia nchi ni watu na vilivyomo wakiwemo wanyama..kama tunawala kwa nini wasuhudumiwe? Hivyo nao wapewe social services...i mean TANAPA waangalie namna ya kuwaokoa ni sawa na samaki umtoe majini umuweke nchi kavu wanapata mateso hao viboko kwa kukosa maji
ReplyDeleteNasikia viboko wakali sana , sasa sielewi huyu alosimama hapa haogopi??? naomba nielimishwe ...
ReplyDelete