hii ni moja ya picha zilizopo katika kijiji cha Mwanalibeneke Maggid Mjengwa.na chini ni maelezo yake ya shukrani kwa wadau.


Ndugu Zangu,
Wapendwa Wangu.

ILIANZA siku, ukatimu mwaka, ikafika miwili, mitatu na sasa ni MIAKA MINNE YA MJENGWA BLOG!

Leo Septemba 19, 2010 Mjengwablog imetimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake. Mwezi na tarehe kama ya leo miaka minne iliyopita ndipo nilipoingiza picha ya kwanza humu kijijini. Niliazimia kuanzisha jukwaa la fikra huru. Ni fikra tofauti zenye kujenga, na zaidi picha
zichagie katika kuamsha fikra hizo.

Ndugu zangu,

Katika hilo natumia fursa hii kuwashukuru nyote kwa kuwa pamoja nami katika muda wote huu wa miaka hii. Hamkukata tamaa ya kutembelea Mjengwablog hata pale ilipopita siku au siku mbili bila mimi kuingiza chochote bloguni. Hakika, malengo ya kuanzishwa kwa Mjengwablog
tunayakamilisha kwa pamoja. Hapa pamekuwa ni mahala pa watembeleaji kuangalia picha, kuacha maoni au kusoma maoni ya wengine na kutafakari. Ni mahali pa kutafakari pia hata kama hakuna aliyeacha maoni, alimradi kuna picha itakayokufanya uburudike, uelimike na
ichochee tafakuri.

Bofya;

http://mjengwa.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. utazid kuelimisha wadau wote wa mjengwa kaka..tuko pamoja..nakuombea usichoke na uzidi kuendelea na libeneke..one love...bigytime

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri brother Maggid, kaza buti safari bado ndefu. Kila la Kheri, Inshaalah tutafika!.
    Mdau
    Tabata

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...