KATIKA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA EID, TANZANIA READING ASSOCIATION ( T . A ) IKISHIRIKIANA NA TANZANIA READING FC INAWALETEA MPAMBANO WA SOKA KATI YA TANZANIA READING FC Vs TANZANIA MILTON KEYNES FC.

BAADA YA KUSUBIRIWA KWA MUDA MREFU NA WAPENZI WA SOKA WA NCHINI UK, MABINGWA WA SOKA NCHINI UINGEREZA TANZANIA READING FC ( REMCO ) HATIMAE WATAINGIA UWANJANI KULITETEA TAJI LAO DHIDI YA TEAM YA MILTON KEYNES KUTOKA MILTON HAPO JUMAMOSI YA TAREHE 11 SEPTEMBER 2010, KUANZIA SAA NANE MCHANA KATIKA KIWANJA CHA KENSINGTON PARK OFF OXFORD ROAD OPPOSITE TESCO READING.

BAADA YA KUKOSA UPINZANI KWA MUDA MREFU, "VIJANA WA TEAM HIYO YA READING WAKO TAYARI KUONYESHA NI KWANINI TEAM ZINGINE ZIMEKUA ZIKIWAOGOPA" ALISEMA KOCHA MCHEZAJI WA TEAM HIO HANIU.

NAE MENEJA WA TEAM YA MILTON ALISEMA VIJANA WAKE WANATAKA KUTHIBITISHA KUWA WAO NI MOTO WA KUOTEA MBALI ,WAKO TAYARI KUCHUKUA NAFASI HIYO YA UBINGWA UNAOSHIKILIWA NA TIMU YA READING TANZANIA FC .
WASHABIKI WA TEAM HIZO MBILI WANAUSUBIRI KWA HAMU KUBWA MPAMBANO HUO KWANI WANATAMBIANA .

WADHAMINI WA PAMBANO HILO, TANZANIA READING ASSOCIATION ( T . A ) KUPITIA KWA MJUMBE FRANCIA CHENGULA WATATOA ZAWADI KWA MSHINDI WA PAMBANO HILO ATAPEWA ZAWADI YA POUND £100, MCHEZAJI BORA ATAPEWA ZAWADI YA MPIRA WA MIGUU , NA MSHINDI WA PILI ATAPEWA ZAWADI YA MPIRA MMOJA.

MJUMBE WA T.A . FRANCIA CHENGULA ALISEMA MORE TO COME FROM TANZANIA READING ASSOCIATION NA TANZANIA READING FC KWANI TUNAANDAA MPAMBANO MWINGINE KATI YA TA READING FC NA TEAM YA READING POLICE; USIKOSE.

TA READING INAKARIBISHA MICHANGO ILI KUSAIDIA TEAM HII AU WAFANYA BIASHARA WANAOTAKA KUTANGAZA BIASHARA ZAO KUPITIA HII TEAM.

TAFADHALI WASILIANA NA MJUMBE FRANCIA 07970113058.
ASANTENT NA KARIBUNI WOTE.

BAADA YA MPIRA HUO BONGO DEEJAYS WAMEKUANDALIA BURUDANI YA KUSHEHEREKEA EID KATIKA UKUMBI WA THE FACE CLUB KUANZIA SAA NNE USIKU MPAKA SAA KUMI NA NUSU ASUBUHI WOTE MNAKARIBISHWA!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. wazushi wakubwa nyie watu wa reading ubingwa huo wa uk kakupeni nani? au mmefanya nini kikubwa kujitangazia ubingwa, acheni hizo nyie kila mwaka watu wanajibondea leo mnatangaza ubingwa humu, tunataka mfanye hivyo uwanjani kama vipi tufanye bonanza hiyo j'mosi la tit 4 tat tukate mzizi wa fitina iteni timu nane tu.....east ham, leicester, mk, slough, coventry, northampton, totenham, reading...
    mdau wa soka slough

    ReplyDelete
  2. reading wazushi kila mtu anajua kuwa Slough fc ndio wakali uk

    ReplyDelete
  3. Reading FC chini ya Kocha Mchezaji Diego Mbegu wanashikilia kombe la ubingwa mwaka wa tatu sasa.

    Sasa nyie wa Slough mnabisha kitu gani...andaeni timu hizo ngebe mzilete uwanjani.

    Reading FC Daima.

    ReplyDelete
  4. NYOTE NGEBE TUPU TULETEENI MWALIKO SISI MABINGWA WA JUMUIYA ZA TANZANIA DUNIANI,TIMU YA JUMIYA YAWATANZANIA SAO POUL(BRAZIL)SEMA VISA TU NDIO INASUMBUA.

    ReplyDelete
  5. jamaa inaonekana mnatafutana sana huko kwenu ukerewe hahaha safi sana
    kubwa acheni maneno mengi mpira sio niture ni tiz kwasana ndio
    utaona matunda ya ushindi.
    sie tunawasubiri tusikize maneni yenu
    baada ya game hiyo. nanyie wa sao poulo poleni mko shimoni sana huko
    mpaka visa mletewe mh mnayenu hhahah. mdau GR

    ReplyDelete
  6. Kwanini tuandikie wino na mate yapo, njoni mshuhudie wenyewe hayo magoli na huyo atakaepokea hiyo £100

    ReplyDelete
  7. Jamani tuleteeni Hiyo Mechi huku Scotland na sisi ninyi mtakaoshinda.
    Mnatupa changamoto.
    Mdau Scots

    ReplyDelete
  8. UK Hakuna Timu kama Reading fred coast(coastal union ) sarai taifa ya jangombe, hassan china simba, richard kagera renja ,kasim ston town , haniu coastal union ,kuna watoto wa reading academy ! 3 abdull , moo , anuwar hawa wote ni watanzania musije sema majeshi ,tutaanza kuwaonyesha milton jumamosi .
    mdau reading

    ReplyDelete
  9. nini watu wa ukerewe wazushi tu kama gemu hamtuwezi sisi watanzania tunaoishi pakistani tunapiga gemu zote kuanzia cricket mpaka soka kama nini njooni huku karachi tupo na mzee kassim mbalo kocha mchezaji

    ReplyDelete
  10. Uzushi Huo... Sina mengi Haniu ukweli unaujua. Mkiwa tayari ndio muite mabingwa wa kweli East Ham na yule kocha wetu msaliti amerudi tupo imara kinoma. Ulizieni African Cuo UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...