Habari kaka michuzi,
Hongera kwa blog nzuri sana, sa kaka yangu, mimi nilikuwa naomba msaada wa mawazo toka kwa wadau wako wote popote walipo.
Ni hivi baada ya kukaa sana huku ulaya natamani tena kurudu TZ kwetu, kwani kunachosha huku.Ila kabla sijakuja huko nilikuwa nimeplan kukodi kontena niweke vitu vyangu ambayo nilikuwa natumia hapa, ni vitu kama furniture za ndani kama machine ya kuoshe vyombo, nguo, n.k, pamoja na kagari kamoja ambako ka 1990, unajua tena huku udhungu ukiuza hako ksbb ni old utapewa just 1000usd ni bora nije nako huko kapate nisukuma.
so wadaua wenye uzoefu hebu nijuzeni sintapata mambo ya kodi nikadondoka chini,kwani tz yetu inatisha kwa rushwa.
pia nilishasikia kuwa personal things have no tax, je ni kweli.Kampuni ya safirishaji nimepata tayari kwa huku huku ulaya, na katika chargers zao wameweka hadi watakao shusha likifika huko tz.
Ushauri ninaoomba je hakuna charge nyingine nitakazo chajiwa nikifika huko.je kama zipo zaweza fika sh, ngapi. kuhusu gari hii ya zamani haita nicost sana ikifika tz, je kama ipo ni sh ngapi.
Naombeni msaada mana faida ya kuleta vitu huko nadhani vingine ni ngumu kupata tz,Lingine eti jamani ukikodi contena may be mpaka bongo ni 8000usd, eti hawaniachii contena hii ni sahii.
Mbarikiwe wotee mtakao nichangia.
Asante Issa
Hongera kwa blog nzuri sana, sa kaka yangu, mimi nilikuwa naomba msaada wa mawazo toka kwa wadau wako wote popote walipo.
Ni hivi baada ya kukaa sana huku ulaya natamani tena kurudu TZ kwetu, kwani kunachosha huku.Ila kabla sijakuja huko nilikuwa nimeplan kukodi kontena niweke vitu vyangu ambayo nilikuwa natumia hapa, ni vitu kama furniture za ndani kama machine ya kuoshe vyombo, nguo, n.k, pamoja na kagari kamoja ambako ka 1990, unajua tena huku udhungu ukiuza hako ksbb ni old utapewa just 1000usd ni bora nije nako huko kapate nisukuma.
so wadaua wenye uzoefu hebu nijuzeni sintapata mambo ya kodi nikadondoka chini,kwani tz yetu inatisha kwa rushwa.
pia nilishasikia kuwa personal things have no tax, je ni kweli.Kampuni ya safirishaji nimepata tayari kwa huku huku ulaya, na katika chargers zao wameweka hadi watakao shusha likifika huko tz.
Ushauri ninaoomba je hakuna charge nyingine nitakazo chajiwa nikifika huko.je kama zipo zaweza fika sh, ngapi. kuhusu gari hii ya zamani haita nicost sana ikifika tz, je kama ipo ni sh ngapi.
Naombeni msaada mana faida ya kuleta vitu huko nadhani vingine ni ngumu kupata tz,Lingine eti jamani ukikodi contena may be mpaka bongo ni 8000usd, eti hawaniachii contena hii ni sahii.
Mbarikiwe wotee mtakao nichangia.
Asante Issa
Haloo pole sana. Hata mie niko Ulaya. Nakushauri kagari hako ukaache huko huko maana kama ni ka miaka ya 90 utachajiwa hela za uchakavu npaka ushangae.
ReplyDeleteUnaweza ukaagiza gari nzuri tu ambayo unaweza kupata vipuri toka Japan kwa bei poa. Kuhusu container kama ni ya kukodi hutaachiwa! Ukitaka nunua container yako huku Ulaya uweke vitu vyako uisafirishe! Kama ni yako utaruhusiwa kuichukua lakini kama ni ya kukodi itarudishwa bandarini baada ya kutoa vitu vyako. Nakushauri ununue container yako.
Bongo ya sasa si ya zamani. Vitu vingi vinapatikana siku hizi. Usipoteze hela kusafirisha vitu vingi. Gari ya 1990's ni ya nyuma sana unaweza kuzuiwa ku import!
ReplyDeleteKaribu nyumbani kijana,
ReplyDeletekuhusu mambo ya kodi ni hivi,
91). TRA hawatakutoza kodi kwa kifaa chochote ambacho umekuwa ukikimiliki ukiwa nje ili hali ilukaa huko kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja. hapa nina maana personal effects zako ulizokuwa nazo.
(2) hako ka usafiri kangepata tax exemption kama ungekuwa nano kwa mwaka mmoja(kakiwa kamesajiliwa kwa jina lako) na kama kataingia Tanzania kakiwa na umri wa chni ya miaka kumi. sasa kwa kuwa kana miaka zaidi ya kumi katapigwa ile kodi inayoitwa ""Uchakavu"" nyingine zitakuwa free. wenye data jamani uchakavu ni how many percent??{nilishapigwa hii tax ila sikumbuki %ge yake],
(3) mambo mengine madogomadogo utapambana na wadau wa bandarini kama ma-clerance charge nk.
Nadhani nimesaida kidogo.
kama sikosei nilimsikia waziri wa fedha ktk bajeti hii akipendekeza kuimport bila kulipakodi kwa sasa uwe umemiliki bidhaa hiyo miaka 4 na zaidi badala ya 1.
ReplyDeletekweli wewe hujaja bongo muda mwingi! unataka kuleta gari 1990 ? utakuwa peke yako mjini !! wenzio mafisadi wana malexus na mavx ya 2010 wewe unaleta 1990 !! kwanza utachafua mji wetu . kaache huko huko tafadhali !!
ReplyDeletena kuhusu hizo machine na furniture kuna kila kitu huku , wewe acha kila kitu usiache pesa tu na mkeo basi ndo uje navyo kama unaye mke ,bongo kila kitu kipo .....
Ha! mizigo yote ya nini tena chakavu, hiyo pesa ya kuvisafirisha inatosha kunua vitu vipya vingine hapa hapa bongo, kama uliondoka miaka mingi utashangaa ukija, Tatizo tu la hapa Bongo NI bei, kila mfanya biashara ana bei yake anayoitaka- Wanatukamua na hakuna anayewashikia bango.
ReplyDeleteHafu huko ulikuwa unasoma au biashara au unafanya kazi? kama uko masomoni na hapa bongo we uliondoka ukiwa teacher utapitisha ka mkoko kako free, lkn kwa kuwa ni ka zaman utalipa ya uchakavu ambayo ni bora kununua nyingine lkn used.TRA Wanakamua kweli kweli ingawa zikienda serikalini hazitoshi kwa maendeleo.
Sasa kaka kwa nini unarudi?au mkataba wa kuishi huko umekwisha? wenzio wanaoa huko huko kama mzee wa Nondoz kule marekani au una mke huku? Kama huishi huko kiichokoraa bora usirudi.
Ushahauri wa bure nyumban ni nyumban lkn panafaa kupatembelea tu na si kuishi nyumbani, lazima utakumbuka ulaya ukisha tia mguu bongo.
Kwa kuwa mchakato wa uraia wa nchi mbili unakuja, ungesubili ukalamba uraia wa bongo na huko uliko.
By MDAU.
KUJISHAUWA TU ULAYA ULAYA ...MNATUMWA KAMA PUNDA .AU MNARINGIA KUWA WAKIMBIZI NA MUKAAMUA KUJISHAUWA HAPA ?!WATU BWANA .TULIZENI AKILI KIDOGO MUANDIKE MAMBO YA MUHIMU HAPA .INAONEKA ILIKUW ABAHATI MBAYA TU KUFIKA HUKO ,WATU KAMA NYINYI NDIO INAKUWA .KUNA MAMBO TELEEEEE YA MAANA OK KIJANA
ReplyDeletemimi ningekushauri kwamba uchukue vitu vyako vya muhimu tu sasa hivi tanzania kuna vitu vingi sana na bei sio mbaya sana. Mimi pia naishi huku Marekani lakini nikienda nyumbani na vitu hasa vya umeme vinasumbua sana kutafuta vifaa vya kurekebishia umeme ili visiungue. Navyoona kama unaweza kuuza vingi uza tu ukanunue nyumbani hasa kama utatumia dola 8000 kwa kontena tu yaani ndio kabisa sikushauri hizo ni hela nyingi sana nyumbani utanunua vitu vingi tu badala ya kupotezea kwenye contena. Gari la 1990 unaweza kuliuza pia na ukaenda kununua gari nyumbani kuna magari kila mahali na bei si mbaya kihivyo. tanzania imebadilika sana. Tangulia kaka na kila la heri
ReplyDeleteDuh! Naona munamiminika tu Bongo! Karibu Ndugu yangu. Kusafirisha mizigo ni kitu kimoja, kuishi Bongo ni kitu kingine. Kuna huyo jamaa anayesema ukitia mguu Bongo tu utakumbuka Ulaya! Huyu haijui Bongo. Hapa ni zaidi ya New York. Ukifika nitafute nikuonyeshe mitaa na tunaishi vipi. Unakula kitimoto ya kuchoma?
ReplyDeleteWEWE ACHA HIZO TANZANIA HAINA RUSHWA TENA NI NCHI NZURI SANA.KAMA IMEJAA RUSHWA KWA NINI UNATAKA KURUDI? SI UNGEKAA HUKU HUKU.ACHE KUWASIFU WAZUNGU HAWANA LOLOTE TENA NI WABAGUZI WAKUBWA.WATANZANIA WENZANGU TUINENEE MEMA NCHI YETU ILI MUNGU AZIDI KUBARIKI
ReplyDeletehuu ushauri wa wadau umu mie hoi tih tih
ReplyDeletendugu zingatia hayo kwa makini USD 8000 ni nyingi mno,gari la 90's utalipishwa adi uchoke.nimesahau tu % gani ngoja nitafute hapa nitarudi
Tafadhali, tafadhali usitumie TZS. 12,000,000/= kukodi container ili kusafirisha furniture na machine za nyumbani! Keep your US $ 8,000 uza hako kausafiri utaongeza $ 1,000 na kuondokana na kodi kubwa ya uchakavu na uza hizo furniture utaongeza some more dollars kisha rudi zako Tanzania ukiwa na vile vya lazima tu! Kama walivyosema wenzangu vitu vyote utanunulia huku huku ukifika. Nakuambia utanitafuta unishukuru kwa ushauri wangu wa bure!
ReplyDeleteKama unavitu vyako muhimu safirisha tu.Hapa Bongo ni mchina tu.Hakuna vitu vyenye quality kama
ReplyDeleteza ulaya.HATA WANAWAKE NI MCHINA TU.HIPS MCHINA,VIUNO MCHINA.Kama una girlfriend bora uje nae tu.Hata madume ya kichina yameanza kujitokeza Sinza.
Du,huyu hajaja tz siku nyingi kweli sijui alikuwa mkimbizi?sasa kukodi container us8000 bado akitia mguu hapa kodi bandarini wanamsubiri kwa hamu hata kama personal things hazina kodi kwanza accalculate hiyo us kwa 1500 exchange rate ya sasa bongo,na hiyo gari sitamani hata kuiona maana bongo yetu kwa leo ina kila kitu kizuri ni pesa yako tuu.
ReplyDeleteKaka Said
ReplyDelete1. Nakupongeza kwa uamuzi wako wa kurudi nyumbani karibu sana bongo maisha yapo na sio kama watu wengine walioko Ulaya wanavyodhani. Kama wadau wengine waliotangulia kusema karibu home, kuzuri tu, kama ulikuwa ulaya ukisoma basi njoo na vyeti vyako, utapata kazi, kama ulikuwa ukifanya "Odd Jobs" karibu pia, kwani naamini utakuwa umeserve vya kutosha kuja kuanza maisha, hapa bongo utafanya kila biashara na utavuna pesa kweli ilimradi biashara zako ziwe halali.
2. Kuhusu kusafirisha mizigo nakushauri kama ulivyoshauriwa na mdau fulani hapo juu, nunua Contena lako pakia vitu vyako ulivyokuwa ukitumia huko, HUTACHAJIWA KODI. kwa hilo gari lako ambalo ni la mwaka 1990 vivyo hivyo pakia katika kontena lako kama halijachakaa sana. Hapa TRA utalipa Kodi ambayo ni 0.75% x Bei ya kununulia gari + kulisafirisha kwa bei za biashara inaitwa (CIF).Mfano sisi tunaoagiza magari kutoka Japani kama nimeliagiza hadi kulileta hapa CIF yake ikiwa ni USD 5000 na kama ni mwaka 2000 kurudi nyuma basi Uchakavu huwa inapigwa 0.75% x USD 5000. Bandarini utalipia kitu kinaitwa Wrapage Ambayo ni $70 na Portcharges ambayo ni kuanzia 300,000/= TSH. mizigo yako ni bure labda tu kama mijitu ya Bandari itataka pesakidogo basi jiandae pia kwa hilo.
3. nimekushauri hivyo kwa kuwa ninauzoefu na watu wa aina yako ambao wamekuwa wakisafirisha vitu vyao kurudi nyumbani baada ya masomo. hutasumbuka kihivyo . Ni kweli vitu Bongo vipo naamini hivyo unavyokuja navyo sio vibaya kuhivyo. sasa ili kuepuka kuviuza huko kwa bei ya hasara na halafu uje kugharamia kununua hapa kwa bei kubwa ni bora uje navyo. CHAKO NI CHAKO BABA SAID!
Karibu sana, umefanya busara kurudi nyumbani, maana ukiwa mbali kila mtu anaongea lake. Ushauri wangu hio gari yako ya mwaka 90 acha huko huko, maana utapalalizi kodi yake, ushauri mwingine ukifika bongo kaa macho utapata marafiki wengi wanajipanga, umeisha watangazia hivyo wanakusubiri, ukiishiwa mshiko tu huoni mtu, lakini tafakari.
ReplyDeleteKaka karibu nyumbani mwananchi.
ReplyDeleteKama unavyeti vya ulaya njoo,utapata kazi mshahara mkubwa mpaka utashangaa,tunajua jamaa wenye vyeti vya ulaya wanaanzia tsh 3,000,000 kwenda mbele,wewe tu na negotiation skills zako.Kama una cheti usije bora utumwe huko mpaka uzeeke,huku utachanganyikiwa utabaki na albamu zako za ulaya.
Achana na hako kagari na mashine za kufuria,hiko ziko kila brand na bei nzuri kuanzia laki 600,000 na guarantee ya mwaka mmoja,kimbembe LUKU-Lipia Umeme Kadiri Unavyotumia.
Hiyo gharama ya contena unanunua gari zuri tu hapa Bongo from Japani,hata mawili ukitaka moja zawadi kwa wazazi wako au mwenza wako.
Rudi kama umesoma,shauri yako kama una degree za ulaya.
Karibu ndugu yetu uliyepotea tule bata original sio hayo maplastic mliyozoea. Vafaa vya ndani visikuumize kichwa. Wewe panga hapa utaishije. una mradi au una kazi. usije ukatagemea misheni town, mwezi mmoja tu utazeeka.
ReplyDeleteWabongo bwana, Ulaya Ulaya tu! Huku ndo jikoni, bongo uani!!! Hizo range rover, BMW nk mnazozitamani huko, zatengenazwa huku babake. Nawaambia hivi, Ulaya ni ulaya tu nduguzanguni!
ReplyDeleteWe baki huko huko tu, naona umelisahau hilo jua na vumbi la bongo! labda ukirudi ukaishi maeneo ya Kituro lakini huko nako umasikini ni wa kufa mtu! Usije huku mafisadi watakuchanganya akili bure. Hao wanaosema mambo safi huku uje uwatafute huwezi hata kuwaona sura zao watakutimulia vumbi wezio wako kwenye tintedi za VOGUE zao. Kama umekusanya dolla 200,000 unaweza kuja utaweza kuishi, vinginevyo achana na hil wazo.
ReplyDeleteMi nakushauri Click hapa uwaulize maswali yako nadhani utajibiwa vizuri, maana hata mimi hupata misaada mingi tu toka hapo nikiwa na shida kuhusu kodi.
ReplyDeleteKifaduro wa Thu Sep 02, 03:27:00 AM acha hate za kijinga jinga, tatizo lako hujui kama hawa watu wana mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa letu la Tanzania endapo wakitumika vizuri.
ReplyDeletehuna lolote ushafulia wewe.
ReplyDeleteusafiri wa 1990!!! biashara ya vyuma chakavu ishaapigwa marufuku bongo. aftarol bongo kuna kila kitu - pesa yako tu.
kama ushaafulia hata kichenchede hupati; ila kama mfuko uko poa hata mke huna haja ya kuja nae maana utapata wengi.
njoo na pesa tu kila kitu utapata hapa bongo. ila ukija na uchafu ulokuwa unatumia huko ujue lazima hapa bandarini tugawane pesa.
Naungana na wadau wengine wanaosema uza hivyo vitu na huku utapata vingine. Natofautiana na wale wanaosema ukifika tu nyumbani utakumbuka ulaya kwani ni mtazamo tu wa mtu, nimeishi Ulaya nikiwa masomoni, nimerudi nimepata kazi nzuri na kwa kweli huko ulaya naenda matembezi ya training au binafsi na sikukumbuki kihivyooo.
ReplyDeleteAmua na simamia uamuzi wako.
Karibu Bongo.
WE NJOO 2 UTALIJUA JIJI..
ReplyDeleteNA KAGARI KAKO HAKO ATA DOLA MIA 5 KIUZE 2 MANA TRA HA2KUACHI..
ULIPOONDOKA BONGO ULIONDOKA KWA FUJO SAIZ WANYENYEKEA
NJE NJE NDAN POPOTE KAMIL BABU KI2 KIMIANI NJE NJE NDAN KAMA IPO IPO 2 KI2 KIMAINIIIIIII.....
ReplyDeleteWE YAONYESHA HUNA UUSIANO MZURI NA NDGU JAMAA NA MARAFKIZO WA UKU SASA SIJUI UTAWAONYESHAJE VIP IYO SURA ULIOENDA KUUZA, UKU LAZMA UUZE NYAGO NA CO SURA TENA...
TRA mmmmh!!! usiombe utalikimbia gari lako bandarin mwenyewe...
lazma tukukimbize
WE HA2KUSHAURI HATA KDOGO, KAFIE MBELE.
ReplyDeleteWADAU AO WAPO SAHII
WOTE MMENENA LAKINI DON KAFUNGA MJADALA!!!!!KWI KWI KWI KWI KWI KWI...TEHE TEHE TEHE TEHE TEHE....NAUMIA KWA KICHEKO ....MBAVU ZANGUUUU....!!!!!!
ReplyDeleteWatu wengine muache wivu. Eti bongo maisha ni mazuri!!!!!!! Watu wana maisha magumu sana. Maisha mazuri ni kwa mafisadi tu. Na muache tabia ya kujibu kitu ambacho hujaulizwa?
ReplyDeleteWewe kama ni Fisadi misha ni mazuri, lakini watu wanalala njaa, wewe unasema maisha ni rahisi tu. Mwenzetu kaomba ushauri kwa uzuri, lakini matokeo yake watu wengine mnajibu ya hovyo hovyo utafikiri mmelazimishwa kuchangia mawazo. Kama huna la kuandika ishia. Wengine ni wivu tu. Kumbe wwengine munko huko Bongo bila jaribu kuomba Visa mkakataliwa. Sasa hasira zenu mnakuwa mnaziweka kwa mtu mbaye anajaribu kuomba msaada na ushauri. Acha acha wivu. Tutakiane mazuri. Naomba Michuzi mawazo mengine usiwe unayaweka kwani yantia kichevu chevu na kinyaa. Na wewe wenyewe unajua kabisa mtu ameomba msaada, lakini bado unaendelea kutundika uchavu wa watu wengine ili wausome. Weka weka mawazo yenye kuleta ufanisi bora. Sio haya matapishi mengine ninayoyasoma humo kila siku. Inabid uwe unaangalia cha kuweka na cha kuacha. Hakuna mtu ambaye ana mtu ya kusoma utumbo wa mawazo tunaousoma humu. Matapishi mengine hayana koma wala semi colon, kitua cha kufunga sentensi. Weka mawazo yanayofanana na kitu kilichoulizwa.
Mdau Kariakoo
Kijana pakia mizigo yako yote na gari lako kwani kodi ya uchakavu nakumbuka kwa marcedes benz ya 1996 c180 elegance nililipa shs milioni moja karibu na laki tatu, vitu vingine ni free, hakikisha gari umekaa nalo mwaka mmoja, kontaina uliza kwa agent uko nchi gani jaribu kunipigia simu kwani kontaina huwa ni mali ya shiping line, ukipakia tuma documents for clearence agent iwe iwe rahisi kuondoa mizigo bila kulipa malipo zaidi, simu yangu ni +447529681411.
ReplyDeleteShukurani
big up baba said, una busara sana na unajua maisha ni nini. kuna watu humu wanatia kinyaa, inakera sana mtu anaomba ushauri halafu jitu zima linakaa kwenye computer na kuandika upupu. ina maana humu ndani hakuna mtu ambaye amewahi kuomba ushauri kwa mtu? hivi ukijibiwa pumba unakuwa katika hali gani? jamani watu jifunzeni kuwa wastaarabu, baba saidi God bless you na wadau wengine wenye utu
ReplyDeletewe don, umepinda kinoma ha ha haa!
ReplyDeleteiyo gari 20% (nimerudi kukupa jibu)
ReplyDeleteNakubaliana kabisa na mdau hapo sep 02, 07:05:00 Pm Kaka said pakia vitu vyako ktk meli njoo navyo uchakavu utalipa ila sio mkubwa kihivyo kama nilivyokuelekeza hapo juu Ma AA. watu wanakushauri ila hawana data kamili wala taarifa sahii zingati awetu. Kalaga bahooooooooo
ReplyDeleteMimi Ma AA
Kaka Napenda kukufahamisha kwamba unafanya jambo zuri kurudi nyumbani, unaongeza miaka yako ya kuishi kwa kiwango kikubwa sana. Zaidi ya hilo najuwa umejifunza mengi kama ukiweza kubadilihsa maisha kijan mmoja utakuwa umefanua kazi kubwa sana. Kuhusu vitu vyako na usafiri piga simu karibu na PORT yoyote uliyo karibu nao na watakupa Agents zaidi ya mmoja kazi kwako kuongea nao na kujuwa uasfiri utakuwa kiasi gani. Nakuhakikishia kama upo USA 40Ft container siyo zaidi ya 4,000. Nakushauri usitupe kitu hata kimoja beba kila kitu na ongeza zaidi hakikisha container imejaa kila kitu. Ungekuwa na Email ningeweza hata kukupatia mtu wa kukusaidia ukifika TZ. Vitu ulivyonavyo ni imara kuliko unavyofikiria, Kidokezo ni kwamba hata plastic ya kuweka maji ni imara unayotumia hapo ulipo kuliko utakayopata Tanzania. Usisahau vitu vya ndani vya ujenzi hata kama ni vichache kiasi gani bado Nyumbani ni vingi lakini feki. KIla kitu nyumbani kuna Feki na vya kweli na hujui kipi ni kipi. Ulizia Port yoyote ilio karibu na wewe na utapata msaada watkuletea conterner nyumbani, halafu kuhusu kupakia gari yako itabidi uende port ukaiweke kwenye container or kama haupo karibu na port watakupeleka mahali ambapo utapakia mizigo yako. Usisahau kununua small transforma ya kubadilisha units za umeme. Angalia kwenye internet na nunuwa huko huko ulipo kuna ambazo ni nzito kg 5 na kuendela. Zitakusaidia sana. Please usiache kitu hata kama unaona kimechakaa bado ni imara wewe beba, kwani hapa nyumbani vitu vipo vinagaa lakini hakuna uaminifu dukani.ni utapoteza pesa yako tu.
ReplyDelete