Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dk. Mohamed Gharib Bilal akishuhudia waliokuwa kambi mbili tofauti wakati wa kura za maoni waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea Jimbo la Tunduru Kaskazini, Omar Karola (kushoto) aliyekuwa wa pili katika kinyang’anyiro hicho na mshindi ambaye ni mgombea wa jimbo hilo kwa sasa, Eng Ramo Makani, walipokuwa wakipatana na kuvunja kambi zao wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Nakapanya jana.
Wananchi wa Kijiji cha Nakapanya Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma, wakifurahia na kumshangili Mgombea Mwenza wa Urais.Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiingia kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kwanza wa kampeni baada ya kuingia mkoa wa Ruvuma.

Mimi naona mpiga picha aliwaambia wanyanyue mikono juu, maana huyo siyo ile mikono inayonyanyuliwa kwa kushangilia kitu/mtu. Kazi kweikwei!
ReplyDeleteWana CCM wenzangu, tukaze buti! Uzi ni ule ule. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM.
ReplyDeleteHONGERA ENGENEER MAKANI NATUMAI UTATEKELEZA AHADI ULIZOAHIDI WANANCHI WAKO. KILA LA KHERI
ReplyDelete