Ndugu wadau,

Napenda kuwakumbusha tu kwa wale ambao wana nia na mipango ya kusoma ughaibuni kwa kupata udhamini toka katika vyuo husika au serikali za nchi husika, huu ndio muda wa application. Kwa wanafunzi wa kimataifa, mfano kutoka Tanzania kuja kusoma Marekani, Ulaya nk muda wa ku-apply huanza September – December kwa niaba ya kuanza mwaka mpya wa masomo wa August 2011.

Ili kuweza kupata udhamini huo, ni vyema mtu ujipange na kuzifuatilia habari hizi za scholarships kwa makini mno. Wiki hii nime-post scholarships information nyingi kwenye Scholarship Forum yangu www.scholarshipnetwork.ning.com na Makulilo Blog www.makulilo.blogspot.com. Nakushauri ujiunge uwe member wa Scholarship Forum hiyo ili uweze kuwa unapata scholarship updates kwenye e-mail yako kila mara ninapoweka nondozi mpya huko.

Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuanzisha Makulilo Foundation www.makulilofoundation.org ambayo inakwenda sambamba na utunzi wa kitabu SCHOLARSHIPS IN AMERICA AND EUROPE: The Secrete From Makulilo, Jr. na pia uanzishaji wa The Ernest Makulilo Peace Scholarship ambayo itasaidia mwanafunzi mmoja kila mwaka kuanzia August 2012 kuja kusoma MA Peace and Justice katika University of San Diego, hapa California.

Nawatakia mafanikio mema.

Kama una swali niandikie hapa makulilo@makulilofoundation.org

MAKULILO, Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nakukubali mzee wa manondozi Makulilo junior.....yaani kama watu wengi wanaokwenda ughaibuni wangekuwa wanatupa mbinu za kutoka kwa njia maalumu na za uhakika kama shule nk, naamini tungekuwa mbali

    Wakenya wanatuzidi kwa hili, mmoja akiwa nje, anatuma taarifa za watu wengine nao waombe wapate, furaha ya wengi...ila sisi wamatumbi roho ya kwanini...mtu akienda huko ndio anataka masifa, sijui mambo ya bakora akirudi bongo...wengine ndio hata ukimtumia e-mail hajibu kabisa

    Mimi nimejipa deadline, hadi 2013 lazima niwe nimeshapata scholarship nami...nimejipanga sana inatosha

    Nimeshajiunga sasahivi kwenye Scholarship Forum yako makulilo

    Mungu akubariki zaidi na zaidi

    Boksiiiii oyeeeeeeeee

    Mudy, Dar

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru sana Mzee wa Nondoz kwa hizi nafasi unazotoa kwa Watanzania wenzako. Mungu akuongezee mafanikio mengi sana kaka.

    Pamoja Sana.

    Mtoto wa Mbwa.

    HELSINKI

    ReplyDelete
  3. KWANZA KABISA NAPENDA KUMPA HONGERA BWANA MKULILO KWA KIBARUA KIGUMU CHA KUTAKA WATANZANIA KUONDOA KITAMBAA WALICHOFUNGWA MACHONI MUDA MREFU,NASEMA KITAMBAA WALICHOFUNGWA MACHONI KWANI KUKOSA TAARIFA NI SAWA NA KUFUNGWA KITAMBAA HUTAJUA NINI KINAENDELEA MBELE YAKO AU PANDE ZAKO ZA KUSHOTO NA KULIA,MBILI NATAKA KUONGEA NA MDAU MUDY HAPO JUU,KWANZA KABISA HONGERA KWA KUPATA USONGO WA KUTAKA KUTAMBAA HILO TU LINAONYESHA ULE UGONJWA UNAOWAANDAMA WENGI UNAANZA KUKUACHA NA UNA KIU YA KUTAKA KUJUA NINI KINAENDELEA UPANDE WA PILI,NATAKA KUKUREKEBISHA KITU KIMOJA TU SIO KWELI KWAMBA WATANZANIA WOTE WAKIENDA MBELE HAWATAKI WENGINE WAJE LA HASHA,HASA KWA SWALA LA KUSOMA,NANI ATAPENDA NDUGU AU JAMAA YAKE ASIPATE ELIMU?NADHANI HAKUNA KAMA YUPO BASI NI KUMI KWA MMOJA,SWALA AMBALO NALIONA LINAZUIA WATANZANIA KUJUA KUHUSU HAYA MAMBO LINA MIZIZI,SIO TUU KWA KIZAZI HIKI BALI HATA CHA NYUMA KWANZA KABISA WATANZANIA SASA HIVI NI KAMA WANAAMKA USINGIZINI NA WATU WANAOWAAMSHA NI KAMA BWANA MKULO,SISI WATANZANIA TULIKUWA NI KAMA TUMEFUNGIWA MLANGO NDANI YA NYUMBA NA KUAMBIWA FANYA KILA KITU,KUNYA,KUKOJOA,KULA NA KILA KITU NA KWASABABU WENGI WALILIRIDHIKA NA HALI HII HAWAKUTAKA KUJUA NINI KINAENDELEA NJE,HAPA NAMAANISHA KWAMBA WATANZANIA TULIKUWA HATUNA INFORMATION YA KUTOSHA HASA KUCHELEWA KUINGIA UTANDAWAZI NCHINI KWETU,WENZETU WALIPATA MA T.V,MA RADIO LONG TIME,SISI NDIO TUMESHTUKA MIAKA YA 90 NA KUACHANA NA RTD NA KUANZA KUPATA TV NA VITU KAMA HIVYO,SO NCHI NYINGINE JIRANI ZILIPATA INFORMATION KWAMBA KUNA SCHOLARSHIPS MBELE LONG TIME MOJA WAPO NI NIGERIA NA HUSUSANI WEST AFRICA NZIMA SISI WABONGO TUMEANZA KUSAFIRI JUZI JUZI WALIOKUWA WANASAFIRI NI MABAHARIA NA VIONGOZI TU FULANI FULANI AU UPATE BARAKA ZA MWALIMU UJE KUSOMA JNE NA NI KUMI KWA MMOJA NA WAO WOTE WALIPELEKWA NCHI ZA KIJAMAA KAMA RUSSIA,CHINA N.K...TUNA KAZI KUBWA SANA YA KUAMSHA WATU ILA SERIKALI NAYO INALALA KIDOGO HUDUMA KAMA ZA MAWASILIANO ZIFANYWE KUWA RAHISI SIO KAMA ILIVYO SASA,MTU HUWEZI HATA KUWEKA INTERNET NYUMBANI KWAKO IT'S TOO EXPENSIVE KULINGANISHA NA MAISHA YA WATANZANIA WENGI,NA HUDUMA KMA HII NI MUHIMU SANA HASA KAMA UNATAKA KUTENGENEZA TAIFA LA WASOMI WAZURI MAANA LEO HII NAONGEA KILA KITU KIPO ONLINE HATA UKITAKA KUJIFUNZA KUTENGENEZA NUCLEAR UTAPATA ELIMU KWENYE INTERNET.
    SO NDUGU YANGU MUDY SIO KWAMBA HATUPENDI NYIE MJE ILA SYSTEM ZETU PIA MBOVU MIMI NITAKWAMBIA KUNA CHUO UK ILA KINATAKA UTUME MAOMBI KWENYE MTANDAO,WEWE MWENZANGU NA MIE HUJUI HATA INTERNET NI NINI.UNAONA KAZI HIYO,MSHUKURU MUNGU WEWE UNAJUA INTERNET NI NINI,MWENZAKO WA KULE KIJIJINI KWETU MUHEZA TANGA HANA HATA MOJA,SASA HAWA TUTAWAFIKIAJE?KUNA KITAMBAA KIMEFUNGWA MACHONI MWA WATANZANIA KINATAKIWA KIONDOLEWE.ASANTE NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  4. Job Title Swahili Language Instructor - Local or Virtual Positions
    Job ID Number 173071
    Company General Dynamics Information Technology
    Location Annandale, VA
    Job Category Installation, Maintenance, and Repair
    Job Description General Dynamics Information Technology is a top-tier IT integrator that provides information technology, systems engineering and professional services to customers in the defense, intelligence, homeland security, federal civil and commercial sectors. With approximately 17,000 professionals worldwide, the company has the customer knowledge, domain expertise and proven performance to manage large-scale, mission-critical IT programs.

    NOTE: Work locations for this project will vary, with the possibility of working at a government site in Montgomery, AL; at an off-government company site in the National Capital Region; or working virtually / telecommute. Positions are Part Time 30 hours per week with benefit options.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...