
wawekee wadau taarifa hii ya mtanzania mwenzetu alieshiriki mashindano ya mbio za baiskeli a.k.a injini kiuno huko Helsinki nchini Finland.
Mtanzania pekee aliyeshiliki mashindano ya baiskeli ya Tour De Helsinki huko Finland ashika namba tatu kati ya washiliki 1800 walioshiliki mashindano hayo.
Akitumia baiskeli aina ya Bianchi aliweza kutumia masaa 3.41 kwa kilomita 140 za mashindano hayo.
Akiwa mtu mweusi pekee aliyeshiliki mashindano hayo wazungu wengi walishangaa kwa kuweza kwake kushiliki na kufanya vizuri kwani historia inaonyesha mchezo huo wa baiskeli unapendwa sana na wenzetu wazungu.
Anajitayalisha sasa kwa Tour de France hapo mwakani.
mdau
Helsinki
Hii imekaa vizuri. Je, ana timu ya kushiriki Tour de France? kwani kule hawapokei indivual washiriki. Afu inabidi ajifue kweli, siku 21 za cycling si mchezo.
ReplyDeleteNitatizama Tour yote mwakani kwa ajili yake.. kwani hiyo ni sababu tosha.
Hongera zako kaka mshiriki zikufikie popote ulipo, pia asante kwa kupeperusha bendera yetu.
ReplyDeleteHuyo Mbongo wa Helsinki hana jina?
ReplyDeletembona hujaweka jina ni mbongo kweli au mbantu tu huyo?
ReplyDeleteJINA LAKE NA NI NANI ANAFANYA NN?TOA HABARI KAMILI BASI KAMA UNATAKA KUTOA HABARI.
ReplyDeleteHongera 'Mbongo' kaza kamba mwanangu!
ReplyDeleteMdau tunaomba jina lake kwa kumbukumbu.
Wwe mdau wa Helsink. Hiyo siyo taarifa kamili. Huwezi kueleza mambo hayo yote kisha ukasahau kutaja jina la mshiriki. Sweden kuna Wwatanzania maelfu kwa maelfu.Tungejua jina ingesaidia sana, huenda kwa wengine ni mtu wa karibu sana nao na kwa hiyo wanahitaji kumpongeza zaidi. Kama huwezi kutoa taarifa iliyokamilika, ni bora ukaacha.
ReplyDelete...Kwa Jina Anaitwa.. MARTINEZ MUNGU MTEFU...
ReplyDeletewashiliki, walioshiliki, aliyeshiliki na anajitayalisha.....mdau wa Helsinki wee noma....L na R kwako tatizo. Anyways thanx for the information
ReplyDeleteKuna umuhimu wa kujua jina na maelezo zaidi ya Mtu huyo, ushindi wake ni muhimu kwake binafsi na kwa taifa kwa ujumla.
ReplyDeleteLink hii inaonesha majina ya washindi wote, ila sijui jina la huyo mshindi mwenyewe
http://www.tourdehelsinki.fi/en/results/results-2010/results-2010-men
MAKULILO
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
www.makulilofoundation.org
huyo anonymous namba mmoja si ungeshiriki ,michuzi usiwe unawakawisha watu kama hawa, ujuwaji mwingi lakini hamna. hayo yote anajua , mpe hongera funga mdomo kitu. mimi hii mijitu inayojifanya inajua sana mambo ya mamtoni inanishangaza sana. si ungeshika namba mbili. kila mtu anajua, funga mdomo . hongera kaka yetu ubarikiwe ,kila la kheri
ReplyDeleteHuyo jamaa anaitwa Ahmada..mwejeji wa morogoro misufini mdogo wake ni Adam a.k.a Pendolino..he is next Chris Amstrong wa Tanzania.
ReplyDeleteMdau Finlad
Mhhh nina wasiwasi kidogo na habari hii. Huyu mshindi wa tatu jina lake ni Joonas Hentalla. Hili jina kwa asili yake ni la kifini. Je huyu jamaa utanzania wake kaupata kwa kuzaliwa bongo au kwa kuhamia bongo au mmoja wa wazazi wake ni m-TZ na yeye akaamua kuwa M-TZ??? Maana wapo jamaa wa namna hiyo nawafahamu mfano ni jamaa anayetumia jina la Majani au P-Funk, pia kuna jamaa anaitwa Umande. So unaweza kutueleza zaidi juu ya huyu jamaa??. DJ EZZA na brother WAGADUGU hebu tufahamisheni hizi habari maana ninyi mko hapo hapo.
ReplyDeleteNdiyo maana hakuweka jina mtu mwenyew anajiita Mungu. Halafu Martinez sio jina common Tanzania ingawa tuna Magoa wengi.
ReplyDeleteFIKSI TUPU!.Matokeo ya Tour de Helsinki 2010 kwa wanaume haya hapa kwenye linki hii:
ReplyDeletehttp://www.tourdehelsinki.fi/en/results/results-2010/results-2010-men
Kam unashindwa kukopi na kupesti tafuta tour de helsinki kwenye google
KWA JINA ANAITWA AHMADA SILVER... alishawahi kushinda pia morogoro tour 1984...
ReplyDeleteMdau Kontula
Jamaa kachanganya,martin Mungu mtefu alishika nafasi ya 3 kwenye mashindano ya kunywa olut na kung'oa
ReplyDelete