Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Zanzibar
Serikali ya Uingereza imetoa kiasi cha bilioni 240 sawa na Paundi milioni 103.5 kwa ajili ya kuchangia Bajeti ya Tiafa (GBS) kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo na Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen O’Brien.
wakati wakitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari mjini Zanibar.
Mkulo alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kutekeleza vipaumbele katika kutekeleza maeneo muhimu katika Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania(MKUKUTA).
Kufuatia hali hiyo ameishukuru Uingereza kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo ya Watanzania.
Alisema kuwa hali hiyo imejidhihirisha katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Uingereza kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania wengi.
Mkulo alitaja wafadhili wengine walichangia Bajeti ya mwaka 2010/2011 kuwa ni Denmark Dola milioni 16.3, Finland Dola milioni 18.8, Norway Dola milioni 31.4 na Ireland Dola milioni 14.2.
Aidha aliwahakikishia wafadhili wote wa Tanzania kuwa Serikali itahakikisha kuwa kuna usimamizi mzuri wa misaada na fedha zote zinazotoka kwa wahisani ili kuendelea kujenga imani kwao.
“Napenda kuwahakikishia kuwa wafadhili na wahisani katika Bajeti ya Taifa kuwa fedha zitakazotolewa na wahisani zitatumika katika miradi na malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha zinazotolewa na wahisani”alisistiza Mkulo.
Kwa upande Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen O’Brien alitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuhakikisha kila kiasi cha fedha zinazotolewa na Uingereza zinatumika katika malengo yaliyokusudiwa ili matokeo yake yaweze kupimika.
NI MKOPO, AU BURE? MICHUZI UMECHOKA MKUU, FUATILIA HABARI KWA UNDANI. TATIZO LAKO UNATUMIA MDA MWINGI KUTAFUTA HABARI TAAAAAMU ZA CHAMA CHAKO
ReplyDeleteHawa jamaa nashindwa kuwaelewa, hivi wanafikiri sisi tunahitaji sana hizo hela kuliko wao wanavyozihitaji?! Sasa hivi kila kukicha wao na kupunguza matumizi, wanakata so many things ili kuziba yale mapengo yaliyoachwa na LABOUR, benefits zinaondoka VAT inapanda yaani maisha yamekuwa magumu si mchezo. Hii leo wanawaletea watanzania msaada wa fedha nyingi hakika kuna kitu nyuma ya pazia jamani waingereza ni wezi saaana!Kuna kitu wanataka kutunyoosha.
ReplyDeleteDr Shayo na bwana Danny Mwasandube Hongereni kwa kupata nafasi ya kuongea na Waziri wa Uingereza, mara tu baada ya kuongea na Mh. Pinda waziri mkuu wa Tanzania nyumani kwa muwakilishi wa uingereza.
ReplyDeleteKwa kweli sasa nimekubali kuwa kurudi kwenu Tanzania kumekuwa chachu ya mawazo mapya.
Kumbe tulipokutana nyumbani kwa balozi wa UK zile issue ulizokuwa unazijadili zilikuwa zinalenga mambo haya?
Wana "diaspora" mkirudi Tanzania au mrudipo nyumbani msipotee jichanganyeni na tunahitaji michango yenu
Hongera Dr shayo, hongera Dany Mwasandube!
Achana na misaada. Soma kitabu kwa jina:
ReplyDelete"HOW TO BE RICH IN AFRICA & Other Secrets of Survival" by Alfred Mutua
...au munakubaliana na msemo kwamba ukitaka kumficha Mtizii kitu kiweke kwenye kurasa za kitabu??
Else, tutaendelea kupiga picha za kupokea misaada as if ni tafrija ya maana mpaka yule atakaporudi!!
Kuna jambo alilisema mwanamapinduzi Che kuhusu waafrika, next taimu itabidi niliseme kama hali ikiendelea hivi!!
Till when we will continue being beggars????
ReplyDeleteWe have every resources other nations would envy and yet, we happily report other nations are contributing to our budget.It's like your neighbour deciding to pay your house bills amongst other bills.
We need to be serious!
Waengereza Mafisadi tu Michango yao ni Rushwa wanachangia hivyo ili wapate wanachokipata hapo Baadae,
ReplyDeleteWanafanya hivi ili mkitaka kutokubaliana nao waseme tuliwasaidia kwanza tunawadai madeni mengi ya Ukoloni.
Uengereza kwanza wanaiba Pesa za Visa kibao Tanzania tumejisaidia wenyewe pesa za waliokosa Visa tu hizo Nani ananiunga Mkono? Michuzi naomba usibanie.
James.
wewe michuzi una bore mbona comments upost ama kampeni ya jk hina kukipi busy sana!!
ReplyDeleteHapa sijafahamu huyu waziri wa Muungano ameenda kufanya nini ZANZIBAR au kwa vile ndio kuna kitika,naona Wazanzibari sasa watu weupe namisaada inamiminika tu,tokea muafaka,lakini sasa hayo mapesa yanafatwa huko huko visiwani-eh haizuru waziri wa Muungano lakini hii sijapata kusikia hata siku moja hata waziri wa kilimo kutembelea Zanzibar,ukweli useme hayo mabilioni yalikua yaende zanzibar kama kungekua naserikali 3 lakini mh-
ReplyDelete