
Familia ya Profesa Tolly Mbwette inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wanajumuiya wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania popote walipo.
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) majirani wote wa Kimara “B” Mavurunza, marafiki,ndugu, na jamaa wote kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia katika kipindi chote cha msiba wa Mpendwa Mama yetu, marehemu Rozina Mbwette.
Ushirikiano wenu ulituwezesha kumlaza mama yetu mpendwa katika nyumba yake ya milele huko Irambo, Mbeya Jumapili tarehe 12 Septemba 2010.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI
Poleni sana familia ya Prof Mbwette na Majirani wa Hapo Marurunza - SUCA MOTEL. Ni pigo kubwa sana kwenu, lakini Mungu amempenda, akamchukua.
ReplyDeleteMarko,
USA