
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA wametakiwa kuongeza ushindani kwenye soko la pamoja la Afrika ya Mashariki ilikuweza kupanua wigo wa kibiashara katika masoko mengine ikiwemo COMESA na SADC.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya viwanda na biashara yalioandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na East Africa Speakers Bureau (EASB), jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee,
Katibu mkuu wa Jumiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu alisema kuwa changamoto ya watanzania iliyopo ni kujituma kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa ilikukidhi masoko ya nje ya Afrika ya Mashariki.
Mwapachu aliwapongeza CTI kwa maonyesho hayo ambayo yanatalajia kukuza wigoo wa biashara nje ya Afrika ya Mashariki. “Tunahakika maonyesho haya ni changamoto na yatavutia zaidi wawekezaji wengi na hata sisi kupata kuingia kwenye biashara ya ushindani katika masoko ya SADEC, COMESA na masoko mengine nje ya Afrika” alisema Mwapachu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CTI, Felix Mosha kuacha uoga na baadala yake kujituma ilikukuza na kuinua soko la ushindani ambalo litakuwa chachu kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa pamoja.
Maonyesho hayo yanajumulisha wadau mbalimbali wakiwemo wajasiliamali wadogo na wakubwa pamoja na makampuni ya bidhaa kutoka katika viwanda vya Afrika Mashariki yataendelea kwa siku tano ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kitu ambacho sikielewi kama mjasiriamali ni hiki:
ReplyDeleteJe mie kama mjasiriamali naweza kufungua kampuni yangu nchi yoyote ya Africa mashariki na kama ndio lipi linahitajika?
Vile nimeona watu wengi wamekua wakizungumzia kupata ajira na ni wachace wanazungumzia kutengeneza ajira!
Sisi tunataka kutengeneza ajira kwa kufungua biashara sehemu mbalimbali, zipi ni fursa na changamoto?
Kikore
Kilimanjaro