DAWASCO inawatangazia wateja wake katika baadhi ya maeneo kwamba,kutakuwa na zoezi la kubadilisha Valve katika Matenki ya Terminal yaliyopo maeneo ya Chuo Kikuu.

TAREHE; 17 -18 /09/ 2010.

MUDA ;Siku mbili (2)

SABABU; Ubadilishwaji wa valve zilizochakaa na kuweka mpya.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA; Ni pamoja na chuo cha ardhi, chuo kikuu cha Dar es Salaam,Lugalo(sehemu ya jeshi) Mlimani City,Mlalakua,(Survey) Coka cola,Sinza,eneo la Sam Nujoma, sehemu ya Ubungo,(NHC) Mabibo,Kigogo,Buguruni pamoja na maeneo ya jirani.

DAWASCO inawaomba wananchi wa maeneo hayo yaliotajwa kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi katika kipindi hicho ambacho matengenezo yatakua yanaendelea na hivyo kusababisha upungufu wa maji kwa muda wa siku hizo mbili.

Huduma ya maji itarejea katika hali yake ya kawaida baada ya muda huo.

DAWASCO inawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Isaidie DAWASCO kwa kutoa taarifa za uvujaji na kwa kulipa bili yako ya maji kila mwezi ili iweze kutoa huduma bora jijini.

DAWASCO

Tutakufikia.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
DAWASCO
Simu:0762979627

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. My goodness!! 2-days???

    ReplyDelete
  2. Sasa hawa wanamtangazia nani? mbona maji yao tumeshayasahau siku nyingi sana(1980s).Siku zote tunatumia visima vyetu tulivyochimba wenyewe,naona mnatuyeyusha dawasco

    ReplyDelete
  3. wadau wa majuu rudini nyumbani kila kitu kipooo!!

    ReplyDelete
  4. wapuuzi DAWASCO,maji yenyewe hajawahi kutoka tangu nizaliwe Makongo Juu,halafu mnatoa tangazo.
    Maji ya wachina imekuwa mapambo.
    I REAL HATE DAWASCO.

    ReplyDelete
  5. Hawa DAWASCO wameshindwa kazi inasikitisha hata sehemu kama Masaki hamna maji unategemea nini? Nafikiri umefika wakatio wa kuleta mabadiliko ya kweli. Hawatufai DAWASCO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Yaani hawa Dasasco sina hamu nao wametufungia line zao za kichina maeneo ya kimara, bomba kubwa linapita haizidi mita 300 lakini maji hatupati, dawasco hawafai ni bora wangebaki wale wazungu wangetupatia maji hawa waswahili wenzetu wameigeuza NGO yao, maji kwa wateja hayatoki ili wauze wao kwenye magari....ufisadi tu!

    ReplyDelete
  7. Sawa tutawasaidia lakini na nyie DAWASCO mmezidi rushwa hata ukiripoti jambo lolote mnalifumbia macho. Valve hizo mnazosema mtakuja kufunga maeneo ya kimara matete barabara zimeharibika kutokana na kuvuja kwa maji ya mchina kwa hiyo hii imeshaonekana kuwa ni jambo la kawaida.Sijui mtajirekebishaje kurudisha imani kwa watu.

    ReplyDelete
  8. TUNAKARIBIA MIAKA 50 YA UHURU LAKINI BADO HUDUMA MUHIMU KTK MJI MUHIMU KAMA DAR BADO SI ZA UHAKIKA.WANANCHI HUU NI WAKATI WA UCHAGUZI...MNAWEZA BADILISHA HAYA YOTE KAMA MKIWATOA MADARAKANI KWA KUPIGA KURA WATU WALIOLIPOTEZEA MUDA TAIFA LETU(CCM) NA KUWEKA MWINGINE NAE KAMA HAWEZI TOA MPAKA TUTAPATA MTU MWENYE UCHUNGU NA MCHAPA KAZI KTK NCHI HII....

    ReplyDelete
  9. BONGO TAMBARAREEEEEEEEEEEE.SIRUDI MPAKA WANIPANDISHE NDEGE HUKU WANANITISHIA BASTOLA.SHIDA ZA MAMUTONI SAWA NA RAHA ZA BONGO.POLENI WALALA HOI NA MNAORUDI KWA KUKURUPUKA AKILI ZENU KICHWANI.HUKU TUNALALA HOI KWA KUPIGA BOKSI LAKINI MAJI NA UMEME MASAA 24,SIKU 7 ZA WIKI NA MIEZI KUMI NA MBILI YA MWAKA.USAWA NA HAKI MTAVISIKIA TU REDIONI NA KWENYE TV.POLEENI.

    ReplyDelete
  10. Home Sweet Home.

    ReplyDelete
  11. Kura yako itasaidia kuliko ulalamika, kila kitu kipo kwako tumia muda wako kwenda kupiga kura , usisahau kupeleka kijiji chako chote kuchaguwa unaeona atbadilisha hizo rushwa na huo uzembe. Kumbuka msaada hauji bure, wajukuu zako watalipa kama vipe tunavyolipa kwa sasa.

    ReplyDelete
  12. DAWASKIO ni kwamba maeneo ya Mwananyamala Ujiji na kwingineko watu wanakata mabomba na kuchota maji, wakimaliza wanafunga kwa mipira maisha yanaendelea, naomba hili suala mlifanyie kazi.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...