Tunasikitiza kutangaza kifo cha Pr. Joseph Shem Onyango (pichani) Kilichotokea jana mchana Kihonda, Morogoro kutokana na ajali ya barabarani. Mchungaji alikuwa akielekea kwenye kituo cha basi tayari kwa safari ya kwenda dar kushiriki katika sabato ya wageni jumamosi tarehe 18.9.10 kwenye kanisa la Tegeta.

Marehemu alizaliwa 1936 na amekuwa akilitumikia kanisa la waadeventista wasabato kwa zaidi ya miaka 40, Pr. atakumbukwa sana na watu wengi africa mashariki kutokana na huduma zake kwenye kanisa za kaya na familia pamoja na sera za ndoa.

Mazishi yanategemewa kufanyika alhamisi mji wa morogoro.

Asanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nasikitika sana huyu mchungaji alinibatiza nikiwa Bongo Tanzania!

    ReplyDelete
  2. Poleni familia ya pastor nilimjua kwa miaka mingi na alikuwa mchungaji mzuri

    ReplyDelete
  3. Pole kwa wanafamilia wote,na kwa wasabato duniani kote.Mchungaji Onyango ame-achapengo lisiloweza kuzibika.Mimi binafsi yeye ndiye alie ni batiza.Nimepokea habari hii kwa majonzo makubwa.

    ReplyDelete
  4. Mchungaji Onyango, tunashukuru kwa kazi na utumishi wako uliowagusa wengi. Tunashukuru pia kwa kutuachia mfano mzuri wa jinsi ya kufanya kazi ya Bwana.

    Natoa pole kwa familia yako, ndugu, jamaa na marafiki. Na pia kwa familia ya Wasabato popote walipo duniani.

    Shukurani zimrudie Bwana wetu.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Paul na Baraka Onyango na ndugu wote. Lo hilo ni pengo kubwa. Bwana ndiye aliyetoa na bwana ametwaa. Amina.

    ReplyDelete
  6. POLENI WAFIWA WA MJI WA KUSOMA PAUL, EUNICE, BARAKA NA WOTE. MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

    ReplyDelete
  7. Nawapa pole wafiwa. Nilimheshimu Pr Onyango kutokana na uhusiano mzuri aliokuwa nao na watu wa dini nyingine. RIP. Ahmad M.DSM.

    ReplyDelete
  8. SENDING YOU DEEP SYMPATHY PAUL AND YOUR FAMILY.brigid

    ReplyDelete
  9. R.I.P "mzee wa sera za ndoa"

    ReplyDelete
  10. MCHUNGAJI ONYANGO AMEMALIZA MUDA WAKE NA ATAKUMBUKWA KWA KUPONYA NDOA ZA WATU WENGI. JE WEWE UNAYESOMA HAPA UTAKUMBUKWA KWA LIPI SIKU ILE UTAKAPOLALA MAUTI?

    ReplyDelete
  11. Nimeguswa sana na msiba wa Mzee wetu Onyango. alinibariki sana katika Sabato ya wageni Ubungo Hill miezi michache iliyopita, Kweli nimeumia sana ila jambo moja naamini "Tutakutana naye katika asubuhi njema" Mike Mchome

    ReplyDelete
  12. Sisi tulipenda sana ila Mungu amempenda zaidi Mtumishi wake Pr Onyango tuache utani nilikuwa na barikiwa sana neno la Mungu alilokuwa analitoa mtumishi wa Mungu nadhani ni mfano mzuri kwa kufuatwa.

    ReplyDelete
  13. Paul, pole sana rafiki yangu

    ReplyDelete
  14. Nimeshtushwa na hizi habariza msiba wa pr. Onyango.Alihusika kwa kiwango kikubwa katika maisha yangu tangu nikiwa mdogo ki umri na mchanga katika imani hii ya kisabato. Hakuishia kunibatiza tu, bali alikuwa mchungaji, baba,na rafiki yangu mkubwa ambaye kila ninapoongea naye iwe kwa uso, au barua, au kwa simu, nilijihisi upendo wa hali ya juu ulio jaa faraja na wenye matumaini makubwa katika maisha.Ni mzee ambaye nilimpenda sana.Ppr. Onyango, amekutwa na mauti katika kipindi kinzuri akielekea kufanya kazi ya kuokoa roho za watu wamuone Yesu, hivyo niimani yangu kuwa siku anafufuliwa atanyakuliwa na bwana Yesu mbinguni. Poleni sana mama na familia nzima ya pr. pamoja na waumini wote wa sabato duniani, na wamadhehebu mengine pia, kwani huduma aliyoitoa ilifaa na kunufaisha maisha ya watu wa dini zote hasa mambo ya ndoa na kumjua yesu. ahsanteni mungu awabariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...