MPIRA UMEISHA NA TAIFA STARS IMETOKA DROO YA 1-1 NA ALGERIA KATIKA MCHEZO WA MGUU WA KWANZA KUTAFUTA KUFUZU KUCHEZA FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA. TAIFA STARS IMECHEZA KUFA NA KUPONA NA KUTANDAZA KANDANDA SWAFI MBELE YA MASHABIKI WA ALGERIA AMBAO WANAJUTIA NAFASI KIBAO WASHAMBULIAJIA WAO WALIZOKOSA HASA KATIKA KIPINDI CHA PILI WALIPOFUNGA KAMBI NUSU YA UWANJA UPANDE WA TAIFA STARS - HUKU WAKIBEBWA NA REFA AMBAYE ALIONGEZA DAKIKA 7 NZIMA ZA MAJERUHI AMBAPO WAMANGA HAO WALIPATA KONA KAMA NANE HIVI MFULILIZO LAKINI WAPI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. UNAPOSEMA WAMANGA JUWA UNAWATAJA WAOMAN. JARIBU KUTAFAUTISHA KATI YA NENO WAARABU NA WAMANGA.WAALGERIA NI WAARABU LKN SI WAMANGA. KAMA VP MUULIZE MWANA LIVERPOOL MWENZIO FAROUK KARIM AKUFAHAMISHE NANI HASA MMANGA

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana vijana wetu. Bao la Ugenini lina Raha yake. Karibuni nyumbani tumalizane na wamanga kwetu hapa hapaaa

    ReplyDelete
  3. ingawa kipindi cha pili timu ye2 ilipoteana,na beki zetu za pembeni kuzidiwa speed na wings za wapinzani, golikipa shaban kado alikua ndo shujaa wa mchezo huo lait angekuwepo maximo na kutuwekea golikipa wake mwalami mbona tungepigwa goli kama 5 hivi!big up coach!!

    ReplyDelete
  4. si vibaya kwakuwa tumepata pointi lakini kimchezo tulizidiwa sana hatukushambulia kutafuta ushindi kwa jinsi nilivyoangalia pambano hili laivu wachezaji wameendelea kutumia mfumo wa maximo wa kujihami????big up kwa kutumia vyema free-kick

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana Staz kwa fighting spirit yenu. Binafsi nimeridhishwa kiasi japo kuna marekebisho kidogo hasa kwenye kupiga through balls, accuracy of passing, stamina na kucheza high balls. Kwa kipa kajitahd ila umakini kwenye timing ya kutoka imarisha sana hapo. Yote kwa yote huu ni mwanzo mzuri kwa Paulsen tunasubiri mazuri zaid

    ReplyDelete
  6. HALAFU INAHUSU NINI MAMBO YA MPIRA NA KUKASHIFIANA?UMANGA UNAHUSIANA NINI NA MPIRA? MBONA MNAINGIZA DHARAU KWENYE BLOG YA MICHUZI?.
    MAMBO YAMEPITWA NA WAKATI HAYO.

    ReplyDelete
  7. saafi sana taifa stars really mmejitahidi innshallah mungu ibariki tanzania nasi tuonekane ki michezo mdau ugiriki! angalau refa amewababa tosha

    ReplyDelete
  8. safi sana vijana wamejitahidi ingawa tulizidiwa sana,with a little bit of quality wi culd av nicked it in the end,all in all not a bad start,aaf yule refa sijui katokea wapi,kama ni ulaya asinge pewa mechi nyingine yoyote,sasa ni kuweka mikakati kushinda mechi zote za home!

    ReplyDelete
  9. Nyie mnaosema wamanga ni waomani toeni uongo wenu WAMANGA NI WAGIRIKI - WAARABU WOTE NI WASHIHIRI TU WAWE WA OMANI AU ALGERIA - HIYO NDIO DEFINITION YA NENO UMANGA- MSIONGOPEENI-WAMANGA NI WAGIRIKI.
    CHA KUSHANGAZA VYOMBO VYA HABARI VYA NJE VIMEANDIKA INTERNATIONAL FRIENDLY NA SIO QUALIFICATION-MARA YA PILI MPIRA UNAONESHWA LIVE www.myp2p.eu KWA YOYOTE ANAETAKA KUONA LIGI ZA DUNIA NZIMA (MDAU UMANGANI)

    ReplyDelete
  10. Nyie wamanga cha muhimu hapo ni mpira sio hilo jina lenu la Ubatizo.Acheni kutukata steam na hizo comment zenu za kishamba.tokea muanze kutumia mtandao basi full makelele.waarabu wako uarabuni mliobaki wote wamanga tu.

    ReplyDelete
  11. Hongera Vijana!!

    Najiuliza kitu kimoja, kwamba waarabu wana mbinu nyingi nje na ndani ya uwanja. Ni kweli ukiangalia mchezo kuna vitu vingi ambavyo ni wajanja kucheza na refa. Na refa wa jana nafikiri sio mjanja kugundua mbinu potoshi za wachezaji!!

    Je, hizo mbinu vijana wetu hawawezi kujifunza?? Maana mpira wa sasa hivi sio msuli tu. Kuna mbinu nyingi ambazo inabidi tuwapatie hawa vijana.

    Maumbo ya kimchezo tayari wanayo, na sio lazima uwe pande la mtu. Angalia Messi, au timu ya Spain.

    ReplyDelete
  12. Jamani tusiongee sana vijana wamejitahidi sana ukilinganisha na kiwango cha mpira Ageria ni wakali sana na vile vile kumbukeni tumechezea ugenini,mpira wa kujihami na kitu cha kawaida haswa unapochezea ugenini hata huku ulaya timu kubwa zinapochezea uwanja wa ugenini huwa wanacheza kwa kujihami,mmesahau kuwa mcheza kwao hutuzwa?Kocha nimemkubali anaijua kazi yake na anaonekana hataki kuingiliwa anapotoa uamuzi,ameniuwa sana alivyowaacha wale wachezaji saba ambao Watanzania tulikuwa tunaamini ndiyo nyota wetu kumbe hawana lolote ubishoo tu,hawa wachezaji aliyo wachagua wanajituma sana na naamini huyu kocha ataleta mafanikio katika timu yetu ya Taifa kwasababu hataki wachezaji wenye anaangalia uwezo wa mchezaji.Hongera Poulsen

    ReplyDelete
  13. Mchawi mliyempata safari hii Taifa Stars .. i mean yule babu wa Kipemba.. mng'ang'anieni. He is good.

    ReplyDelete
  14. Hivi mfungaji wa goli la Tanzania alikuwa Abdi Kassim kweli au Idrissa Rajab? Michuzi kuwa makini, ulizia nani alivaa namba 10!

    Mzozaji

    ReplyDelete
  15. Safi sana Stars. Kama mnaweza kutoa droo na Aljeria mnaweza kutoa droo na Waingereza. Tena basi bahati yao Aljeria. Wangekuwepo Chuji na Kaseja tungeshinda mechi!

    ReplyDelete
  16. Hivi Kaseja alizuia sana mpaka Algeria ikatoka 1-1 huko jijini Algiers?

    ReplyDelete
  17. KASEJA HANA NAMBA KWENYE HII TIMU, MTAJIONEA WENYEWE. CHIPUKIZI NI WABAYA ZAIDI YAKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...