Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji kiongozi mstaafu Ramadhani Manento akizungumza na wawakilishi wa mabaraza ya watoto nchini mara baada ya kutembelea ofisi za tume hiyo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amewataka kuwa watii kwa wazazi wao na wazingatie Haki na wajibu katika maisha yao.Viongozi wa mabaraza ya watoto wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yanawasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji kiongozi mstaafu Ramadhani Manento leo jijijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Fides Shao akitoa ufafanuzi kuhusu Dawati la Watoto na jinsi linavyofanya kazi kwa wawakilishi wa mabaraza ya watoto nchini waliotembelea ofisi za Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Amiri Ramadhani Manento (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa mabaraza ya watoto nchini mara baada ya kuzungumza nao leo jijini Dar es salaam.
Viongozi wa mabaraza ya watoto nchini na wale wa shirika linalojihusisha na masuala ya watoto la "Save the Children" wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na nyaraka wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Epifania Mfundo (wa tatu kulia) mara baada ya kuhitimisha ziara yao leo jijijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI (MITAANI) WANAKOSA FURSA NYINGI ZIKIWEMO USHIRIKI WA MAKONGAMANO NA WARSHA KAMA HIZI. JE ASASI HUSIKA ZINA MPANGO GANI WA KUWANGALIA WATOTO HAWA? TUSIJIKITE KUWAANGALIA WATOTO AMBAO NI PRIVILEDGED, WANAISHI NA WAZAZI WAO NDANI YA MAJUMBA, WANAKWENDA SHULE, WANASHIRIKI MICHEZO NK IL HALI WENZI WAO WANALALA MABARAZANI MITAANI, WAKIJITAFUTIA KULA WENYEWE NA WAKIWA KATIKA HATARI ZA KUTUMIWA KATIKA KUUZA NA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA NA KUBAKWA.

    KK
    MAGAMBA COAST

    ReplyDelete
  2. ILA ANKAL MICHUZI SAFARII HII KWELI TUMEJUA RANGI ZA KILA MMOJA KATIKA FANI HII, YAANI BLOG IMESHINDWA KABISA KUONYESHA WELEDI.

    MAANA HUKU KUNUNULIWA NA NAMBARI WANI MPAKA KUTUONYESHA PICHA ZA FAMILIA WAKATI WAGOMBEA WAPO KIBAO.
    HAPA MICHUZI MMETELEZA, CCM WATAWAPELEKA PABAYA. RIDHIWAN ANAGOMBEA JIMBO GANI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...