Warembo 30 wanaoshiriki shindano ya Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipozi kwa picha kwenye gari yao aina ya Hundai i10 lenye thamani ya shilingi Milioni 12 ambalo mshindi wa taji hilo ndiye atakaeondoka nalo pamoja na kitita cha shilingi milioni 10 fedha taslimu.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza akiongea wakati wa kuonyesha gari lenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa warembo wanaoshiriki shindano ya Vodacom miss Tanzania 2010,ambapo mshindi wa taji hilo ataondoka na gari hilo pamoja na kitita cha shilingi milioni 10 fedha taslimu.
Warembo 30 wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakifungua gari lao Aina ya Hundai I 10 lenye thamani ya shilingi Milioni 12,ambapo mshindi wa taji hilo ataondoka na gari hilo pamoja na kitita cha shilingi milioni 10 fedha taslimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hapa kunahitajika maelezo...mshindi wa mwaka jana alipata gari lenye thamani zaidi ya hili kama sikosei(naomba mnirekebishe kama nimekosea)iweje mwaka mmoja baadae shindano lile lile thamani ya zawadi ishuke...mwakani used vitz!!!!

    ReplyDelete
  2. cheap ass car!!!!!

    ReplyDelete
  3. Moja kati ya Hundai 100! huyo mshindi KAPATWA maana walopita walinyakuwa Vitara Grande. Voda mteremkoooooooo!

    ReplyDelete
  4. Muhaya kakabidhiwa ma-miss......hii kitu inatisha!!!!!

    ReplyDelete
  5. He! Yaani Miss Tanzania na yeye anapewa kagari hako kama washindi wengine mia moja wa "kamata mkoko"?

    Kweli Miss Tz sasa hivi wachovu ... mi nilidhani watampa mashine ya nguvu kama mamiss Tz waliotangulia.

    ReplyDelete
  6. Duh!. Sasa kuna dalili VODACOM wana mpango wa kutema sponsorship ya haya mashindano. Kigari gani hicho cha kumpa Miss TZ. Huko nyuma wametoa magari ya maana hadi nyumba kwa mshundi wa kwanza. Iweje leo watoe hivyo vigari vya bahati nasibu. Shame an too bad for VODA. Uncle najua wanaku sponsor voda lakini usiibanie hii coment, ni kwa manufaa ya watoto wetu warembo wetu, wanaojitoa muhanga katika fani hii, ili next time sponsors wafikirie mara mbili zawadi za kuwapa

    ReplyDelete
  7. NADHANI NI WAKATI KINA LUNDENGA WAANZE KUJIULIZA MASWALI KWA NINI HADHI YA ZAWADI IMESHUKA MWAKA HUU. KIGARI GANI HICHO?

    ReplyDelete
  8. Mweeh! Mweeh! Mweeh!,

    Yaani mwaka huu wanatoa kiBajaji?!?

    Khaah!

    ReplyDelete
  9. Miss TZ ya mwaka huu hakuna mvuto kabisa sijui warembo hasa ambao wangekuwa Miss TZ wameogopa nini waandaaji wafikiri hili suala vinginevyo ni aibu kusema hao ndo Miss Tz wkt kuna warembo hasa hasa

    ReplyDelete
  10. wadau wote hapo juu wameongea ya kweli. lakini mimi mtazamo wangu ni tofauti kidogo. yale magari ya thamani sana waliochukua warembo waliopita, naona ni gharama sana kuyamaintane, halafu kwa habari nilizokuwa nazo mimi, warembo wengi wa nyuma, wanauza magari wakimaliza muda wao. hii gari ni nzuri sana kwa kuservice na kuimaintein.

    ReplyDelete
  11. Jamani hivi vigari vinawafaa sana. Wtaoto hawa uwa wanapewa magari kumaintain kazi kweli2 bora hili kwakweli.Kila la kheri warembo wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...