
Kundi la kwanza la washindi wa promosheni ya Shinda Mkoko kutoka Vodacom Tanzania limekabidhiwa magari yao katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la Voda (Vodashop) lililopo Mtaa wa Ohio jijini Dar-es-Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru, alisema kuwa washindi wataendelea kukabidhiwa magari yao kadri promosheni hiyo itakavyokuwa ikiendelea.
Vodacom Tanzania inawapa wateja wake fursa ya kushinda gari aina ya Hyundai i10, kila siku kwa siku 100 (zaidi ya miezi mitatu). Promosheni hii ya kihistoria ilizinduliwa Jumatatu tarehe 2 mwezi Agosti mwaka huu.
Promosheni ya Shinda Mkoko ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya kuwepo kwa Vodacom nchini Tanzania. Promosheni hii itakapofika ukingoni, magari 100 yatakuwa yametolewa , kila moja likigharimu shillingi million 12 za kitanzania.
Watumiaji wote wa mtandao wa Vodacom wanaweza kushiriki katika promosheni hii.
“Tunasherehekea miaka kumi ya kutoa huduma zetu hapa nchini, kwa ubora na mafanikio, hivyo tunawiwa kurudisha fadhila kwa wale walioyawezesha mafanikio haya” alisema Mafuru.
Hyundai i10 ni gari mahususi kwa mijini, linatengenezwa na kampuni ya Hyundai Motor na kuzinduliwa tarehe 31, oktoba 2007.
Gari hili hukupa faraja zote za gari la kifahari, na wakati huohuo ni gari lenye gharama nafuu za utunzaji na pia matumizi madogo ya mafuta.
Namuona pale Mary natema akiuza sura, vipi baby wako hajambo.
ReplyDeleteMMh huyo mshindi bonge la kabati!
ReplyDeleteKAMA BAADHI YA MAONI KUHUSU SHINDANO HILI YANACHAKACHULIWA, BASI UKWELI WAKE WA USHINDI UNANITIA MASHAKA.
ReplyDelete