Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inakemea vikali mauaji ya mtoto Fotidatus Focus (7) aliyeuwawa kwa kukatwa kichwa na mtuhumiwa kutokomea nacho kusikojulikana tukio lililotokea maeneo ya Kyerere Wilayani Kyaka.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo baada ya kumlalamikia mtoto Fitidatus Focus kwamba aliwasha moto uliounguza maharage yake yaliyokuwa nje ya nyumba na pia kuteketeza fedha zilizokuwa ndani ya maharage hayo.

Wizara inasikitishwa na mauaji aliofanyiwa mtoto huyo maana suala linalolalamikiwa na hasara iliyoripotiwa haikuwa kubwa kiasi cha kukatisha uhai wa mtoto wa miaka saba.

Aidha, Wizara inalaani tukio la mauaji ya mtoto Diana Dionis (17) aliyekuwa mfanyakazi wa ndani aliyenyongwa na mwili wake kuning’inizwa kwa waya kwenye mpapai katika mtaa wa Kashabo Mjini Bukoba. Matukio haya yote yametokea hivi karibuni Mkoani Kagera.

Wizara imepokea taarifa ya mauji ya watoto hao kwa masikitiko makubwa maana matukio ya kikatili ya aina hii yanapotokea katika ngazi ya familia, yanarudisha nyuma kwa kiasi kikubwa juhudi za Serikali katika kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukiukwaji wa Haki za Msingi na Ustawi wa Mtoto ikiwemo haki ya kuishi ambayo ndio haki kuu kuliko zote.

Matukio ya mauaji kama haya yanawakosesha watoto haki yao ya msingi ya kuishi ambayo ni haki yao ya kikatiba na ni kitendo kinacho pingana na Mikataba ya Kimataifa ya Haki na Ustawi wa Mtoto ambayo imesainiwa, kuridhiwa na kutekelezwa na nchi yetu katika ngazi zote na kwa kila mtu mmoja mmoja.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto inahimiza jamii kubadilika na kuhakikisha kuwa familia na jamii kwa ujumla ambako kitovu cha makuzi na malezi ya watoto wa Kitanzania panakuwa ni mahala salama penye upendo amani na usalama kwa watoto wote; taasisi hizo kuihakikishia jamii ya watoto haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kutobaguliwa na kuendelezwa.

Wizara inatoa rambirambi kwa wazazi, walezi, ndugu, na jamaa wa watoto hao maana haki yao ya kuishi imekatishwa katika umri mdogo kwa kufanyiwa mauaji ya kinyama. Wizara inawaomba wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi mazito.

Mariam J. Mwaffisi
KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. nyie vijana wa michuzi. mi si niliuliza sasa huyo kijana mnatuambia aliitwa fotidatus ama fitidatus??mnagoma kutoa, mbona hata na kurekebisha hamrekebishi??mnajua skills na ethics za uandishi ninyi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...