Hivi karibuni kwenye blogu mbali mbali, kumekuwa na mwelekeo hasi wa kukatisha tamaa watanzania wanaoamua kukaa nje ya nchi. Tanzania ina kiwango kidogo sana cha ‘diapora’ kulinganisha na idadi yetu ya watu.

Wengi wetu ndio tumenza hivi karibuni ku ‘DARE’ kuweka makazi nje ya nchi, wengi wetu ni ‘FIRST GENERATION.’ Nchi nyingine kama majirani zetu na hasa ‘West Africa’, tayari wana ‘third au fourth generation diaspora.’ Diaspora wao wamejiimarisha nje ya nchi na wanasaidia nchi zao kwa njia moja au nyingine kwa mfano:

Moja, kutambulisha nchi zao huko waliko (Tanzania haijulikani sana, moja wa sababu ni kwamba watu wa nje hawajakutana na watanzania!), mbili, wanapeleka ndugu zao nje ya nchi, kwa masomo na kazi; tatu wanawekeza kwenye nchi zao; na nne kwa mafanikio yao, wanaletea sifa nchi zao za asili walikotokea, kupitia kushiriki kwenye michezo, mafanikio kitaaluma, kikazi, kibiashara, nk.

Kwa upande wa mahusiano ya kindoa, Barrack Obama ni uzao wa aina hii. Obama asingekuwepo kama si mjaluo kufanya mavituz huko Hawaii! Mfano mwingine ni kama Adebayo Ogunlesi, yule Mnigeria aliyenunua ‘London Gatwick Airport.’

Vile vile kuna wanamichezo, wanamuziki lukuki wa Ghana, Nigeria, etc ambao ni ‘third generation dispora.’ Vile vile kuna ‘ first generation diaspora’ wameingia kwenye jukwaa la siasa Ujerumani, Uingereza, nk.

Ghana ina idadi ndogo ya watu na haina vivutio vyovyote vya utalii kulinganisha na sisi, lakini inajulikana zaidi ya Tanzania sababu ya nguvu ya ‘diaspora.’ Mara nyingi nikisafiri watu wananiuliza kama nini ni Mghana. Sijawahi kuulizwa kama mimi ni Mtanzania!

HATA KAMA MTU LEO ANABEBA BOKSI NJE YA NCHI, BADO KUNA UWEZEKANO MTOTO WAKE, MJUKUU WAKE, AU MTUKUU WAKE AKAWA MTU WA MAANA HUKO NJE ALIKO.

Hao “third generation diaspora” wa nchi nyingine ambao wana mafanikio, SI KWAMBA BABU au BIBI ZAO WALIKWENDA NJE WAKIWA MATAJIRI.

Wengi wao wali ‘struggle,’ na hata kama hawakufika mbali, kizazi chao cha sasa wanaona faida. Mapambano ya kweli ya kimaisha, kimaendeleo na kidunia hayako Dar es salaam , Bukoba, Mbeya au Lindi, etc, yako New York, London, Los Angeles, Tokyo, Paris, etc.

Huko watu wanapambana na DUNIA. Mimi naona ATTITUDE YETU TULIYORITHI KWENYE UJAMAA BADO INATU “HAUNT” NDIO MAANA TUNARIDHIKA NA KIDOGO TUNACHOPATA TANZANIA, TUNAOGOPA USHINDANI NA KUKEJELI WANAOJARIBU MAISHA NJE.

MTANZANIA AKISHAKUWA NA NYUMBA NA GARI ANAONA AMEFIKA! lakini mtu wa “West Afrika” hata kama vitu hivyo anavyo, atafikiria njia nyingine za kuji ‘establish’ zaidi nje ya nchi.

Na ndio maana mipango ya ‘East African community’ inapoendelea watanzania wanaanza KUOGOPA na KUTETEMEKA! Ni kwa sababu hawajazoea ushindani wa kidunia, wanaridhika tu na wanachopata nchini.

‘Utajiri wa Watanzania haufikii viwango vyovyote vya kimataifa! Sasa hivi Tanzania kuna makampuni mengi ya Kenya, lakini hakuna makampuni ya Tanzania Kenya!.

Watanzania tusiwe na mtazamo wa karibu (MYOPIC), tuone mbali. Tusifikirie mafanikio yetu, bali ya vizazi vijavyo, wajukuu na watukuu wetu. KAMA MTU YUKO NJE ANABEBA BOKSI HATAKI KURUDI, MWACHE SABABU WATOTO, WAJUKUU AU WATUKUU ZAKE HUKO NJE WANAWEZA KUWA NA FAIDA KWA NCHI YETU.

‘Afterall,’ uzoefu unaonesha hao ‘first generation diaspora,’ mbao siku hizi tunaitwa wabeba boksi, umri ukiongezeka huwa tunarudi Tanzania! Wanaozeekea nje hadi mwisho wa maisha yao mara nyingi ni 'generation' zinazofuata. Nadhani ujumbe umefika!

tehe.. tehe… teh..!!!

By Mbeba box

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Nakuunga mkono. Kuna siku Lady J Dee alisema 'anawaza' kununua ndege mfano wa DASH 8 (aina ya ndege).. watu wakaanza kumponda.. wakati inawezekana kabisa kukiwa na nia.
    Umeongea ukweli.

    ReplyDelete
  2. Mbeba boksi hoyeee...Tanzania itajengwa na wenye moyo na wanaodiriki hata kubeba boksi...

    Japo nashauri tuangalie namna ya kutengeneza boksi pia...


    Mdau,
    Norway

    ReplyDelete
  3. Well said and wish you all the best

    you have said the truth,the whole truth. nothing but the truth.

    Mbeba Masanduku

    ReplyDelete
  4. Mwanangu, nondo umeshushaaaa! kongrachulesheen. Viziwi na waoneee, na vipweeff pia wasikie.

    Chiaaz Mchiiz

    ReplyDelete
  5. ni vizuri umejaribu kuwaambia watanzania,lakini walivyowabishi wataanza kukutukana,ulichoongea ni kweli kabisa,tubadilike jamani na tusaidiane si kupigana vijembe tu.

    ReplyDelete
  6. Napenda kumuunga mkono ndugu Mbeba Box katika maoni yake hapo juu.

    Ni kweli wabeba box tulioko huku tuna "option" ya kurudi nyumbani ili kupambana na maisha huko tukilijenga taifa letu. Lakini vile vile kwa sababu alizozieleza ndugu Mbeba boxi twaweza amua kubaki huku na kulitetea jina la Tanzania tokea nje. Na hata kama "magharibi" imeshatukumba na hivi kushindwa kung'ara, hiyo bado si hoja sana kwani bado tuna uwezo wa kuwasaidia watoto wetu wakafanikiwa na hivi kuchangia katika kulitetea taifa letu na kulipatia sifa katika nyanja mbali mbali.
    Jambo hili laweza fanikiwa kwa kukazania mambo makuu matatu: kwanza, elimu ya watoto wetu (kuwafundisha na kuhakikisha wanazingatia masomo); pili, kuwa na nidhamu katika uchumi binafsi (hasa hasa kukaa mbali na madeni) na tatu, ambayo ni muhimu sana kumuomba Mola abariki.

    Wengi tunashindwa maisha hapa ughaibuni kwa kupoteza malengo kwa kubweteka na starehe za muda mfupi ambazo hatimaye hutuweka matatizoni. Siri ya ushindi ughaibuni ni: Kwenda shule, Kukaa mbali na madeni na mwisho kutomsahau Mola wako. Asante

    ReplyDelete
  7. Good point,but "mbeba box" is just a term commonly used to generalize verieties of jobs done by Tanzanians living abroad no matter people are dump truk operators,lisenced lawyers,restaurant servers, or lisenced nurses.Despite the fact that we're all well known as "wabeba mabox"a significantly low profile term commonly despized by some people back home,but we all know how much we can flex our financial and intellectual muscle rather than it would have otherwise been had we chosen to remain back home sharing ignorance and poverty.

    ReplyDelete
  8. alichoongea mmbeba boxi ni cha ukweli madiaspro kotoka east africa tunapendana ,tunaumoja atubaguani kama ilivyo kwa wenzetu kutoka west afrika ukabila umewajaa tofauti na sisi ila kitu kimoja kinachoturudisha nyuma uswahili umetuzidi, ni kweli tunaishi kama familia moja lakini hatupo tayari kusaidia pale mmoja anapokuwa chini atafurahi udididmie ili uzidi kumuomba na akufanye mtumwa sio kama wenzetu wa west wanabebabna japo kwa ukabila.

    ReplyDelete
  9. EVERYTHING IS TEMPORARY IN THIS WORLD ACHA TURIDHIKE NA HICHO HICHO KIDOGO TUNACHOPATA MAMBO MAKUBWA YA NINI ??

    TUNATAKA AMANI TU SHWARIIIIIIII

    ReplyDelete
  10. Ndugu wabeba mabox au "diaspora" msisubiri umri uende. Tanzania bado ni nchi tajiri na inawahitaji wakati mkiwa na mawazo ya kuwezesha kubadilisha mambo. Mimi ninawaunga mkono wabeba maboxi kama vile akina dr Shayo ambaye aliwahi kuahidi ndani ya glob hii ya jamii na kwa kweli ametimiza ile ahadi yake ya kuja kujenga taifa kwa nafasi yake kama mtanzania. Mfano kama hii ni ya kuigwa. na kwa kweli ninawaomba akina John mashaka na wengineo ambao kwa kweli mmekuwa chachu ya kizazi kipya kutoa mchango wenu katika kuwasaidia wale tunaowachagua kuliongoza taifa hili.
    Hongera Dr Shayo kwa uamuzi wako wa kurudi bongo na kwa kweli mchango wako umeanza kuonekana kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia maendeleo yako tangu uliporudi Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Hullo there,
    Kitu cha ajabu ni hiki: Chini ya sheria ya uraia nchi za Afrika mashariki raia wa Kenya anaruhusiwa (to a limited extent) kuwa na haki sawa na mtanzania kama ataamua kuwekeza na kuishi Tanzania. Moja ya mabadiriko ya katiba ya Kenya ya hivi karibuni ni pamoja na raia wake kuamua kuwa na uraia zaidi ya moja (duo- au multi-citizenship). Ndiyo kusema, wakati mkenya huyo (ambaye pia ana haki ya kuwa raia wa nchi nyingine zaidi ya Kenya au Tanzania)anaweza kuja Tanzania chini ya sheria za EAC na kupata haki zote za kuishi na kuwekeza kama mtanaznia, lakini mzawa wa mtanzania ambaye tayari ni raia wa nchi nyingine hana haki hiyo, kwa sababu imetokea akawa na gamba (passport) ya nchi tofauti!! When other nations kama Kenya wamekwisha fahamu umuhimu huo, bado Watanzania na viongozi wake wanajishauri kwa visingizio vya national security na ujinga mwingine. In the end tuatanza kuwalaumu wakenya, while ukweli uko wazi. Hivi sisi ndani ya vichwa vyetu tumelogwa na mchawi gani?

    ReplyDelete
  12. Ujumbe umefika kabisa..wape vipande vyao wakiwa na kagari, nyumba na fridge basi maisha ni mazuri. Life is more than that. Wengine wazazi wetu walikuja kusoma huku walivyomaliza walirudi nyumbani wamestaafu pension kama utani vile. Kila siku namuuliza mzee kwanini hakuzamia? Maisha yangekkua malaini kidogo kwa sisi na tungekua mbali sana. Huku nabana kwa nguvu na mali kwa ajili ya watoto wangu nikizaa wakijitahidi watafika mbali sana. Mtoto akiwa na akili huku ni mteremko tu. My friend amepunguzwa kazi kesha kimbilia unemployment mke wake kajifungua wamepewa sijui nini hiyo maziwa, cheese, cereal, formula wamepewa...saangapi nikiwa TX+Z nitapata hayo

    ReplyDelete
  13. hongera mbeba box kwa ujumbe wako usio na chembechembe za siasa,siku hizi haka ka nchi kananuka siasa,watu wamesahau kufanya kazi,wanafikiria siasa tu.

    ReplyDelete
  14. EBANAEEE!!!!!!!! MIMI NINA GARI NA NIMEPANGA HAPA SINZA LION, HUWEZI AMINI NIMEOTA MPAKA NUNDU NIKIJUA NIMEYAPATIA MAISHA, NAOMBA NIKIRI KWAMBA UMENIAMSHA NA HUU WARAKA WAKO NITAUFANYIA KAZI IMMIDIATLI.

    AVGOTA NASING MACH TU ADI

    ReplyDelete
  15. Kwa sababu ya Upendeleo Michuzi anaoutoa kwa CCM niliamua kuikacha hii blog, leo nimejikuta nimekuja na nakutana na hii post ya mbeba box, sikuwahi kuwaza mbali namna hii, kweli UNASTAHILI PONGEZI, wewe ni kichwa kama SLAA. Umenigusa sana na nazidi kuipongeza blog ya Michuzi kwa machache inayotupa, nimejengeka sana leo. Muono wa juu mno!! Mwanangu atakwenda nje mapema iwezekanavyo akapate eksipodzha!!

    ReplyDelete
  16. Njoo nyumbani tuzindue vijiwe vya ccm uchaguzi unakaribia. Achana na hayo, unajua mzee wetu Makamba hajawahi kutumia king'amuzi lakini wanamjua mpaka Uganda! hata hivyo hatapenda kusikia unataka kuwajanjarusha Watanzania.

    ReplyDelete
  17. Safi sana. Mbeba box. Maoni yako hayana ubishi. Wakati umefika watanzania tunatakiwa kuthubutu. Ndiyo maana kwa kukosa hii akili ya kuthubutu kazi yetu kubwa ni kulaumu tu serikali. Serikali haiwezi kukufanyia kitu zaidi ya kukuwekea an enabling environment.

    ReplyDelete
  18. Sasa wewe nia yako ni ipi? Yaani umefungua darasa ili mimi niliko huku baada ya miaka ishirini ninunue airport ya Canada au? Sasa unataka kusisitiza kuwa Baba yake Baraka alifanya kitu cha kimaendeleo ili leo kuwa na raisi wa Marekani Mkenya? Maana ninavyojua mimi alimtupa na hata hakusaidia kumlea wala kumkuza..NI SAWA NA SPERM DONOR TU!, na sijui MJALUO Atajivunia nini huko alipo RIP , kwa mafanikio ya BARAKA...
    "MAPAMBANO YA KWELI YA KIMAISHA, KIMAENDELEO NA KIDUNIA HAYAPO DAR,BUKOBA, MBEYA...YAPO NEW YORK NA PARIS...WHAT??? Hivi unajaribu kuwaambia nini wakazi wa hiyo miji hasa vijana wetu wanao-struggle na maisha ? Wakulima wanaotulisha na waliovyuoni nk? waende L.A NA TOKYO ILI WAKAPAMBANE NA MAENDELEO YA KWELI YA KIMAISHA , ILI TANZANIA IZAE AKINA OBAMA NA KUNUNUA AIRPORT? UNAJUA DHULUMA NA UFISADI ULIOPITA KUFIKIA HAPO? TUFUNGE SOKO LA KARIAKOO NA MASOKO YOTE YA HIYO MIJI ULIYOITAJA, NA MGOMO WA WAKULIMA WANAO SUPPLY HAYO MAZAO KWA WIKI TU , UONE MAENDELEO YA KIMAISHA NI NINI?
    MSHKAJI NAONA KAMA ULIKUWA NA KA-POINT FULANI LAKINI MWISHO WA WITO, UMEBOLONGA TUUUU....
    NA WEWE ULICHANGIA WAPI, AU GLOBUNI TUU..?
    UBARIKIWE MICHUZI , WADAU WOTE NA HASA GLOBU YETU YA JAMII KWA KUTOA NAFASI ILI VIJIMAWAZO FINYU PIA VIPATE ....
    NAWAKILISHA
    MDAU NYUTRO
    KANADA

    ReplyDelete
  19. salaams,kama watanzania wote tungekuwa na mtazamo(upeo)wa kimawazo kama wewe tungekuwa mbali sana,

    ReplyDelete
  20. MIMI NAKUBALIANA NA WEWE KABISA ILA TU SHIDA YENU NINYI MLIO HUKO NJE MARA NYINGI MNAPOTOA COMENT ZENU KUHUSU TANZANIA MNAKUWA VERY NEGATIVE WAKATI HUKU NDIO NYUMBANI KWENU. JUST BE POSITIVE NYUMBANI NI NYUMBANI TU

    ReplyDelete
  21. Sidhani kama ujumbe utafika. Una-deal na watu wenye "backward mentality". Utaambiwa urudi utafikiri watakukaribisha ufikie kwao.

    ReplyDelete
  22. Asante Ndugu yangu kwa ujumbe wako,

    Swala la kurudi au kutorudi mimi naona lisiwe la msingi. Mtu anatakiwa kuishi na ku "settle" pale anapoona anatumika vizuri zaidi na kupata riziki yake vizuri, na kufurahia maisha!!

    Kama unafurahia ughaibuni ruksa, kama unaona utafurahia huku 3rd world sawa (wengine wanaitumia 3rd World kutukaniana - msome advisor wa Pope safarini UK).

    Ila cha kustaajabishwa ni hiki: mkulima mzuri upendelea kulima sehemu mpya ambayo haijalimwa, au imelimwa kidogo ili apate tija kubwa. Na alime pale ambapo wakulima wengi mahiri hawajapaona. Mkulima mwingine asiyependa usumbufu wa kufyeka mapori atakimbilia pale ambapo wameshalima sana, na hatapata hata sehemu kubwa atavumilia tu kulima kwa kuhamahama, na kupata mazao finyu huku akitumia nguvu kubwa tu kuliko hata ile ya kufyeka pori sehemu mpya.

    Sasa swali ni hili, kwa nini shamba la Afrika watu wanalikimbia?? wengine mpaka watawekewa watu wa kuhakikisha hawatoki huko shambani kama tunavyowafungia au kuwazuia Tembo wa mbugani, wakija mashambani tunalalama kwamba wamevamia makazi. Hivyo ndivyo Mheshimiwa Ghadafi alivyoomba pesa Ufaransa (kama euro 4.0 mln) ili atoe ulinzi Waafrika ("tembo") wasivuke mpaka na kuingia kwenye makazi ya watu (Ulaya).

    3rd world = mbugani
    Ughaibuni = Makazi ya watu

    Kazi ipo!!

    ReplyDelete
  23. wewe kweli mbeba boksi hata waraka wako umekaaa kiboksi boksi ( hayana maana )

    ReplyDelete
  24. Hi Mbeba Box,
    AISEE MKUU WEWE NI BALAA YAANI UMEGUSA MULE MULE MKUU. MIMI NAISHI TANZANIA NA NINAWEZASEMA NI MFANYABIASHARA TENA MKUBWA HASWA. KWAKUWA UKU TANZANIA NIKIWA NA MTAJI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 5 ZA KIBONGO SIO MCHEZO NI ZAIDI YA 5 MILLION USD, LKN HAUWEZI AMINI NINAISHI KAMA DIGIDIGI AU NGURUWE PORI, YAANI KILA MTU ANATAKA KUNIPOTEZA MIMI, YAANI SISI WASWAHILI TUMEKUWA OVYO SANA MTU ETI ANATAKA APATE PESA BILA HATA YA KUFANYA KAZI, MTU ANATAKA KUIBA AU KUPOKEA RUSHWA NA KAMA UKIMNYIMA UTAMKOMA,WATAKUJA TRA (TANZANIA REVENEW AUTHOLITY), WATAKUJA POLICE WA KAWAIDA WATAKUSUMBUA WANAOJIITA WANAPAMBANA NA RUSHWA, WATAKUSUMBUA WAFANYAKAZI WAKO WEWE MWENYEWE WANAOKATAA KUFANYA KAZI. YAANI INAKUWA NI BALAA MTINDO MMOJA, NA MBAYA ZAIDI IMEJENGEKA MENTALITY MBAYA KWA WASWAHILI ETI MFANYABIASHARA NI MTU MMOJA MBAYA SANA KWASABABU ANAWADHURUMU WATU NA ANAJINUFAISHA YEYE PEKE YAKE.TUKIENDE KUNUNUA KOROSHO ILI MKULIMA AISHI TUNAAMBIWA TUNAWADHURUMU WAKULIMA, TUKINUNUA PAMBA VILEVILE TUKINUNUA KAHAWA VILE VILE, ILA AKIJA MZUNGU HATA KAMA FEKI ATAPEWA PAMBA ATAPEWA KOROSHO NA KILA ATAPEWA TENA KWA BEI RAHISI MNO NA HATA AKITAKA IKULU ATAPELEKWA, SASA JARIBU WEWE MZAWA KUFANYA HIVYO UONE HIYO PURUKUSHANI YAKE. YAANI RAIS YUKO HAPA HAPA BASI KUMUONA NI AFADHARI UWENDE MWEZINI ITAKUWA RAHISI KULIKO KUMUONA YEYE.
    MKUU WEWE BEBA BOX UKO UKO NJE WALA USIRUDI UKU UTAKUWA NA AKILI MBAYA KAMA SISI. MIMI MWENYEWE NIMESOMA NJE YA NCHI NA NILIFAURU VYEMA NIKAKATAA KUFUNDISHA CHUO KIKUU NILICHOMALIZIA NA KUAMUA KUGEUZA HOME, LKN HAUWEZI AMINI HAPA NILIPO LICHA YA KUONEKANA NAFANYA BIASHARA KUBWA MNO LKN SILALI KAKA, KILA KUKICHA NI MATATIZO TU, MALA CHAMA FURANI KINATAKA MICHANGO, MALA TRA WANATAKA KUKUKAGUA, YAANI WASWAHUILI TUMEKAA OVYO SANA, MALI WAKIWA NAZO WAZUNGU AU WAHINDI NI HALALI YAO ILA ZIKIWA KWA WAZAWA INAKUWA NONGWA, POMBE KWELI WATU HAWA. MKUU KAA UKO UKO ILI WATOTO WAKO WAWE NA AKILI NA USIJE ZAA KITUKO KIKASUMBU, UKU TUWACHIE SISI TULIOZOEA MAJUNGU NA WIZI. WATU WANAFANYA BIASHARA FEKI, WANAIBA PESA BOT, WANAIBA KOKOTE PALE, TENE MBAYA ZAIDI PESA ZILIZOKUWA TAYARI ZIMESHATAFUTWA, YAANI HAWA WATU HATARI SANA. UNAJUA NI BORA MTU AIBE HUDUMA LKN ASIIBE PESA AMBAZO TAYARI ZIMESHATAFUTWA. WEWE UTASHANGAA WATU WANAJENGA MAJUMBA YA AJABU AJABU LKN WALA BIASHARA WANAZOFANYA HAZIJULIKANI, KILA KWENYE MABENDI WANAIMBWA TU. YAANI FULL USANII.

    MKUU KAA UKO UKO.

    MUDDY NICE

    ReplyDelete
  25. Honest work is honest living, mbeba maboksi, toilet cleaner, or bank manager may earn different salaries,but they have the guts to make honest living.
    I think we Tz are happier to see a person seat behind a desk and ask for bribe to compesate for his salary as a success story. We are so used to looking for seating allowances, travel allowances etc,we all do cause we are still scared to venture out and do things different. Yes we can agree there are viable support from financial institutions for startups. But how many people you know won't be able to give you a loan for business if you present it right and they can see the possibility of earning something too.
    Work is work! Better then begging!

    ReplyDelete
  26. ....you guy.. you must be mad!!! km kufua kupiga deki na kuwasafisha wazee wa kizungu ni kustruggle.. basi elimu uliyonayo (kama unayo) basi haikufai, unamtizamo hasi kwa kiwango cha juu sana!! ndugu, tunamapori ya kutosha sn tu afrika njoo ulime kaka, watoto na wajukuu na watukuu wako watatoka tu hata km ww utaishia njiani! pole sana.

    ReplyDelete
  27. kama wewe ulikua unaishi kimaskini bongo ndio ukakimbilia nje usidhani wote, wengine tuna maisha mazuri na kazi nzuri bongo, kisa cha kuzugaragaza digree zangu kubeba mabox? wakati hapa nna kazi na cheo kizuri kulingana na elimu yangu?
    mdahalo wako hapa hauna mpango wala nini, Ghana haijulikani kwa ajili ya kuwa na watu wengi nje, ila kwa michezo, hasa mpira...
    hayo maisha ya ki-hindi hindi ya kutangatanga kila nchi hatuna mpango nayo, washamba mnaodhani kukaa ulaya ndio maana yake maisha mazuri, ili mradi unakaa ulaya ndio mnaokupapatikia, sisi tunakuja huko, tunasoma tunarudi zetu bongo kula maisha!

    ReplyDelete
  28. anony wa 12.25 unayesema watu wanapapatikia ulaya mbona wewe unaenda? kama bongo unakula raha basi baki huko all your life! na hapo bongo unakula raha gani wakati maji ya tabu na sio salama kunywa hadi uchemshe, umeme wa mgao, hospitali za kuunga unga.barabara ndo usiseme,foleni hadi zinakera! oh nilisahau, majambazi nayo je? au wewe una agreement nao kwahiyo huogopi kuvamiwa or else you are one of them!! hakuna anayelazimisha mtu/watu kwenda ulaya, ni opinion yake tu. either u take it or leave it..neeextttttt

    ReplyDelete
  29. mmbeba boksi mwenza, acha tuuu umelengesha kabsaaa, yaani mmh sina la kusema uku boksi ni tamu bwana manake hela yake ndefu, ila nachukia winter jamani acheni tu, anyway tumeamua kuwa wagumu hadi kieleweke!!
    maboksini
    canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...