Mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyerere wilayani Iringa aliyefahamika kwa jina na Baraka akiwa hoi huku akisaidiwa na wauguzi pamoja na wanausalama baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wamnanchi wenye jazba kali wakimtuhumu kuwa ni kibaka wakati mwanafunzi huyo Chapombe aliporuka ukuta na kuingia katika nyumba moja eneo la Kijiweni mtaa wa Paris Manispaa ya Iringa usiku wa leo akimfuata mke wa mtu.

Hata hivyo wananchi hao hata bila kujua sababu iliyompeleka kijana huyo ndani ya nyumba hiyo walianza kumpa kichapo huku mwenyewe akiwa hajitambui kutokana na kuzidiwa na pombe.

Kwa maelezo ya mashuhuda Baraka alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja katika nyumba hiyo ambaye kwa siku ya jana aliweza kumkana baada ya kuwa na mpenzi wake wa zamani hivyo kulazimika kupewa kichapo akituhumiwa kuwa ni kibaka kijana Baraka ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sokondari ya Nyerere.katika tukio lingine lililotokea usiku wa kuamkia asubuhi hii,

linaripoti kwamba mwanafunzi mwingine wa kidato cha tano shule ya sekondari Mwembetogwa pia ameponea katika tundu la Sindano kuuwawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.picha na Francis Godwin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. HIVI MTU USIYEMFAHAMU AKIRUKA UKUTA WAKATI WA USIKU NA KUINGIA NDANI YA NYUMBA YAKO, KUTAKUWA NA MUDA WA MAHOJIANO? AU ZAKO AU ZAKE, HIYO NDIYO HALI HALISI.

    ReplyDelete
  2. Ahahahhah safi sana hii , hatarudia tena nazani na pombe sasa hatapunguza !ahhaha

    ReplyDelete
  3. du huyo mshikaji ninoma! waenga walisema mke wammtu ni sumu! naona kijana somo kalipata.

    ReplyDelete
  4. Hoa wanafunzi wa huko watakuwa na mapepo sasa,au ni mambo ya bariidi!

    ReplyDelete
  5. na nyie wanafunzi mbona mnashangaza wanawake za watu ni sumu mtapoteza maisha bure,baada ya kukazana na masomo mnaebdekeza mambo ya kijinga..

    ReplyDelete
  6. Wanafunzi wa siku hizi wanasoma kwelikweli,wanajifunza na kuchakachua mapenzi

    ReplyDelete
  7. Jamani hawa wanafunzi vp???? Khaaaa!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi sishangai sana,watu wa Iringa wanapenda sana ngono.

    Tete he he "We niangushage tu"

    ReplyDelete
  9. Jamani mbona dunia imekwisha. Kidato cha sita na mke wa mtu. Hiyo haitoshi na pombe juu! Kwa nini wanafunzi wanakimbilia maisha namna hii. hii ni hatari.

    ReplyDelete
  10. Daaah vijana tuache hii tabia... Mbona wanawake ni wengi? Kumbuka unayoyafanya kwa mke wa mwenzako na ww utafanyiwa vivyo hivyo kwa mkeo..!

    ReplyDelete
  11. keh! hawa wanafunzi wa Iringa vipi jamani? naona wana-specialize kwenye wake za watu tu!

    Ila nahisi wanachezea kifo sasa!

    ReplyDelete
  12. "Penzi ni kikohozi, ukishika huliweziiii"
    "Mapenzi yangu kwa yule kijanaaa, nikaamua kumfanyia mambo yoteee...ili anieleweee, na ajue nampendaaa"

    ReplyDelete
  13. Jamani dunia inaisha, nyie waume pendeni na muwajali wake zenu, ona sasa watoto wadogo wanaenda kuwavunjia heshima. na nyie wazazi leeni vijana wenu kwa maadili wasiende kutafuta wake za watu na kuletea ukimwi wanafunzi wenzao, na ENYI vijana wahusika embu kuweni na haya na kujua mipaka yenu pombe na ngono na shule havipatani hata siku moja hamtoweza ona ufalme wa maendeleo na wa mungu. Mshindwe!

    ReplyDelete
  14. ilitakiwa hao watu wakamatwe na wafunguliwe mashitka ya kumwitia mtu mwizi,mi sielewi viongozi wanafanya nn?mnasema nchi ina Amani,amani gani watu wana uawa kila kukicha,nchi zilizoendelea wana akili moja inabidi tuige,mlinde mwenzio ili na wewe uje ulindwe,weka sheria kali ili na wewe siku ije ikusaidie maana na wewe ni binadamu inaweza ikutokee,upuuzi mtupu,kama kafumaniwa na mke wa mtu watu wengine yanawahusu nini?ni mke wenu wote,Tanzania ni Nchi yetu ina ndugu, mama zetu, baba zetu,kesho na kesho kutwa hakuna mtu wa kutusimamia kama hatutaweza kusimama wenyewe na miguu yetu tukathamini ubinahadamu..sky

    ReplyDelete
  15. They should listen what their mothers told them...Never go out with a married woman/Man...They will never leave their husband or wives for you ...They'll use you just for your for money, just for show off, or something else...you know what I am talking...

    ReplyDelete
  16. Huruma nilimuone stori ilipoanza ilipofikia kua alikua kalewa mbavu zangu zina uma kwa kicheko.

    ReplyDelete
  17. madenti wa bongo wanaendekeza ngono ile mbaya!! yani kutoka na wake za watu wanaona fashion..ila hivyo vichapo sio vya kitoto. next time tafuteni wapenzi wa rika lenu.hayo majimama yatawaua..

    ReplyDelete
  18. jamani watanzania tusione sawa watu kuchukua sheria mikononi mwao na kuwashambulia watu wengine. hii inauzunisha sana. ukatili wa namna hii tunautoa wapi watanzania wakati watu wanasema tunapenda amani. polisi hufanya nini wakati mambo kama haya yanatokea au wao ucheka na kuona ili jambo ni sawa. serikali ni lazima washughulikie hili jambo na kufanya kila watu wanaoshambulia watu wengine wanapelekwa kotini na kupewa adhabu kali. mimi kwakweli sielewi sheria za tanzania ziko aje.

    ReplyDelete
  19. mbona unatuchanganya hapa? unasema alituhumiwa kuwa ni kibaka, ilhali unasema aliruka ukuta kumfuata mke wa mtu. Sasa hapo inakuwaje? ni kibaka, alichofata kuiba ni nanhii ya mtu, amekwenda na lengo la kuiba huyo, ingawa sio kuiba mali!!!!!!

    ReplyDelete
  20. huu ni umbumbumbu wa sheria. wengi wetu watz hatjui sheria, tunawaachia manjagu na mahakimu kila kitu. ndiyo maana dhuluma na uvunjaji wa sheria vimekithiri. na hili ndio chimbuko la rushwa. katu mambo hayatakuwa sawa il hali suala la uraia na sheria haziko richabo kwa wengi.

    ReplyDelete
  21. Watu wa huduma ya kwanza wamevaa Boti za matope..#@! Hii kali

    ReplyDelete
  22. Ina maana watu hawajui kwamba hakuna familia zilizo sawa. Kama familia haijasimama haya ndiyo matokeo yake. Kwanza kabisa napenda kusema kwamba nusu ya wanume haswa mjini Dar wantembea na wanfunzi haswa wa kike, sasa ni ajabu gani huyu kijan kwenda kutembea na wake zao. Tangu enzi hizo za shida za usafiri wakina baba wengi wamekuwa wakiwadanganya mabint za watu kuwapa lift na simu na kila kitu, wewe baba au mama unasoma huu ujumbe hakikisha unajuwa kinaja wako kapita wapi. Hili ni tatizo sugu tanzania kwa sasa. Lakini Karibuni kuna kampuni yataanza kupiga picha za akina baba ambao wantembea na wanfunzi. Hili ni tatizo kubwa sana haswa Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...