Mkuu wa kanisa la Anglicana la Tanzania, Askofu Dr. Valentino Mokiwa

Na Ripota Wetu

Zikiwa zimebakia siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu, Mkuu wa kanisa la Anglicana la Tanzania, Askofu Dr. Valentino Mokiwa, ameonya dhidi ya uchakachaji matokeo ya uchaguzi kwa aina yoyote, huko ni kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

Askofu Dr. Mokiwa, ametoa onyo hilo leo, katika mahojiano maalum na Ripota wetu, yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Dayosisi ya Kanisa la Anglicana Tanzania, yaliyopo eneo la Ilala hapa jijini Dar es Salaam.

Askofu Mokiwa amesema uchaguzi huru na wa haki ndicho kipimo cha demokrasia iliyopevuka ambapo mshindi katika uchaguzi ndio chaguo la wengi, hivyo vitendo vyovyote vya kuchakachua matokeo halali ya uchaguza, ni kitu cha hatari kinachoweza kutishia amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

Pia askofu Dr. Valentino Mokiwa, ametoa angalizo muhimu kwa vyama vya siasa nchini, wagombea wao na Watanzania kwa ujumla, kuwa tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo yoyote ya uchaguzi huu, hata kama atakayeshinda sio mgombea uliyemtegemea.

Askofu Mokiwa, ametoa angalizo hilo kufuatia kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, kugubikwa na hamasa ya hali ya juu Ambato ameielezea haijapata kutokea tangu harakati za kupigania uhuru, hivyo kufuatia hamasa hii, inaweza kupelekea vyama na washabiki wake kuhamanikia ushindi, hivyo matokea yakiwa kinyume cha matarajio yao, wanaweza kufanya chochote.

Askofu Mokiwa amekiri uchaguzi wa mwaka huu, hautabiriki kirahisi kama chaguzi nyingi zilizo tangulia, hivyo ni muhimu kwa wadau wote wanaoshiriki kwenye uchaguzi huu, pamoja na kuwashabikia wagombea wanaowataka, lazima wawe tayari kupokea na kuyakubali kwa moyo, matokeo yoyote ambayo ndio chaguo la wengi.

Amesema, baada ya kutangazwa kwa matokeo, huo ndio mwisho wa ushindani, hivyo amewaomba wagombea walioshinda na walioshindwa, kushikana mikono, kupongezana na hata kukumbatiana kama ishara ya upendo, kudumisha amani utulivu na mshikamano baina ya Watanzania, na kuwasihi walioshinda, wasiwabeze walioshindwa.

Askofu Dr. Mokiwa, naye amejiunga na viongozi wengine wa dini nchini kwa kutangaza kuwa Kanisa la Anglican, halina mgombea linalomuunga mkono, na kuwahimiza wafuasi wake, wajitokeze kwa wingi situ ya kupiga kura, na wawapigie wagombea wowote wanaowataka bila kujali dini zao.

Wakati huo huo, Askofu Mokiwa ametangaza kufanyika kwa misa maalum ya kuombea uchaguzi wa amani nchini Tanzania, itakayofanyika kesho saa 4:00 asubuhi katika kanisa la St. Albano, lililope eneo la Posta Mpya, watu wote wamekaribishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Asante sana baba askofu tumekusikia na tunamumba mungu uchaguzi upite salama kabisa.

    ReplyDelete
  2. Unaposema uchaguzi hautabiriki kwani hii ni mechi ya Simba na Yanga? CCM itashinda Bara bila wasiwasi suala ni percentage ngapi. Mpambano uko Zanzibar na Dk. Shein atamshinda Maalim Seif kwa kura kiasi zitakazopelekea kukamilisha azma ya kuunda Serikali ya Mseto.

    ReplyDelete
  3. Unaposema uchaguzi hautabiriki kwani hii ni mechi ya Simba na Yanga? CCM itashinda Bara bila wasiwasi suala ni percentage ngapi. Mpambano uko Zanzibar na Dk. Shein atamshinda Maalim Seif kwa kura kiasi zitakazopelekea kukamilisha azma ya kuunda Serikali ya Mseto.

    ReplyDelete
  4. Big Up Askofu Dr. Valentino Mokiwa

    Naunga mkono kwa asilimia mia

    ----mdau----

    ReplyDelete
  5. Sawa lakini ya Kaisari apewe Kaisari na ya Mungu apewe Mungu. Tumesikia na tutampa JK. Bwana ahimidiwe sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...