JK akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
JK akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
JK akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...