Marehemu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe

Familia ya Marehemu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe iishio Uingereza na Tanzania, kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Jumuiya ya watanzania Reading na Slough ,Kanisa La wasabato (Angaza SDA Church -Reading), Madhehebu yote ya kidini hapa UK ,vyama vyote vya kisiasa,Waganga wote kutoka Mkoa wa Mara ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na pia bila kusahau blog zote zilizo shiriki kutoa taarifa(Hakingowi,Issa Michuzi,Majid Mjengwa ,TZUK,Watanzaniaoslo,Musoma -tanzania ,wavuti n.k) , kwa kufanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu baba yetu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe ambaye alifariki Kutokana na ajali ya gari tarehe 3/October /2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 9 /October/2010 kijijini kwake Kirongwe Tarime MkoaniMara.

Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali ambayo imewezesha familia ya marehemu walioko Uingereza kuweza kuwahi mazishi.

Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunasema tu kwamba Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili wa Marehemu hadi kuzika.

Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mibaraka katika shughuli zenu za kila siku.Tumeambatanisha picha za ajali .

Sisi tulimpenda sana Marehemu Nyitambe lakini

Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,

Jina la Bwana lihimidiwe.

Asanteni sana

Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Poleni sana familia ya Mchumgaji Nyitambe. Mungu ampumzishe mahali pema pepono.

    Eng. J. Msonge

    ReplyDelete
  2. Nilimjua sana Mzee Nyitambe....kila wakati tulipokutana tulikuwa tunacheka na kutaniana ukizingatia alikuwa mtani wangu. Nilifanya kazi zake vizuri na yeye aliniamini. Mara ya mwisho nimeongea nae katika simu alikuwa Musoma mie niko Dar....He was such a great person....Nawapeni pole wafiwa...hasa mama Nyitambe, NETO( wa Kinondoni Manispaa) na watoto wake.

    ReplyDelete
  3. May his gentle soul rest in Peace AMEN.. Poleni sana Beatrice and siblings.. Hope MUNGU ataendelea kumponya mama na kuwatia nyote nguvu!! Chichi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...