JK akiwa na Mzee Constantine Millinga, mmoja wa waasisi wanne wa TANU walio hai leo mjini Mbinga, mkoa wa Ruvuma ambao pamoja na Mwalimu Nyerere ndio walioanzisha chama hicho. Mzee Millinga, mwenye unri wa miaka 89 sasa, amefurahi kukutana na JK ambaye pamoja na matunzo mengine stahiki amemnunulia gari la kumwezesha kufanya shughuli zake za kila siku bila bughudha ya usafiri. Leo JK amehitimisha mkoa wa 23 kuutembelea katika kampeni zake za uchaguzi ambapo sasa anaelekea Lindi na Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Msaada tutani....
    -Hivi mbinga iko ktk mkoa wa Iringa au Ruvuma?

    -Tunaposema JK amehitimisha mkoa wa 23 kuutembelea katika kampeni za uchaguzi tunajumlisha pamoja naile ambayo imetembelewa na member wengine wa familia yake? au hii ni ile aliyotembelea yeye tu kama JK?

    samahani kwa usumbufu kaka.
    its i, the die hard ccm fun!

    ReplyDelete
  2. Picha nzuri na historia nzuri ya Mzee Millinga kukutana na JK, lakini Mbinga kuwa mkoa wa Iringa badala ya Ruvuma? Imenistua na bado najilaumu kwani nimeshindwa kufuatili mabadiliko mengi ya wilaya zinazozuka kama uyoga Tanzania bara. Mbinga imekwenda Iringa?

    ReplyDelete
  3. kuwaenzi waasisi ni jambop zuri jk keep it up.
    boaz ntukula
    mwanza

    ReplyDelete
  4. babu wa watu kajipatia kijigari kake angalau akifa wajukuu wapate urithi ...... ccm oye

    ReplyDelete
  5. Q. Of all the places you’ve been, what’s the best?

    A. Tanzania. It’s raw and beautiful, and made me feel so alive.

    http://www.nytimes.com/2010/10/12/business/12flier.html?src=busln

    ReplyDelete
  6. Swali???

    Numshabiki mkuu wa JK kwani sera zake na CCM hazina ukabila wala udini ukilinganisha na vyama vingine ambavyo washabki wake wako kwa ajili kiongozi ni mdini wa dini fulani au kabila flan.

    Labda Historia yangu ni ndogo na kitabu nilichosoma cha Mwalimu Nyerere inaonesha kua Mwalimu alipotoka Musoma kuja Dar Tanu ilikua ishaanzishwa. Sasa Mwalimu nyerere atakuaje muasisi???

    Alipewa uongozi wa TANU pale wakoloni walipoweka vikwazo vya elimu kwa mgombea yeyeto wa Udiwani na kazalika.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...