Mdau Fred Alfred akiwa na mai waifu wake
Mdau Fred Alfred siku alipochukua jumla.

Habari Kaka Michuzi,

Nategemea umzima wa afya. Mie ni blogger mwenzio kutoka chuo kikuu Mzumbe, Morogoro, nafikiri utakuwa unanikumbuka.

Napenda unarushie habari hii ya kumbukumbu ya ndoa yangu kutimiza miaka kumi. Ndoa yetu ilifungwa pale katika kanisa la mtakatifu peter (St.Peter) jijini DSM, hiyo ilikuwa ni th. 30.09.2000.

Hivyo tarehe kama hiyo na mwezi kama huo mwaka huu mimi na mwenzangu tulitimiza miaka 10 ya ndoa yetu. Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha na kutufikisha hapa tulipo sasa.

Pia tunawashukuru ndugu, jamaa na marafiki kwa kutuombea kwa dua na maombi yao.

Mungu wetu awabariki sana. Kwa habari zaidi kuhusiana na tukio hili tembelea

www.fredalfred.blogspot.com.

Naambatanisha picha mbili. Ya kwanza ni siku ya harusi pale st.peter (th. 30.09.2000) na ya pili ni ya siku ya kumbukumbu ya ndoa yenyewe majuzi (th.30.09.2010)

Natanguliza shukrani kaka!

Fred

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera, Alfred, Mungu kawajalia Watoto wangapi? Mungu azidi kuwapa uzima ili mje kufikie Jubileeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Mr A na dada yangu mpendwa Fellie. Baraka tele na salaams nyingi toka kwetu,
    Dr Imani & Family.

    ReplyDelete
  3. Hongereni kwa miaka kumi ya ndoa. Mungu awape neema zote. Ushauri wa bure. Msisahau kusali rozari kila siku. Ina nguvu ya pekee. Mkeo anaonekana mama kweli wa sala.

    ReplyDelete
  4. wadau wa ashira girls jamani nimefurahi kumuona mwana ashira mwenzetu kaolewa na sasa ana miaka 10 kwenye ndoa yake. ni furaha iliyoje, hongereni sana kwa kuleana kwa jinsi hii....kisungura

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana Fred na Felista. Mungu awape miaka mingi zaidi ya kudumu katika ndoa yenu.

    ReplyDelete
  6. How nice! I was at this wedding 10 years ago. Hongera sana Felista.

    ReplyDelete
  7. Hongereni sana mzidi kupendana na ndoa yenu idumu milele, kaka wewe ndio utakayeifanya ndoa yako iwe imara na idumu, hapa namaanisha yale mambo yenu yaleeeee ya small house kama huna hayo mambo mtakuwa na amani daima na ndoa yenu itakuwa na afya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...