Aslaam aleikhum Mjomba,
Tukuyu joto mwezi huu na vumbi, sijui ndio
mambo ya Global warming? ama Mabadiliko ya tabia nchi!?

Jumamosi kulikuwa na patashika na nguo chanika wakati timu ya darts toka kituo cha kati Mbeya mjini ilipofanya ziara ya mchezo wa kirafiki wa darts hapa Tukuyu na kukutana na wana Laximi Darts Club.
Mwisho wa Mchezo Maafande wa Central Police Mbeya walijikuta wakitiwa korokoroni kwa mabao 8 kwa tatu kwa singles na 3-3 kwa doubles. Nyota wa mchezo alikuwa Ankal Juma Liganja wa Laximi Darts Club ambaye alipewa zawadi maalum.

Hii ni katika matayarisho ya mashindano ya darts kitaifa yatakayofanyika Mkoani Mbeya kuanzia 19/11/2010 na kufuatia na yale ya Afrika Mashariki baadaye mwaka huu na kuzikutanisha timu toka Tanzania bara na Visiwani, Uganda, Kenya na kwa mara ya kwanza Rwanda na Burudi zitashiriki.

Ndaga fijo mjomba.
Pata mapicha ya siku hiyo
Na Juma Liganja wa Globu ya Jamii, Tukuyu

Mshambuliaji wa Laximi Darts club ya Tukuyu akiondoa ngoma kimiani

Straika wa Central Police Mbeya akikosa penati...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh...jamani mbona kila kona na kila kitu kimechakaaa ovyo!!!yaani kweli kwa wanyakyusa tambarare!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...