Mgombea wa Urais kupitia chana cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwenye mkutano wake wa kampeni za lala salama mchana wa leo kabla ya kurejea Dar es Saalam kufanya mkutano wa mwisho wa kufunga kampeni za chama hicho.
Mmoja wa shabiki wa Chama cha Wananchi CUF akiingia uwanjani kwa ajili ya kumpokea Mgombea wa Urais wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ( hayupo pichani) leo siku ya mwisho wa kampeni za uchaguzi mjini Morogoro kama alivyokutwa.
Baadhi ya waangaalizi wa uchaguzi mkuu wa hapa nchini kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walifuatilia mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ( hayupo pichani) leo mjini Morogoro ambao ulikuwa ni kati ya mikutano yake ya mwisho kabla ya uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...