Tanga ya Mjerumani, nimji wakizamani
kavutiwa mkoloni ,kukaa hapa nchini
wambali wamikoani,walikuja mashambani
sikwambii viwandani,napirika bandarini
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Umaarufu mwambao,kwenye bahari yahindi
umeandikwa ubao,kuwa siku hazigandi
elimu ndio funguo,idai japo hupendi
jamani muhimu ngao,ndio siri yaushindi
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Inakuponza imani ,nahiyo yako subira
umeanikwa juani ,kwakuipenda hadhara
Tanga umaskini,nahali wewe nibora
amka upo vitani,kabla hujawa ngawira
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Umekuwa Tanga bora,kwakutaka yakokura
nawe sifanye papara, ukaipata hasara
bali uwape harara,natumbo lenye kuhara
silaha yako nikura,mpe kiongozi bora
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Kashindwa kulinda maji,chura nachake kijicho
amkeni wana mji,fungueni yenu macho
sasa niwenu mtaji,mtapata mtakacho
danganya kuitwa jiji, wacheza mwan jificho
unani tanga kunani,akuonae ni nani?


Watizame mikoani, watu naheshima zao
wapewa kitu makini,kuridhi matakwa yao
ajira za viwanadani,afya navingi vyuo
wewe upo makwapani,wafanya lako hashuo
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Naongea kiswahili,nasio kiingereza
fungua zako akili,wito kuutekeleza
usijekuwa dhalili, wenzio watakubeza
Kura yako ya awali,mazuri kutengeneza.
unani tanga kunani,akuonae ni nani?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...