Marehemu Omary Msoke wakati wa uhai wake.

Familia ya Bw. Ibrahim Msoke, wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Bi. Faith wa AAR Health Services, wanatoa shukrani kwa wote walioshiriki katika kipindi cha msiba wa mtoto wao mpendwa OMARY MSOKE, aliyefariki kwa ajali ya gari eneo la magomeni tarehe 9 Septemba, 2010 na kuzikwa huko Lusanga Muheza, Tanga tarehe 11/09/2010.

Shukrani za pekee ziwaendee wafanyakazi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, wafanyakazi wote AAR Health Services pamoja na ndugu, majirani na marafiki wote.

Arobaini itafanyika Tanga tarehe 16 na 17 Oktoba, 2010.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI

- AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. RIP mkaka mzuri jamani duh! kazi ya mola haina makosa. poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...