Align CenterWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia katika sherehe za siku ya wazee duniani zilizofanyika kitaifa Mjini Morogoro, Oktoba 1, 2010. Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Luteni Kanali Mstaafu Issa Mchibya.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea maanadamo ya wazee ( hawapo pichani) siku ya Wazee Duniani, ambayo hufanyika kila mwaka, Oktoba Mosi , ambapo kitaifa ilifayika Mkoani Morogoro.Bibi Mary Enock , mkazi wa Manispaa ya Morogoro, akichugunzwa macho na mmoja wa wataalamu wa magonjwa ya macho wakati wa siku ya Wazee Duniani , ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba Mosi, ambapo kitaifa ilifanyika Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wachezaji wa timu mbili za soka la wazee wakitoana jasho katika mchezo wao wa siku ya wazee duniani ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba Mosi, ambapo kitaifa ilifanyika Mkoani Morogoro, Mchezo huo ulihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda , katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa
Mshindi wa kufukuza kuku katika mashindano ya wazee wakike pamoja na wakiume wakati wa siku ya wazee duniani inaayofanyika kila mwaka Oktoba Mosi, ambapo kitaifa iliyanyika Mkoani Morogoro.
Maandamano yakiingia katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nonesense kwa Tanzania kusherekea siku hii kwani wazee kama akina matonya wateseka kwa sababu ya watu wachache kama akina Rostam!

    ReplyDelete
  2. mahmoud al-jabri wa tennis bakery, email yangu ni samateryussuf@ymail.com, tuwasiliane imekuwa muda mrefu toka 2000,keep in touch bro!!

    ReplyDelete
  3. Hivi ni kiswahili chetu kibaya au hii ni siku y a old people kweli? Hii siku ni siku ya babu na bibi. Sio ya wazee. Mimi nina rafiki yangu ana miaka 32 na ana mjukuuu. Yeah ...inrun kwenye family ...sasa sijui yeye naye mtamuita muzee...Hii ni siku ya grand parents bwana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...