Mkurugenzi wa USAID/COMPETE, East and Central Africa Trade Hub Bw. Holm Olsen amefafanua kuwa Siku ya mwisho ya Swahili Fashion week USAID/COMPETE itaandaa workshop itakayotoa taaluma kwa wabunifu katika suala la muonekano bora katika fashion show kwa vitu vitakavyotengeneza na wabunifu pia mafunzo yatakayosaidia katika kutoa miongozo ya kuelekeza katika mauzo, na kuangalia suala zima la masoko kwa ujumla. Workshop hiyo pia itaangalia kwa jinsi gani wabunifu wanaweza kupata nafasi katika masomo nchini Marekani na ya kimataifa kwa ujumla, sambamba na kukuza ubunifu hapa nchini na hata kuvuka mipaka hadi nje ya nchi. " Kama wabunifu wengi wataonyesha mavazi, kitaifa na kimataifa, waliyoyabuni kwa kutumia malighafi zinazizalishwa na viwanda vya nguo vulivyopo katika hali itakayoleta faida kwa viwanda vya nguo vilivyopo Afrika Mashariki. Na huu utakuwa mwanzo mzuri na endelevu katika sekta hii," amesema Barry Fisher kutoka USAID/COMPETE.
Mwandaaji wa onyesho la mavazi la Swahili Fashion Week ambaye pia ni mbunifu mahiri wa mavazi Mustafa Hassanal akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya hotel ya Southern Sun,jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa onyesho la Swahili fashion week,ambalo linatarajia kufanyika katika bustani ya Karimjee mnamo novemba 5 mwaka huu.

"Tunatengeneza kwamba siku moja sekta hii ya Fashion kwa Afrika Mashariki itakuwa zaidi na kutambulika kuwa kiungo bora kwa Sekta ya viwanda na kuwa moja ya wachangiaji wakubwa wa uchumi kwa hii",amesema Mustafa.

Origin Afrika na Swahili Fashion week inatoa fursa kwa wabunifu wa kuonesha ubunifu wao, na kuwapa taaluma katika masuala ya mauzo kwa ujumla. Hii ni nafasi adimu kwa wabunifu kuitumia ipasavyo katika kuonesha vipaji vyao na pia kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuitangaza kimataifa kwa upana zaidi African Fashion. Picha na Jiachie



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...