NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, BALOZI SEIF IDDI AKICHANGIA MAJADILIANO YA MCHAKATO WA KISIASA KUHUSU SAHARA YA MAGHARIBI AMBAYO KWA MUDA MREFU IMEKUWA IKIPIGANIA KUJITEGA NA SERIKALI YA MOROCCO

NA MWANDISHI MAALUM

NEW YORK

Tanzania imeungana na jumuia ya kimataifa na taasisi zisizo za kiserikali katika kuhimiza Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu kushughulikia taarifa za kuwapo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika Sahara ya Magharibi, inayotaka kujitenga na Morocco.

Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Iddi, ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la 65 la Umoja wa mataifa, uliokuwa ukijadili mstakabali ya eneo hilo la Sahara Magharibi.

Kamati hii inahusika na masuala ya kisiasa na kumaliza ukoloni kwa nchi ambazo kwa namna moja ama nyingine hazijapata uhuru wao kamili au zina uhuru nusunusu.

Balozi Seif Iddi aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaofanyika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, anasema Tanzania inakaribisha tamko namba 1020 la mwaka huu la Baraza Kuu la Usalama linalonyesha kuwa kumekuwapo na ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo.

“Kwa tamko hilo Tanzania inaona kuwa kuna mwelekeko wa kujenga mazingira ya kuaminiana kati ya pande zinazohusika na mwelekeo kuelekea katika kulishughulikia tatizo hilo . Tunaamini kwamba suala hili litashughulikwa kikamlifu na taasisi za umoja wa mataifa yaani baraza kuu la usalama na baraza la haki za binadamu” akasisitiza Naibu Waziri.

Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimekuwa na msimamo usioyumba wa kuisaidia na kuitetea Sahara ya Magharibi kujipatia uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe.

Kwa muda mrefu sasa Sahara ya Magharibi ambayo ilikuwa nchini ya utawala wa Spain hadi mwaka 1976 imekuwa katika mgogoro mkubwa na Morocco ambayo imekuwa ikidai kwamba eneo hilo ni sehemu ya mipaka yake.

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika zimekuwa zikiendesha majadiliano na michakato ya kumaliza mgogoro huo kwa njia za amani.

Kwa mujibu wa Naibi Waziri, Tanzania inakaribisha mazungumzo yasiyo rasmi kati ya serikali ya Morocco na chama cha POLISALIO yaliyofanyika Durnstein, Austria na yale yaliyofanyika Westchester, nchini Marekani.

“Tunahimiza na kushauri pande zote zinazohusika kushiriki kikamilifu na kwa nia njema ili hatimaye kufikia makubaliano yatakayoridhisha pande zote mbili, na hatimaye kuwawezesha wananchi wa Sahara Magharibi kujiamulia mambo yao wenyewe kwa kuzingatia misingi na kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa.

Akaliomba Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kutumia mamlaka iliyonayo kuendeleza mchakato na kumaliza mukwamo wa kumaliza mgogoro huo kati ya serikali ya Morocco na Sahara ya Magharibi.

Akasisitiza kuwa Tanzania inaamini kwamba Baraza hilo na hasa wajumbe wa tano wa kudumu maarufu kama P5 wanawajibu wa kipekee katika jambo hilo na hasa ikizingatiwa nguvu na wajibu wa wajumbe hao katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa.

“ Naomba nitumie nafasi hii kutoa msisitizo wa kuwaunga mkono watu wote ambao bado wako chini ya utawala wa kikoloni, kwamba tunaunga mkono bila ya kuteteleka juhudi zao za kutaka kujikitawala na kujiamulia mambo yao kwa kuzingatia matamko mbalimbali ya Umoja wa Mataifa” akasema Balozi Seif Iddi

Wajumbe wengi wakiliozungumza katika mkutano huo kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa, taasisi na mashirikia yasiyo ya kiserikali wamesisitiza kuwepo kwa njia za amani za kumaliza mgogoto kati ya pande hizo mbili. Ili hatimaye wananchi wa Sahara ya Magharibi waweze kuendelea na maisha yao, wakiwa huru na uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe

Sahara ya Magharibi inabaki kama eneo pekee Barani Afrika ambalo bado ni koloni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ni abu kubwa hadi leo afrika inashindwa kujitoa katika ukoloni ambao ni vyepesi kuliza kwa kutumia umoja wa nchi huru za afrika maana tatizo hili liko katika umoja wa afrika badala ya kutegemea P5.
    afrika fanyeni kazi ndugu zangu kwanini kila kitu wazungu leo tanzania hata kulinda victoria tunataka msaada nje wakati tunalo jeshi halina kazi kila sehemu majambazi eti tunagonja wafadhili ni hatari jamani MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete
  2. waswahili wanasema toa kwanza kibanzikilichopo jichoni kwako ndo utoe boriti iliyo kwenye jicho la jirani yako.Huyu balozi seif idd anaposema ukiukwaji wa haki za binadamu ushughulikiwe huko sahara magharibi anafikiria nini?mbona hafikirii kushughulikia kwanza nyumbani kwake Tanzania?maana hakuna haki za binadam.

    ReplyDelete
  3. Charity starts at home!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...