Ndugu Issa: unanisamehe kwa kushindwa kupost maoni yangu moja kwa moja--niko huku Addis na inaelekea kuna utata na blogs! Haya ni maoni yangu juu ya mdau aleyetuma malalamiko na ushauri juu ya ajira za kampuni za Wakenya ambayo aliyabandika tarehe 10Nov asubuhi. Utanisamehe kwa hadithi ndefu.
Wasalaam- Luno

Mdau wa "Aluta Continyua", INGAWA ALIANZA NA MANUNG'UNIKO MENGI YA KUONEWA, ametoa hoja nzuri sana ya jinsi ya kuhakikisha kuwa mahali popote pale unapofanya kazi, iwe ni kampuni ya Baba yako, ya Mchina, Mwingereza au ya Mkenya, unatakiwa kuzingatia: fanya kazi kwa bidii, tumia muda wa kazi ipasavyo, timiza malengo uliyopangiwa, hakikisha kuwa boss wako wa kazi amejua kuwa umetimiza wajibu wako (kama hakuna mfumo wa tathmini ya utendaji kazi), pale penye mapungufu mwambie ungependa kujifunza zaidi, nk.
Lakini cha msingi zaidi ambacho waajiri wengi wa kutoka nje za wanakwazwa ni tabia za Watanzania wachache maofisini na viwandani (sio wote) kushindwa kutofautisha muda wa kazi na na muda gumzo na mambo ya kifamilia. Je ni mara ngapi unafika ofisi unakuta mtu amekazana kupiga gumzo na rafiki yake au anaongea kwenye simu mambo ya kicheni pati?
Kuomba ruhusa kila wiki ni kawaida, leo anauguliwa na jirani yake (wala siyo ndugu) na kesho mjomba wa babu yake kafariki. Wenzetu huko wanakotoka watu wanajituma sana, na wanafuata sheria za kazi kwa makini sana.
Kumbuka hata hapa hizo sheria zipo lakini tuliamua kuzipuuzia na imekuwa kama utamaduni wafanyakazi kudhani wana haki ya kutembeleana na kupiga gumzo muda wa kazi. Hatujali viwango vya ufanisi--hata nimeona mafundi cherehani akishona shati anaacha nyuzi zinaning'inia-- au ukiingia kwenye mgahawa meza hazijapanguswa na wafanyakazi wamesimama tu wakipiga gumzo. Hilo wenzetu linawakatisha tamaa, maana hujaajiriwa ili kugeuza mahali pa kazi ni sebule ya nyumbani kwako.
Samahani kwa Watanzania ambao hawana hizo tabia, wanachapa kazi kwa bidii-- wako wengi--ndo maana mdau wetu kwenye malalamiko yake hakusema hao Wakenya humfukuza kila Mtanzania.
Jambo jingine ambalo ningependa kugusia ni ile dhana ambayo imejengeka kuwa Mkenya (au mgeni yoyote) akija hapa Bongo akaanzisha kampuni yake na kuajiri, kwa mfano, Wakenya wenzie watano na watanzania kumi na tano, sisi tunalalamika kuwa hawa Wakenya watano wamechukua kazi za Watanzania. Je ni kweli usemi huo? Kwa maoni yangu, ni Watanzania 15 wamechukua kazi za Wakenya 15 kama huyu Mkenya angeamua kufungua hiyo kampuni Mombasa au kupanua ukubwa wa kampuni kule Kenya.
Kwa maneno mengine, mgeni yoyoye, au Mkenya au Mchina, anapokuja TZ na kuwekeza hapa kwa kufungua kampuni (hata kama ni mgahawa), anakuwa amesaidia kuziba pengo la huduma au bidhaa zinayohitajiwa (pengine ni kuboresha tu), na hivyo kutengeneza ajira ya Watanzania. Tukilijua hilo tutaona kuwa malalamiko yetu yangetakiwa kuelekezwa kwa Watanzania wenye mitaji ambao wanashindwa au serikali imeshindwa kuwawezesha kuanzisha hiyo huduma au biashara ili itoe ajira kwa Watanzania.
Angalizo la pili ni kuwa, unapopata mtaalamu (daktari, injinia, mekenika, mwalimu, nk) kutoka nje, ni sisi tunaofaidi kwa maana ya kujaza mapengo ya wataalamu ambao ilitakiwa tuwe tumewasomesha na kuwatengenezea sehemu za ajira. Kimsingi inatakiwa ile nchi ambayo anatoka yule mtaalamu itulalamikie kuwa tumewaibia mtalaamu wao ambao walitumia raslimali yao kumsomesha.
Kwa maelezo hayo, ningependa kurudia tena umuhimu wa kijikagua wenyewe kwa nini waajiri toka nchi za nje wanatulalamkia na hivyo kupata kisingizio cha kuleta wataalamu wao. Kwa hilo narudia kumsufu tena mtoa hoja kwa kutushauri tufanye nini ili waajiri toka nje za nje (ametumia mfano wa Wakenya) wasipate sababu ya kutubadili.
Kanuni alizozitaja zinatakiwa zitumike hata kwa ofisi za serikali, mashirika ya umma na kampuni binafsi za Watanzania wenzetu ili huduma ishamiri kweli kweli. Kumbuka kuwa hakuna bepari ambaye anawekeza mtaji wake ili kupata hasara. Lengo ni faida: hivyo Mtanzania asiye na ufanisi hamfai, lakini pia raia mwenzange kama ni mvivu hamfai, au kama anatoza mshahara mkubwa kuliko Mtanzania mwenye bidii kama yeye,naye hamfai. Hivyo akipata fursa ya kuchangua kati ya watu wawili wenye sifa sawa, Mtanzania na Mgeni, kama mgeni anadai mshahara zaidi atamchukua Mtanzania, kwa vile anataka faida.
Tuache kunung'unika na badala yake tufanyie kazi mapungufu yetu.
Poleni kama nimwekwaza kwa maelezo haya.
Mdau Mzalendo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Ahsante mdau.mimi nasema hivi,Mtanzania ni mwoga sana kuambiwa ukweli na tusipojichanganya hakiyanani tutaula wa chuya dunia hii.wachina,wajapani waingereza hawajapiga hatua kwa kuogopana kuambiwa ukweli.watanzania tuna kasumba ya kununa na longolongo za chini chini bila ku deliver yaani ukilinganisha ni kweli hatuna lolote katika utendaji.kwa kweli tunapoteza muda MWINGI SAAAAANA maofisini halafu tuna unafiki mwingi wawe wakubwa kwa wadogo bila kuwakaribisha hao waliochangamka kwenye ucapitalist hatuendi popote.bisha piga kichwa chini ukweli utabaki pale pale

    ReplyDelete
  2. Thannx God,Tanzania imeanza kupata wasema kweli na wasioogopa kuambiwa kweli,spot on mdau.

    ReplyDelete
  3. Good point taken.Hakuna ubishi.

    ReplyDelete
  4. Sawa kabisa watu wafanye kazi waache majungu kisha kulalamika. Mtu akizembea awajibishwe.

    ReplyDelete
  5. Mimi nilivyokua mfanyabiashara Tanzania, nilishuhudia mwenyewe kuwa Watanzania ni wavivu wa kazi. Watanzania tunapenda story nyingi kazini na kazi hatupendi kufanya.

    Pia, kwa elimu, Wakenya wapo mbele sana kuliko sisi. Ndio maana, ofisi nyingi kubwa za Umoja wa Mataifa na NGOs wapo Kenya na sio Tanzania. Uchumi wao pia ni mkubwa kuliko wetu kutokana na elimu yao na ujuzi wao.

    Kwa kuwa tumewapa ruhusa serikali ya Jamhuri kukubali Tanzania kuwa katika jumuiya hii, ni lazima tuwakubali Wakenya na wennginewe wafanye kazi Tanzania kwa kuwa kuna uhuru wa wananchi wa Jumuiya kufanya kazi popote sasa.

    Nadhani Watanzania bado tupo na siasa yetu ya Ujamaa ndio maana ni tabu sana kufuata matakwa ya "bepari" kazini. Ukiitwa kujieleza kwa nini kila siku unachelewa au unasoma gazeti wakati wa kazi, unaanza kulalamika kuwa unaonewa au "wageni" wana ubaguzi wa rangi.

    Mimi nilikuwa mfanyabiashara mjini Dar es Salaam miaka 15, na najua kuwa kama tajiri, nitampa kazi Mkenya kuliko Mtanzania japo kuw a mimi ni Mtanzania kwa kuwa Mkenya anafanya kazi na kuheshimu kazi yake. Pia Kiingereza chake na elimu yake ni bora zaidi. Tabia ya kikazi ya Mkenya na Mtanzania ni tofauti kabisa. Sisi ni gumzo sana , wao ni kazi sana.

    Maraha ni pesa
    USA (karibu an Mungu)

    ReplyDelete
  6. Tatizo hata mashuleni bado tunafundishwa mfumo wa ujamaa, na unajamaa bado upo akilinimwetu. Wenzetu wanakuja na mfumo wa kibepari ndiyo umetawala vichwani mwao.
    Pia semina zetu ni za kwenda kula tu hakuna mfumo wa kipepari ambao watu wanafundishwa haki zao. Watanzania wengi tumezoea cha urahisi na cha haraka chukuwa chako mapema. Mfumo wa kipeperi ni unatufundisha kufanya kazi na kupata cha haki kutokana na nguvu yako. Tatizo ni lataifa zima tumeshaibiwa na kuonewa kwa sababu hatujui haki zetu na labda hatujui hata tunachokifanya. Nashukuru kwa ujumbe wako mtowa maoni.

    ReplyDelete
  7. Huku Marekani, kuna wakuu wa kazi (CEO) ambao wanapewa mishahara mara 200 kuliko Mfanyakazi mwingine. Kuna sasabu kuu ambayo huyu CEO ana uwezo wa kuzalisha na kuiendesha kampuni kuliko hawa wafanyakazi wengine. Labda ni elimu ya juu, au bidii au alishazalisha sana katika makampuni mengine. Huwezi kusema kuwa tusimpe mshahara mkubwa kwa kuwa hatuko katika ujamaa tena. Market ndio itasema mshahara gani mtu apewe kutokana na ujuzi wake.

    Mimi Mtanzania, nina elimu ya juu ya MBA ya Marekani (biashara, Finance) na ninafahamu lugha tatu za kigeni. Nimefanya kazi katika nchi tatu za ulaya na Marekani. Je, utasema kuwa nikija Tanzania mshahara wangu uwe sambamba na Mtanzania aliyesoma UDSM (Biashara), na hajawahi kutoka nje ya Tanzania au kufanya kazi katika makampuni makubwa ya Kimataifa na asiejua Kiingereza vizuri acha lugha za kigeni?

    Ndio maana, wageni wanapewa mishahara mikubwa zaidi ya Watanzania kwa kuwa wana elimu nzuri zaidi yao na ujuzi mkubwa. Watanzania tunapenda sana kupiga story tu kazini. Mfano mdogo tu ni wa Madaktari Muhimbili. Kama utaumwa wikiendi ujue kuwa hutapata matibabu kwa kuwa wikiendi ni siku ya kunywa sio kufanya kazi kama wenzao ambao wana shifti hata kama ni mkubwa gani, lazime awe karibu na simu wakati wowote na atakuja kukutibu hata saa tisa alfajiri kama akiitwa.

    Mzazi wangu alipata mpasuko wa moyo siku moja na kushindwa kuhema vizuri. Profesa Mtulia Akashindwa kunisaidia wala sijamwona, nikaambiwa kuwa "amelala" japokuwa ni jirani yangu na ilikuwa asubuhi saa nne Jumapili nilipokwenda kuomba msaada. Nilipoenda Uingereza kumtibu mzazi wangu, nikatibiwa na MWALIMU wa Huyo Huyo Profesa Mtulia pale St. Thomas Hospital, LOndon, JUMAPILI saa NNE usiku. Hii ndio tofauti ya tabia za kikazi kati yetu na wenzetu mpaka wanaamua kuleta wafanyakazi wa nchi zao Tanzania.

    ReplyDelete
  8. AMEN! You have said it so well! I wish Tanzanians will take this to heart and work towards developing their country and themselves instead of constant complaints and "kupika majungu" from morning to morning...

    ReplyDelete
  9. points nzuri japo yaelekea ndugu huyu hana first hand experience na hawa watu..
    i have seen and experience this, hawa watu si wazuri kabisa. tumefanya kazi na wachina, waganda, wazungu au south africans...wote hawa si kama kenyans when it comes to other people particulary Tanzanians! wapuuzi sana hawa ndugu zetu.
    ujumbe wangu kwa wa-tz, tujipange na tuwe wamoja. hawa jamaa kwa kawaida they gang on some one, so when necessary na sie tupambane pamoja....UMOJA NI NGUVU

    Note: Ila tufanye kazi si longolongo, no stereotype

    ReplyDelete
  10. Honestly I like working with kenyans,ile spirit,aggressiveness na kujiamini kwao nahisi wameniambukiza kiasi kwamba siwahofii kabisaaa and now I dont see any difference btn me and them lakini ninapokutana na utendaji wa ndugu zangu hasa kwenye mabenki,makampuni ya simu,mashirika ya umma na ofisi za serikali kwa kweli inakatisha tamaa yaani working class yetu bado ni mzigo kwa wawekezaji iwe wa ndani au nje yaani we're not fast moving brand in the global job market unless we CHANGE otherwise we'll remains crying babies forever!

    ReplyDelete
  11. Mimi mwenyewe nasema Mungu akinijalia nikafungua kampuni yangu naajiri watu wa nje tu yani watanzania ni wavivu mno na majungu tuu kazini na kudai mishahara mikubwa wakati mwenyewe elimu ni ndogo.

    ReplyDelete
  12. MkandamizajiNovember 11, 2010

    watanzania acheni uvivu tufanye kazi malalamiko ya kuchukuliwa kazi ni kwa sababu huwezi ndo maana unaachwa na mfumo tuliomo wa kibepari na soko huria unaniruhusu kuchukua mfanyakazi toka popote ulimwenguni right now what sells you is your ability soma piga kazi uone kama hakuna atakayekuhitaji mbona wengi wawezao wako mamtoni kwenye makampuni makubwa tu unayoyajua wewe with huge expertise na wanafanya kazi kwa uwezo mkubwa tuuuu we unashindwa nini? Umetendwa kwa sababu huwezi.......

    ReplyDelete
  13. These are directions to GO..
    Asanteni sana wadau kwa kuelimisha Uma

    Sango, M

    ReplyDelete
  14. Ukwl wabongo ha2jiamin ktk utendaji we2 na hii inatokana na kuwekana kiundugu ktk kaz! 2ache izo bana 2najiabishaaa...

    ReplyDelete
  15. Hivi hao wakenya "educated, aggressive, competent" wanaishi dunia gani? Mbona mimi sijawahi kukutana nao na ninawafahamu wakenya zaidi ya lukuki?

    Ukweli ni kwamba, nyinyi ni watu waoga na mkikutana na wakenya mnaanza kujinyeanyea. Na wao wakishaisikia harufu ya woga tuu basi wanajisaidia wanavyotaka.

    Wakenya ninavyowajua mimi ni walevi mbwa tuu, na usipowaogopa basi hakuna watu waoga na wazembe kama wakenya.

    Jiamini Mtanzania.

    ReplyDelete
  16. Well done friends this is the time for change and if we miss the ship GOD will not help us.

    When we do not get proper service at government offices we are the first to complain.The government can afford such lazy workers because nobody is loosing money.

    When it comes to private company the boss cannot afford to pay lazy people and incur loses.

    Ujamaa days are gone forever,friends.In those times we nationalised every business and people stole left right and centre.What remained were skeletons.WAKE PEOPLE START WORKING HARD.

    ReplyDelete
  17. Kwa mtazamo wangu tatizo la wa-Tanzania ni uvivu, visingizio, na kuwalaumu wengine. Nimeandika hayo katika kitabu changu kiitwacho CHANGAMOTO, ambacho najua wa-Kenya kadhaa wameshakisoma.

    Binafsi, nimeshughulika na wa-Kenya katika nchi yao na huku ughaibuni. Walinikaribisha vizuri nchini kwao, na tunaheshimiana, hata ughaibuni. Soma hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...