Waziri Ally akichangia mada ya libeneke
la Sanaa kila Jumatatu ukumbi wa BASATA
Na Aristides Kwizera wa BASATA
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa jana katika ukumbi wa BASATA huku Ilala Shariff Shamba jijini Dar, Ankal aliweka wazi kwamba blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.
Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.
Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.
Na Aristides Kwizera wa BASATA
Ankal amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani. Mwenyewe anaita kuendeleza Libeneke.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa jana katika ukumbi wa BASATA huku Ilala Shariff Shamba jijini Dar, Ankal aliweka wazi kwamba blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.
Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.
Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.
Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.
Katika kuonesha kwamba teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.
Pitia intavyuu ya Ankal katika BabKubwa
Safi mara moja moja kuelimishana ni jambo la msingi ila waelimishwe na haki zao za msingi ikiwa pamoja na sheria za mirahaba.
ReplyDeleteZAUNUNU-AMSTERDAM
Oyaa Dollarman acha kuwapiga watu kamba.
ReplyDeletemimi shati la ankal tu nilidhani bustani ya mnazi mmoja
ReplyDeleteAsalaam alaykhum ancal,
ReplyDeleteHongera sana kwa darasa ulilotoa naimani wameelewa na watayafanyia kazi. Ukweli muziki unahitaji kujitangaza sana kazi ya msanii haitoshi kujitangaza katika TV au Radio station tu libeneke linasambaa dunia nzima kwahiyo ni njia bora sana ya kujitangaza ili kupanua uwigo wa soko.
Thanks wajina
Chef Issa ( MDGSCA)
Big up Ankal, sote tumefata nyao zako na mafanikio yanaonekana, naimani somo ulilotoa wameelewa na watafanyia kazi ili watangaze sanaa yao.
ReplyDeleteAsante sana libeneke lisonge mbele
Chef Issa