Banda la Tanzania kwenye maonyesho ya utalii
yaliyofanyika mjini Montreal, Canada hivi karibuni.
Mwakilishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bw. Steven Lelo Mallya akihojiwa na waandishi wa habari wa shirika la habari la FUTURMEDIA la Montreal. Waandishi hao walitaka kujua mikakati ya NCAA ya kutangaza vivutio vya Tanzania nchini Canada.
Balozi wetu Canada Mh. Alex C Massinda akihojiwa na waandishi wa habari wa shirika la FUTURMEDIA la Montreal. Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania,
Canada wakiwa kwenye maonyesho ya Utalii ya Montreal. Mheshimiwa Balozi Alex C Massinda akiwa na baadhi ya washiriki kutoka Tanzania waliohudhuria maonyesho ya utalii yaliyofanyika Montreal hivi karibuni.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Tanzania utalii iko juuu sana nawapa hongera sana.....Go Tanzania Goooo

    ReplyDelete
  2. KELAND SCHOOLNovember 16, 2010

    HEBU NISAIDIENI WADAU HIVI TANZANIA SIKU HIZI INAITWA TANZANIE AU NDIO UZUNGUNIZATISHENI????????

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili wameandika hivyo sababu asilimia kubwa ya wenyeji wa montreal wanaongea french, hivyo wameweka kibiashara zaidi wakaona waiandike kwa kifaransa ili wenyeji wavutiwe na banda, na kweli wakafanikiwa,akili kumukichwa eeh!
    mdau montreal

    ReplyDelete
  4. Mimi sina hakika km Tanzania,ina jina la kifaransa.Kweli Tanzania kwa kifaransa ni Tanzanie!Wangeandika tu Tanzania,maana watu walivutiwa vitu,na si jina.

    ReplyDelete
  5. Pongezi TTB kwa jitihada zenu za kuinadi nchi yetu nje ya nchi. Ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa tunapata wageni wengi na kuinua pato la nchi na sekta ya utalii kwa ujumla. Utalii umetoa ajira kwa watu wengi sana, kuongezeka kwa wageni ni neema kwa wengi pia.

    wakati mkiendelea na hayo kwa walio nje, si vibaya mkajaribu pia kuweka mkakati kwa wazalendo ili nao wawe 'watalii' ktk nchi yao na wasiishie kusimuliwa na wageni.

    tembeatz.blogspot.com

    ReplyDelete
  6. Utalii na utamaduni wetu haupendezi bila vazi la asili la kitanzania. Tunatangaza utalii Canada tumevaa suti kama zao, hakuna tofauti yoyote, ndo kwanza tunajaribu kuiga utamaduni na mavazi ya kizungu kuliko wazungu wenyewe. Hivi yale ya West Africa, wenye mavazi yao ya asili sisi yanatushinda nini!?

    ReplyDelete
  7. Hii ya leo kali ..yaani Tanzania kwa kifaransa ni Tanzanie ..kuanzia lini? wewe anony wa Nov 16 usiwafanya watu malimbukeni ..Hapa hao watu waliotumwa kutuwakilisha katika haya maonyesho walikuwa wanaburuzwa tu ..hawajui wanafnya nini..this is totally a wrong approach ya kutangaza nchi.

    Buheti.
    Malmo.

    ReplyDelete
  8. Jina halifana kifaransa wala kimatumbi, hampo wamechemka tu. Ni vema tuitangaza nchi yetu kama ilivyo bila kuichakachua

    ReplyDelete
  9. haya TANZANIE KENYIEN WABONGO UTAWAFANYA UNACHOTAKA

    ReplyDelete
  10. Tanzania kwa Kifaransa ni Tanzanie...kama kenya kwa khisipania ni kenía..hizi ni lugha tu.sisi tunaitwa Ubelgiji ama Belgium (english) wakati wao wabelgiji hawalijui lina hili la kiswahili wala la kingereza bali ni BELGIE kwa kidachi ama BELGIQUE kwa kifaransa....sema wewe hapo mdau Oostende,Koniklijk Belgïe

    ReplyDelete
  11. Tanzania kwa kifarnasa ni TANZANIE kama kwa kiswahili tunaita Ubelgiji ama Belgium (kingereza)lakini wao wenyewe hawayajui majina haya...BELGIE kwa kidachi ama BELGIQUE kwa kifaransa...sasa tufahamu kuwa lugha nyengine majina ya nchi ama ya miji hubadilika,(Italy-Italia,Rome-Roma)kutoka Oostende, koniklijk Belgïe

    ReplyDelete
  12. Tanzanie ni Tanzania kwa Kifaransa. Sielewi tunalalamika kitu gani. Mbona sisi tumezipa nchi za wenzetu majina ya Kiswahili kama Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Ureno, Ubelgiji, nk. Ikumbukwe kuwa majina haya ni ya Kiswahili na sivyo wenyewe wanavyoziita nchi zao.

    ReplyDelete
  13. Namuunga mkono anony wa Tue Nov 16, 05:56:00 PM kwa asilimia 100. Jina Tanzania limeandikwa Kifaransa kwa kuwa maonyesho hayo yamefanyika sehemu ambapo wakazi wake wengi wanazungumza lugha hiyo. Hivi italeta maana kwa Watanzania wanaotembela Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam endapo, kwa mfano, banda la Ujerumani litakuwa na maandishi makubwa yanayosomeka “DEUTSCHLAND”? Hili ni jina la Ujerumani kwa Kijerumani, lakini ni wangapi wataelewa ukweli huu. Tuwe tunafanya utafiti kabla ya kuanika umbumbumbu wetu humu.

    ReplyDelete
  14. Jamaa anashangaa nini wakati yeye England anaita Uingereza?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...