Wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Mpanda mjini na mpanda vijijini wakiwa katika picha ya pamoja mbunge mteule wa jimbo la Mpanda kata Bw Said Arfi (Chadema) wa pili kulia baada ya kumalizika kwa mdahalo wa wagombea ubunge katika majimbo hayo uliomalizika katika ukumbi wa Katavi Mpanda mjini,mdahalo huo uliendeshwa na jumuiko la asasi za kiraia Tanzania na kuratibiwa na asasi ya kiraia mkoa wa Rukwa (Rango) kutoka kushoto ni Juma Shaban (CUF) Said Arfi (Chadema) Ezekia Ndimubenya (CUF , Masanja Katambi ( Chadema) na Masanja Kakofia ( NCCR-Mageuzi ) . Picha na habari na Francis Godwin


Hata hivyo Matokeo ya Uchaguzi wa ubunge ulioahirishwa Oktoba 31 na kufanyika jana Novemba 14 katika majimbo saba yamevipatia vyama vya upinzani viti vinne na chama cha mapinduzi (CCM) viti vitatu.
Katika uchaguzi huo, chama cha wananchi CUF kimeshinda Majimbo ma

tatu ambayo yote ni kutoka upande wa Tanzania Zanzibar nayo ni Jimbo la Mtoni kupitia mgombea wake Faki Haji Makame, Jimbo la Magogoni ambako mshindi ni Hamad Ally Hamad pamoja na Jimbo la Wete mshindi akiwa ni Mbarouk Salum Ali huku CCM ikilipata jimbo la Mwanakwerekwe baada ya mgombea wake Haji Juma sereweji kuibuka na ushindi.

CHADEMA kimefanikiwa kuendelea kushinda katika jimbo la Mpanda Mjini ambapo mgombea wa chama hicho Arfi Said Amour ameibuka na ushindi huo baada ya kupata kura 8075 dhidi ya mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Kapufi Sebastian Simon aliyepata Kura 8026 na Ndimumenya Ezekye wa CUF amepata kura 39.

Majimbo yaliyonyakuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania bara ni Jimbo la Nkenge wilaya ya Misenyi mkoani Kagera na jimbo la Mpanda vijijini Mkoani Rukwa.

Katika Jimbo la Nkenge, mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi Assumpta Mshama amepata kura 23,772 na kuwashinda wapinzani wake ambao ni Amri Sadick wa chama cha wananchi CUF aliyepata kura 606 naWilliam Kweyamba wa Tanzania Labour Party (TLP) aliyepata kura na 597.

Jimbo la Mpanda Vijijini Kakoso Moshi Selemani wa CCM ametangazwa kuwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho baada ya kupata kura 5693 na kuwashinda wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani ambao ni Masanja M Katambi wa CHADEMA aliyepata kura 3260, Shaban J Kisabo wa Chama cha wananchi (CUF) aliyepata kura 74 na Makofira Joseph wa NCCR - Mageuzi aliyepata kura 22.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...