kachero akipekua moja ya mabegi mawili ambayo yalikuwa na bwimbwi hilo wakati wa kupekuliwa kabla mwenyewe hajakwaa pipa la Kenya Airways kuelekea Accra kupitia Nairobi. Kila begi lilikuwa na kilo 6.5 kwenye mifuko maalumu inayotumiwa kusafirisha vifurushi vya kibalozi.

Bwimbwi likiibuliwa toka kwenye moja ya mabegi hayo

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Afande Godfrey Nzowa akikagua moja ya mabegi hayo huku mtuhumiwa akiwa kajishika tama pembeni kuleee....



Mtuhumiwa Kwaku Sarfo toka Ghana akiwa mbele ya kago la bwimbwi lililofumwa kwenye mabegi yake mawili alipokuwa akitaka kusafiri kurejea kwao Ghana kupitia Nairobi. Upelelezi unaonesha alikuja Tanzania Septemba 15, mwaka huu na kuishi hoteli moja maarufu (jina mkobani) huko Mikocheni jijini Dar. Mwenyeji wake (jina mkobani pia) ambaye alimkaribisha na kusadikiwa kula naye dili anasakwa na polisi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Polisi wangetumia gloves jamani. Hiyo ni contamination of evidence.

    ReplyDelete
  2. Hats Off....jeshi la Polisi..wapuuzi hawa wamegeuza nchi yetu transit point ya kupitishia bwimbwi zao...nadhani mwenyeji wake asakwe na aanikwe hadharani ili tumuogope kama ukoma

    ReplyDelete
  3. contamination of evidence!?? kuna mtu alikuambia kuna kesi?? sidhani. mwakani siku kama leo ukikumbuka niambie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...