Kamanda Muhidin Maalim Gurumo

Na Ras Makunja,
Kamanda wa FFU Ughaibuni

Mwanamziki Muhidin Gurumo Kalazwa Hosptalini Muhimbili
ward ya Mwaisela Na.5
Mwanamziki mkongwe wa muziki wa dansi Muhidin Maalimu Gurumo
alimaarufu kama Anko,kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, amelazwa katika hosptali ya Muhimbili,ward ya Mwaisela namba 5 akiwa anasumbuliwa na matatizo ya mapafu kujaa maji.

Mzee Muhidin Gurumo ni baba mwanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz ambayo sasa "Msondo Ngoma Music Band" aka Baba wa Mziki, aka Mambo hadharani.

Anko Muhidini Maalimu Gurumo amekuwa katika medani ya mziki kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950s rasmi mwaka 1960 na akiwa moja ya wanamziki wanzilishi wa Nuta jazz band 1964, kabla ya kubadili jina na kuitwa JUWATA JAZZ ikiwa chini ya chama cha wafanyakazi.

Anko Gurumo ni mwanamziki mtunzi,mwimbaji mkongwe na mbunifu wa mtindo mbali ya dansi kama vile Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae (alipokuwa Mlimani Park) na Ndekule (alipohamia kwa muda Orchestra Safari Sound wana OSS) n.k yeye akiwa ndie anayetoa majina haya.

Mzee Gurumo ni Baba wa mziki wa dansi nchini na pamoja kuwa amewahi kupigia bendi nyingi lakini "Msondo Ngoma Music Band" ndiyo ngome yake.

Ras Makunja na Globu ya Jamii inamwomba Mwenyezi Mungu ampe afueni Kamanda wetu Mzee Gurumo. Na pia wadau wa muziki tujitokeze kumsaidia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Oough my god! Get well soon mkubwa!
    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  2. Mume Wangu, Mikanjuni TangaNovember 27, 2010

    Ankal, hizo Breaking Nyuuuuz zako nyingine zinatushtua sana, hebu jaribu kuzirekebisha kidogo ili zitofautiane kati ya zile za Ajali, Kifo, Ugonjwa,Burudani, Siasa, Machangu, kina kaka poa Rambirambi,Kumbukumbu na masuala mengine ya uchaguzi na udaku.

    ReplyDelete
  3. Michuzi uzito wa hii habari ni kama vile jamaa amefariki,mapafu kujaa maji kiutaalamu pnomonia ni ugonjwa wa kawaida na si suala la kutangaziana breaking news na kuanza kuelezea wadhifa wa mgonjwa,anyway Dr.michuzi thanks kwa kuleteletea news mbalimbali.
    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  4. michuzi mbona unatutisha breaking nyuuz ni kitu hatari kuumwa usiweke breakingnyuuz tafuta usemi mwengine mi nilizani amefariki

    ReplyDelete
  5. Nkonongwa, MafiaNovember 27, 2010

    Habari imenibabaisha sana hii, nilianza kupiga simu kwa jamaa wa Kisutu Cemetery watupatie nafasi karibu na tulipomhifadhi 'Jenerali' wa soka Juma Mkambi, Mwenyeezi Mungu amuweke kwenye Bustani ya RAHA.
    Utoaji wa Breaking News urekebishwe kidogo Ankal.

    ReplyDelete
  6. aliyetoa hii inabidi asilete tena katika mfumo huu. seriously i knew the guy is no more, kumbe kalazwa tu. anyway asanteni kwa taarifa.

    ReplyDelete
  7. Kwanza nampa pole Mzee wangu, Msanii wangu, Mshauri wangu, mwanamziki wangu na kipenzi changu katika mziki, Mzee Gurumo. Mungu amponye na maumivu yanayomsumbua arudi katika shughuli zake na tumsikie akito raha jukwaani kama ilivyo kawaida yake

    Pili, namuunga mkono mtoa maoni aliyesahauri kuwa tuwe na jinsi ya kutofautisha breaking news. Hakika mimi niliposoma kichwa cha habari nilishtuka sana. Inawezekana kwa sasa hatujawa na vichwa vya habari muafaka lakini ni changamoto kwa waandishi kuonyesha ubunifu wao. Mi napendekeza tutumie kichwa kama "AMELAZWA, ANAUMWA N.K" hii itapunguza mshtuko kidogo.
    Naomba kuwasilisha. HASANTE

    ReplyDelete
  8. pole ngurumo maradhi hayo ni ya kawaida kama maradhi mengine

    ReplyDelete
  9. unajua watoa maoni wengine ni watu wa nongwa za uswahilini,sasa kuna kosa gani habari hii ikiandikwa kuwa breaking news? kama mwanamziki huyu maarufu kalazwa hosptilini? au mlitaka breaking news lazima iwe kwa mwanasiasa na viongozi wa dini? tujaribu kuwa waungwana,wanamziki ni kiungo muhimu katika jamii,msilete unafiki wa kumpiga vita Ankal kwa kuwa anaongoza katika libeneke

    ReplyDelete
  10. Mzee Gurumo tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu upone haraka na uendelee na kazi yako ya mziki kama kawaida.

    Bado tunahitaji nyimbo zako za nasaha na upendo kwa Watanzania wote.

    Wewe ndiyo katika nguzo chache za muziki wa asili wa bendi.

    ReplyDelete
  11. DR Michuzi naona ni heri ukituhamishia michuzi post kwasababu humu naona tuna banana. Sasa tukianza kposti na wanaolazwa tutamaliza leo kweli.

    Mwee ni mtu mashuhuri lakini huo ugonjwa mbona wa kawaida au mlishaanza kugawa na mali?

    Get well soon na mungu akujalia upate speed recovery na ukitoka hospital uwakalie kikao hao wadaku

    ReplyDelete
  12. Ugua pole Muhidini Maalimu Gurumo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...