Ni wakati wa mazishi ya 'Jenerali' Juma Mkambi katika makaburi ya Kisutu jijini Dar ambapo mamia ya wapenzi wa soka, ndugu jamaa na marafiki walijitokeza kumuaga kiungo huyo nyota wa Taifa Stars na Yanga aliyetutoka Jumapili alfajiri. Pamoja na mambo mengine marehemu Juma Mkambi atakumbukwa kuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Afrika huko Nigeria mwaka 1984 na alifunga bao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. BW MISUPU ACHA KUCHAKACHUA FACTS. NI KWELI TUNASIKITIKA KWA KIFO CHA JENERALI JUMA MKAMBI KWANI HUYU JAMAA ALIKUWA NI MCHEZAJI WA HALI YA JUU SANA NA NI MMOJA WA WACHEZAJI WACHACHE AMBAO KAMA NINGEKUA NA UWEZO NINGEMPELEKA KUCHEZA ULAYA ENZI ZAKE. KWA WALE WASIOMFAHAMU UCHEZAJI WAKE ULIKUA NI KAMA PATRICK VIERA.

    HATA HIVYO UKWELI NI KWAMBA TAIFA STARS HAIKWENDA NIGERIA KWENYE MICHUANO HIYO MWAKA 1984 BALI NI 1980.

    AIDHA JUMA MKAMBI HAKUFUNGA GOLI. MECHI YA KWANZA TAIFA STARS ILIFUNGWA NA NIGERIA 3-1 , YA PILI NA MISRI 2-1 NA YA TATU SARE NA IVORY COAST 1-1. MAGOLI YOTE HAYO MATATU YA TAIFA STARS YALIFUNGWA NA THUWENI ALLY WINGA NO. 11 WA SIMBA. KATIKA MICHUANO HIYO YA NIGERIA MCHEZAJI WA TZ ALIYEONDOKA NA SIFA LUKUKI NI JUMA PONDAMALI MENSAH

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi!! Ni mwana wa Tanzania aliyeitumikia nchi yake kwa moyo wake wote licha ya kipindi hicho kutokuwa na maslahi kama sasa!!

    Je sasa kwa nini hatuvutwi na utumishi uliotukukuka kama wa watu kama hawa??

    Tumelewa uhuru??, au tumekata tamaa?? Vipaji vyote hatuna mtu kwenye UK Premier, au hata ligi kubwa duniani??

    Na hii ni katika nyanja zote, sio michezo tu!!

    Rai yangu naomba turudishe juhudi, tucheze nafasi zetu tulizopangiwa kwa uadilifu mkubwa, kama Jenerali alivyokuwa akikaa vizuri pale namba sita, huku akipewa ushirikiano mzuri kutoka nyuma kwa Kinye, Amasha, Bana, Chuku, n.k na kuwapatia "vyumba" vya ushindi kina Mkwasa, Mziba, Makumbi, Omari, n.k.

    Tukienda kama timu tutafanikiwa!!

    mambo ya itikadi za vyama yaishe wakati wa chaguzi, baada ya hapo, Tanzania Kwanza!! Tanzania Mbele!! sio chama kwanza au mambo mengine ya kibinafsi!! Busara nyingi zitumike kumaliza tofauti za kisiasa!!

    Idumu Tanzania!!

    ReplyDelete
  3. Mungu aiweke roho ya Marehemu katika amani ya milele.
    Michuzi historia uliyotoa ni ya uwongo, moja marehemu hakuwa kufunga goli katika michuano hiyo.
    Mbili Tanzania ilishiriki mwaka 1980 na wenyeji wa mashindano walikuwa Nigeria.
    Tatu mwaka 1984 Ivory Coast ndio walikuwa wenyeji wa mashindano hayo.

    ReplyDelete
  4. RIP Juma mkambi.
    He was very fantastic boy.
    mdau Norway

    ReplyDelete
  5. Ni Mwaka 1981 wakati wakisaka nafasi ya kushiriki World cup ya 1982 kule Spain.

    Walikutana na Green Eagles, ktk mchezo wa kwanza kule Nigeria matokeo yalikuwa ni 1-1 ni Juma Mkambi ndiye aliyefunga goli la kusawazisha.

    Mchezo wa pili hapa Dar tulikula 2-0, nadhani mtamkumbuka Tungi Banji na John Chedozie (aliyekuwa akichezea Everton) ndio waliotumaliza, licha ya Mohamed Salum na Peter Tino kupoteza nafasi kadhaa.

    Ni mechi hizi ndio zilizomtoa Mohamed Salum jumla hakurudi tena kucheza mpira hapa kama wanavyorudi vijana wenu.

    ReplyDelete
  6. R.I.P Brother. Ni masikitiko makubwa kwa washabiki wa Yanga.

    ReplyDelete
  7. kwahiyo kumbe u kibonde stars iliuanza zamani ee, afu mnatudanganyaga zamani bolu lilikuwa la ukweli

    ReplyDelete
  8. Poleni familia ya Mkambi

    ReplyDelete
  9. R.I.P Jenerali Juma Mkambi.
    Mengi yaliyosemwa humu yamenikumbusha mbali sana nakumbuka miaka hiyo ya 1980 hadi 1985 nilikuwa mdogo sana lakini nilimpenda sana mchezaji huyu haswa anapotangazwa radioni. Nakumbuka miaka ya 1983 kama sijakosea tulikuwa kule Mwanza na nikaenda GOLANI kule milimani kuchungulia wakati huo YANGA ikipepetana na PAMBA ya Mwanza kama siyo Coop United.
    Sasa tumejifunza nini? Juma Mkambi alikuwepo na alijitoa mhanga na kuipigania nchi yake 'kimichezo' lakini inanisikitisha TFF yetu wao ni kuangalia MAPATO tu! Mlangoni hawana hata utaratibu wa kuwaenzi wachezaji wetu kama hawa. Sioni katika picha hata mwakilishi mmoja toka TFF. Hivi wao wapo kwenye mapato tu! Nalia sana kila nikiona wachezaji wetu nyota wanaadhibika na MAISHA mtaani Angalia JELA MTAGWA mchezaji ambaye alitoka hadi kwenye STAMP na sisi wakati tunasoma tukawa tunabandika kwenye MADAFTARI lakini leo amekuwa omba omba TFF iko wapi jamani? Hatuna hata HALL OF FAME ya Wachezaji wetu? Juma Mkambi ameshazikwa watoto wetu watamkumbuka vipi? Hii ni changamoto kubwa kwa TFF yetu, pale viwanjani kwetu hakuna hata sehemu ya ku-display picha na kumbukumbu za WACHEZAJI wetu tunawaenzi vipi?. TFF ni ya mapato Tu Mlangoni! Come-ON Tenga na kundi lako la walaji hapo! Hivi kina Sunday Manara, Othman Mambosasa, Ezekiel Grayson "JujuMan", Madata Rubigisa, Daniel Poka, Mrage wa Kabange, Malota Soma " Ball jugler", Zamoyoni Mogella " Golden Boy", Danny Mhoja (R.I.P),Juma Amiri Maftah, wote hawa tunawaenzi vipi? Hakuna utaratibu kabisa wa hata kuweka kumbukumbu na Historia zao Jamani! Kazi Mapato tu ya Mlangoni....!
    Inapaswa katika Uwanja wetu Mkubwa tuwe na wachezaji wetu Nyota ambao wamefanya mambo makubwa wawekwe kwenye " Walk Of Fame" ili kila tunapokwenda kuangalia mpira tupite kwenye hizo sehemu tuone picha na majina yao na history na hii itawapa changamoto. Na huko Mikoani walipotoka kina Hamisi Thobias Gaga " Gagarino" pale Jamhuri stadium kuwepo na sehemu ya kuweka picha na kuwe na utaratibu wa induction to the hall of fame na ziwekwe category. Siyo kazi ya kudhibiti mapato tu.
    R.I.P Brother Jenerali Juma Mkambi

    ReplyDelete
  10. Tuwe na utaratibu wa kuwaenzi mashujaa kama hawa kabla hawajafariki. Kwa kuanzia tunaweza kutengeneza vitamburisho kwa ajili ya wachezaji waliochezea timu ya taifa ili waweze kuingia bure uwanjani wakati timu ya taifa ikicheza, vile vile vilabu vikubwa vya Simba na Yanga wafanye hivyo katika michezo yao kwa wachezaji waliozichezea. Ingawaje njia hii haiwaongezei kipato ila ni ukweli kwamba wengi wao kwa sasa hawana hata fedha za kuingia uwanjani na inatia aibu na simanzi tunapokutana nao uwanjani wakibembeleza waingie bure maana walinzi wa uwanja ni vijana wa siku hizi ambao hawatambui michango yao. Wachezaji hao sio wengi kwa hiyo hawataathiri mapato.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana wafiwa na Mungu amlaze pema peponi marehemu.

    Msimlaumu Ankal, enzi hizo alikuwa bado dogo ndoo kwanza anaanza kucheza black and white camera ya urithi.

    ReplyDelete
  12. MZEE MWINYI AMIRINovember 24, 2010

    HABARI ZA LEO WANAMAONI WENZANGU KWA KWELI MACHACHE YANGU NINAYOTAKA KUTOA NI KWA YULE MKOSOAJI WA SAA 12-54 CHA KWANZA YEYE MWENYEWE HAJUWI LAKINI ANATAKA KUKOSOA ASIYEJUWA. NIMEMSAMEHE MDOGO WANGU MICHUZI ANAJITAHIDI KUTUPA HABARI LAKINI KIPINDI KILE CHA MWAKA 1980 TANZANIA ILIPOPOKEA KIPIGO CHA MABAO 2-0 DHIDI YA NIGERIA ALIKUWA DOGO BADO ANATOKA KAMASI LAKINI WEWE UNAYEDAI KUMKOSOA SIJUWI ULIKUWAJE MAANA UNAPOTOSHA UMMA. UKWELI NI KWAMBA NI KWELI TZA TULIFUNGWA MABAO 2-0 NA NI KWELI MFUNGAJI WA BAO LA KWANZA NI JOHN CHIDOZIE LAKINI BAO LA PILI LILIFUNGWA NA SEGUN ODEGBAMI NA SIYO TUNGI BANJI KAMA ULIVYOMUITA KIMAKOSA (SAHIHI NI OLATUNJI BANJO AU TUNJI BANJO) NA PIA CHIDOZIE ALIKUWA ANACHEZEA COVENTRY CITY SIYO EVERTON. NAWASHAURI WADAU TUNAPOKOSOA TUWE NA UHAKIKA VINGINEVYO TUTAPOTOSHA ZAIDI.

    ReplyDelete
  13. Tutam-miss sana JM!
    Wakazi wa Tumbi Kibaha.
    RIP

    ReplyDelete
  14. Asante Mzee Mwinyi kujazia taarifa, kama walivyo ma- star jina la Tunji lilifupishwa tu kama ilivyo Segun ingawa jina lake kamili ni Patrick Olusegun Odegbami.

    Ni kweli Chiedozie hakuwahi kucheza Everton lakini pia hakuwahi kucheza Coventry City bali alicheza Leyton Orient, Notty County na The Spurs.


    Pia huyu Segun hakufunga goli la pili ktk ushindi wao wa 2-0 dhidi Taifa stars, bao lile lilifungwa na Christian N'Wokozhi.

    Najua umepoteza kumbukumbu kwa sababu ya uzee.

    ReplyDelete
  15. RIP General,Mungu aiweke mahali pema roho yake
    Umgambile Juma Mkambi,he is fantastic player,he plezs twu positions at the samu taimu,he genda he irudi kwa wale watani wangu Wahaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...