Salam Ankal

Urban Pulse Inawaletea video fupi kuhusu ziara ya Diamond nchini UK kwa ajili ya kuchangia vita dhidi ya Malaria. Tarehe 03.11.2010 Timu nzima Ya Urban Puse ikiwa na Diamond walipata fursa ya Kutembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kumtambulisha Diamond na kutoa shukrani.

Urban Tour itaanza Rasmi jumamosi tarehe 6.11.10 Milton keynes Club Opus ikifuatana na Croydon London tarehe 12.11.10

Asante sana,

Urban Pulse Creative

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. "Tumempoteza kocha Mziray,"she" was a healthy man....
    Halafu Diamond,summer imeisha na huko uliko hakuna jua. Hiyo miwani weka utavaa ukirudi. Haya michuzi nibanie na hii..

    ReplyDelete
  2. hivi mijitu mingine haiwezi tu kuongea kiswahili mpaka ichanganye na kiingereza, inakera!!

    ReplyDelete
  3. Saaaasa wajomba mbona adress hakuna, sisi wengine siyo watu wa club, ilipo hiyo club mtakayofanyia shoo sipajui na huku ulaya kuuliza uliza noma, tupeni postcode tuje kuchangia vita dhidi ya maleria.

    ReplyDelete
  4. Namuunga mkono huyo jamaa wa pili hapo kwamba hii imekuwa ni tabia ya watanzania wengi wanoishi nje wanapenda kuchanganya kingereza na kiswahili sana sana wakiwa wanongea na waswahili wenzao ilimradi tu waonekane wanatema yai wakati kiwango chao cha ngeli ni cha kima cha chini.Ni ukweli unaojidhihirisha kwamba watu hawa japokuwa wanaelimu lakini hawajaelimika vya kutosha kuelewa mipaka ya kuitumia elimu yao vizuri mimi binafsi napenda kuwambia wajitahidi kubadilika wanapokuwa na wa swahili wenzao hizi fikra za kudhani kingereza ni cha maana kuliko lugha mama ni fikra potofu tujivunie kiswahili chetu kwani kingereza ni yebo yebo hakina dili sana kila mtu anakijua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...