Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr. Ali Mohamed Shein akila kiapo cha kuiongoza Serikali ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akila kiapo cha urais mbele ya jaji mkuu wa Zanzibar Hamid Mahamoud(kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan Stadium mjini Zanzibar leo asubuhi.Katikati anayeshuhudia ni rais wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume.
Rais Wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume akimpongeza na kumkabidhi miongozo ya kazi Rais Mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za kuapishwa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar leo asubuhi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia Taifa katika sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa awamu ya saba wa Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikaguwa gwaride la vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama, baada ya kula kiapo kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Amani leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya Dr.Shein kuapishwa mjini Zanzibar leo asubuhi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimpongeza mumewe Dr.Ali Mohamed Shein muda mfuoi baada ya Dr.Shein kuapishwa kuwa Rais Mpya wa Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mshindi wa pili katikA KINYANG’ANYIRO cha urais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimaina na mgombea Mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo asubuhi.Katikati ni Mshindi wa pili katika mbio za urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Shariff Hamad.
Sehemu maalum iliyoandaliwa rasmi kwa kuapishwa kwa Rais Mpya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dr. Ali Mohamed Shein.
Vikosi mbali mbali vilivyoshiriki katika gwaride la kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar,kikiondoka uwanjani hapo.
Wananchi na wanachama wa vyama mbalimbali wakiwa katika sherehe ya kuapishwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein zilizofanyika leo katika uwanja wa Amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mhe. Dkt. Shein mungu akutie nguvu katika jukumu jipya unalolianza leo katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2010 - 2015 kila la kheri Mhe. HONGERA HONGERA HONGERA

    ReplyDelete
  2. Zanzibar ni Njema atakaye na aje, imedhihirika zaidleo. Ewe Mungu Muweza! tunakuomba utudumishie umoja wetu Wazanzibar (na Watanzania kwa ujumla), ujaalie visiwa vyetu vifikie maendeleo endelevu kwa haraka.

    Ishallah Mungu muweza! utuepushe na kila balaa katika kipindi hiki kigumu cha uanzishwaji wa Serikali MPYA na PENDWA ya Kitaifa. Wabadilishe nia wale wote wasiotakia wema umoja wetu huu. AMEEN.

    Mpenda Umoja.

    ReplyDelete
  3. Mama Shein! Mkumbatie kumpongeza Mumeo. Kupata yeye.. wewe wafaidika maradufu.

    ReplyDelete
  4. This is just too cute.. wow, CCM oyeeee. Yani na bado, tutaona nani ataangukia PUA, pambafff zenu!

    ReplyDelete
  5. KARIBU DR.SHEIN WANZANZIBARI TUMERIDHIA IJAPOKUA TUMEPUNJWA ILA SASA WEWE NDIO MKOMBOZI WA MAISHA YA DHIKI YA WAZANZIBARI NA HASA KULE PEMBA,JAHAZI UNALO WEWE USILIENDESHE MRAMA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.....

    ReplyDelete
  6. Mie nashauri tuanze kumuita Maalim Seif naye kama Dr Maalim Seif. Maana viongozi wote wanajipachika u-dakta siku hizi.

    ReplyDelete
  7. yaani mamsap anatoa handshake only...angekuwa mume wangu angepata french....

    ReplyDelete
  8. wameonye kukamaa kwa siasa,si yule kiongozi wa chadema ameanza kuongea habari za kumwaga damu kwani ni lazima awe rais

    ReplyDelete
  9. zanzibar wameonyesha jinsi walivyokomaa kisiasa,siyo kiongozi wa chadema ameanza kwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kukataa matokeo,cha ajabu anaanza kuongea habari za umwaga damu,hivi nilazima awe rais,nimemshangaa sana huyo kiongozi wa chadema baada ya kusikiliza radio bbc swahili; ni mtu hatari kizazi hiki siyo cha vita,

    ReplyDelete
  10. Mama shein basi hata kumkumbatia mumeo umpe hongera mmmmh ni mikono tu? ningekuwa mie hapo ni bonge la hug na kiss la nguvu, wacha waswahili mseme ndio tushauchinja

    ReplyDelete
  11. no comment

    ReplyDelete
  12. kwa kweli naamini Dk. Ali Mohamed Shein kashinda ki halali , hila naamini pia CCM wamempendekeza kama kama mbinu ya kushinda tu. jamaa anaonekana ni mtu safi na mpole na mpenda maendeleo.hila hatatumika na ccm kama bendera tu ! hatakuwa anafata upepo tu, kutoka main land !!

    Mdau numberi ONe

    Paris

    ReplyDelete
  13. M/Mungu ibariki Zanzibar na watu wake huu ni mwanzo mzuri sana wa maendeleo kwa waZanzibar.

    Yeah, nimesikia Dr.Slaa amekwisha anza uchochezi,eti hakubali matokeo, uchaguzi urudiwe! huyu jamaa sasa naona amepata bichwa kubwa sana....kweli ameamsha watu na kusaidia upinzani kunyakuwa viti vya kutosha vya ubunge na udiwani lakini yeye kuwa RAIS bado, na hilo analijua.

    Kama anafikiria uchochezi-chochezi hautamuathiri nafikiri yuko kwenye ndoto kwani yeye ndiye atakuwa wa kwanza kukiona cha mtemakuni,mambo yatakapoharibika, labda tayari anayo sehemu ya kukimbilia nje ya nchi na hao wanaomsukuma kutuletea vurugu ndani ya nchi yetu.

    Dr. Slaa wacha tume imalize kazi yake, na matokeo yatangazwe, baada ya hapo ndiyo unaweza kuleta matatizo yako au kwenda mahakamani, siyo kuwashawishi vijana kuleta vurugu na kuigawa nchi katika makundi.

    ReplyDelete
  14. Mtoa maoni alosema watu wanajipachika UDAKTARI NA SEIF AITWE NYAMAZA KAMA HUNA CHA KUCHANGIA,DR.SHEIN ANA PHD YA MAMBO YA KIZAZI ALIYOPATA UNIVERSITY OF NEWCASTLE UPON TIME HEBU NENDA WIKIPEDIA KAANGALIE HISTORIA YAKE,NI WACHACHE WENYE TAALUMA HIYO KAMA VILE DR.GHARIB BILAL YEYE NI MWANASAYANSI WA NYUKLIA ANGELIKUA IRAN ANGEKUA WANTED KWA MAREKANI LAKINI KWA VILE TANZANIA HATUNA NUKLIA NDIO MTU WA KAWAIDA.NAYE ANA PHD YA SAYANSI YA NUKLIA NA MIONZI NA UNAPOPATA PHD UNACHUKUA SIFA YA DR.SI LAZIMA AWE DAKTARI WA SPITALI HIYO NI HESHIMA YA JUU KIMASOMO.MASTER OF PHILOSOPHY PHD

    ReplyDelete
  15. Haya ndio mambo tunayotaka kuona watanzania kuungana, viongozi kuonyesha njia ya mshikamano bila kujali itikadi za kisisa.

    Zanzibar na Tanzania kwa ujumla tuko nyuma sana, mda wa kurumbana wenyewe kwa wenyewe hatuna jamani. Tuchangamke kuleta maendeleo kwa ajili ya wananchi wote.

    Msemaukweli.

    ReplyDelete
  16. Amani si sembe wala chips kwamba unauzwa Hotelini, vunjeni misingi yake.......halafu endeleeni kusema sie ni kisiwa cha "amani" Walioharibikiwa yaliwakuta baada ya kuendekeza dhulma, upendeleo na kubebana!
    Ankal bora hii uiweke kwa faida yetu sote!

    ReplyDelete
  17. huyo mpambe wa Rais naona bado anapeta, alianza na Komandoo akarithiwa na Karume sasa yuko na Dakta,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...