Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati CECAFA Bw. Nicolas Musonye akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia maandalizi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2010 yanayotarajiwa kuanza Novemba 27 hadi Disemba 11 mwaka huu. Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu huyo wa SECAFA Bw. Nicolas Musonye amesema timu 12 zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambao ni Wenyeji Tanzania,Kenya, Burundi, Uganda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia, Sudan, na ytimu zilizoalikwa ni Ivory Coast, Zambia na Malawi.
Mtendaji Mkuu wa SBL Bw. Richard Wells amesema SBL itahakikisha timu zote zinapewa huduma zote muhimu wakati zitakapokuwa hapa nchini kwa ajili ya mashindano ikiwa ni pamoja na Chakul, Mlazi na Usafiri wa ndege na itatoza zwadi kjwa washindi zinazofikia dola za Kimarekani elfu 60.000 ikiwa ni sehemu ya udhamini ambao ni dola za kimarekani laki 450.000 ambapo mshindi wa kwanza atajipatia dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 huku mshindi wa tatu akijinyakulia dola 10.000. Kampuni ya Serengeti Breweriers ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Tusker Chalengfe Cup 2010 kwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya SBL Caroline Ndugu akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo wakati Shirikisho la vyama vya mpira wa Miguu Afrika Mashariki na kati lilipozungumzia mashindano ya Tusker Challenge Cup yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini hivi karibuni kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda, kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa SECAFA Nicolas Musonye, Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga na Mkurugenzi wa SBL Richard Wells.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. CECAFA NA SIO SECAFA

    ReplyDelete
  2. Aliyeandika SECAFA atakuwa na elimu ya darasa la saba tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...