POLISI NA MAGARI MABOVU
YA KUBEBA SARUJI-WAZO
WADAU,
NIMELAZIMIKA KUANDIKA HAYA KUTOKANA NA AJALI ZA MARA KWA MARA ZA MALORI HAYO TOKA KIWANDA CHA SARUJI WAZO NA MACHIMBO YA MCHANGA BOKO NA BUNJU. JUZI ALFAJIRI LORI MOJA LILIACHA NJIA NA KUTUA KWENYE DUKA MOJA PALE TEGETA KIBAONI, HII NI MARA YA PILI NDANI YA WIKI TAKRIBAN MBILI BAADA YA AJALI KAMA HIYO KUTOKEA HAPOHAPO! WAKAZI WA TEGETA NA PAMOAJA NA WATUMIAJI WA BARABARA YA BAGAMOYO TUMEKUWA KATIKA HALI YA WASIWASI KUTOKANA NA AJALI HIZI AMBAZO CHANZO CHAKE NI UBOVU WA MALORI YANAYOBEBA SARUJI NA MCHANGA.
HALI YA KUSHANGAZA;
· KUNA KITUO CHA POLISI NDANI YA ENEO LA WAZO; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI ? JIBU NI RAHISI RUSHWA!
· KWA NINI UONGOZI WA KIWANDA UNARUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA KIWANDANI NA KUPAKIWA SARUJI? KUNA RUSHWA? MFANO; KUNA MAGARI MENGI KWA JINA ' KOMBE' MENGI NE HAYANA HATA BIMA WALA LESENI ZA BARABARANI LAKINI YANATEMBEA KARIBU BARABARA ZOTE ZA DAR KUSAMBAZA SARUJI.
· KIWANDA CHA SARUJI MBEYA( TEMBO CEMENT) HAKIRUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA ENEO LA KIWANDA; KWA NINI WAZO (TWIGA)WASIIGE MFANO HUO?
· KUNA KITUO CHA POLISI ENEO LA TEGETA; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI NA KILA MARA POLISI WAPO BARABARANI? JIBU NI RAHISI RUSHWA!
WADAU,
NIMELAZIMIKA KUANDIKA HAYA KUTOKANA NA AJALI ZA MARA KWA MARA ZA MALORI HAYO TOKA KIWANDA CHA SARUJI WAZO NA MACHIMBO YA MCHANGA BOKO NA BUNJU. JUZI ALFAJIRI LORI MOJA LILIACHA NJIA NA KUTUA KWENYE DUKA MOJA PALE TEGETA KIBAONI, HII NI MARA YA PILI NDANI YA WIKI TAKRIBAN MBILI BAADA YA AJALI KAMA HIYO KUTOKEA HAPOHAPO! WAKAZI WA TEGETA NA PAMOAJA NA WATUMIAJI WA BARABARA YA BAGAMOYO TUMEKUWA KATIKA HALI YA WASIWASI KUTOKANA NA AJALI HIZI AMBAZO CHANZO CHAKE NI UBOVU WA MALORI YANAYOBEBA SARUJI NA MCHANGA.
HALI YA KUSHANGAZA;
· KUNA KITUO CHA POLISI NDANI YA ENEO LA WAZO; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI ? JIBU NI RAHISI RUSHWA!
· KWA NINI UONGOZI WA KIWANDA UNARUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA KIWANDANI NA KUPAKIWA SARUJI? KUNA RUSHWA? MFANO; KUNA MAGARI MENGI KWA JINA ' KOMBE' MENGI NE HAYANA HATA BIMA WALA LESENI ZA BARABARANI LAKINI YANATEMBEA KARIBU BARABARA ZOTE ZA DAR KUSAMBAZA SARUJI.
· KIWANDA CHA SARUJI MBEYA( TEMBO CEMENT) HAKIRUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA ENEO LA KIWANDA; KWA NINI WAZO (TWIGA)WASIIGE MFANO HUO?
· KUNA KITUO CHA POLISI ENEO LA TEGETA; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI NA KILA MARA POLISI WAPO BARABARANI? JIBU NI RAHISI RUSHWA!
TAHADHARI KWA KAMANDA WA POLISI DSM NA IGP MWEMA;· MHE. RAIS HUTUMIA NJIA HII KWENDA NA KURUDI KWAO BAGAMOYO HALI ISIPODHIBITIWA TUTASHUHUDIA MAAFA MAKUBWA YA AJALI KATIKA MISAFARA HASA PALE TEGETA KIBAONI NA KWINGINEKO BARABARA YA BAGAMOYO
· POLISI WA WAZO NA TEGETA WAHAMISHWE KWA SABABU WAMEKUWA WAZEMBE KUDHIBITI AJALI ZINAZOHUSISHWA NA UBOVU WA MAGARI YA SARUJI NA MCHANGA YANAYOTUMIA BARABARA YA BAGAMOYO.
Wadau naomba kutoa hoja.
Mdau
USIOMBE SASA UKUTANE NA YALE MATIPA YA SKY BLUE YALE, MATIPA HAYANA HATA BREAK HATARI KWELI KWA WATOTO MITAANI, NA WAENDESHA MAGARI. TANZANIA BWANA TUSHAZOEA HATA POLISI WANAWEKWA SEHEMU ZA MATAJIRI SEHEMU MASIKINI TUNAAMBIWA TUWE SUNGUSUNGU WENYEWE.
ReplyDeleteNaunga mkono swala hili. Wazo langu ni kutuma copy ya hii text kwa IGP na Ikulu pia, ili wakubwa waelewe chanzo cha ajali hapo na ajali ambazo zinaweza kutokea(pending). Nilijifunza kutokana na uzoefu, ukilalamika kwa mkubwa, kuna nafasi ya kusikilizwa kwa sababu mkubwa atatoa maelekezo kwa mdogo wake, kuliko ukianzia ngazi ya chini, kuna uwezekano malalamiko yasifike kwa mkubwa.
ReplyDeleteWalifanya zoezi la ukaguzi wa magari kwa wiki moja tu nalo lilijaa rushwa tu!!tena ni baada ya lori kutimka lenyewe na kugonga gate kuu la wazo na likiwa na cement na bila dereva!!! Hoja ilijitokeza ni kwa nini magari aina zote yapimwe kwa kutumia mtambo wa Scania? magari ya mjomba Usangi hardware yatasomeka kwenye mashine Hizo?
ReplyDeleteWewe vipi? Mbona hayo ni mapya! Haujayaona yanayobeba taka? Na mabreakdown mabovu yanayopaki kwenye vituo vya polisi ambayo mengi ni mabaki ya Landrover.
ReplyDeleteJamani mimi nazani tunatakiwa kuchukua hatua kwasasa, tatizo ni kuwa hata ukisema uende kuwaona ndugu zetu wa Wazo hali ni ile ile tu.
ReplyDeleteNa kumbuka watu wengi tunaoishi maeneo ya Boko, Tegeta, Bunju na hata mpaka Madale kwa mzee wetu kule juu kituo chetu kikubwa ni Wazo sasa kama wenyewe ndo hawayaoni haya tutakimbilia wapi?
Naunga Mkono hiyo hoja. Kwa kweli kwa sisi watumiaji wa barabara ya TEGETA ni hatari sana.Yangu ni haya yafuatayo;
ReplyDelete1.Malori hayana Break,ni kweli pale KIBAONI tunakoswa koswa mara nyingi!Mpaka unajiuliza hawa policy wa WAZO kazi yao nini? au trafic wa maeneo ya TEGETA wao wanakazi gani???? Mweee labda hii ARI ZAIDI....itatusaidia kusolve hili tatizo.
2. Mengine yanabeba michanga hayafuniki, najua sheria za mazingira zinamtaka mtu awafikirie watumiaji wengine wa barabara, unakuta michanga inapeperushwa, na inatuadhiri sana wengine, maana lazima itaingia machoni, au kama unatembea unakosa dira kabisaaaa!na ndo mwanzo wa kukongwa.
3. kituo cha daladala na SOKO pale barabarani TEGETA. Unashangaa kuona foleni zisizo za lazima, kwa sababau tu daladala na SOKO vipo barabarani. HV jamani mbona kule NYUKI kumewekwa mazingira mazuri kabisaa. Sheria Nchi hii hazifuatwi hata kidogoooo! injasikitishaaaa. na hiyo njia kuna wakubwa kibao wanapita, na viongozi wa Chama ndo huko huko nyumbani,wanaona hiyo kero lakini wamo tu!TUBADIRIKE JAMANI, VIONGOZI WAJIBIKENI
4. NASHUKURU MICHUZI KWA HII NAFASI YA KUTOA KERO
Wewe unaesema mapya umeyaona? Kila mara yana kosa break na kupitiliza pale Tegeta wakati yanatoka ile barabara ya Wazo, baada ya kushindwa kukata ile kona.
ReplyDeleteHuo ndio mtaji wa POLISI wanayapiga mkono halafu wanachukua rushwa sh.2,0000 halafu wanayaachia,lakini ukweli ni kwamba yale magari ni mabovu mno na yanahitaji matengezo.Polisi acheni kuhatarisha maisha yetu kwa kuchukia rushwa
ReplyDeleteNaona wote tunamawazo sawa sasa angalia kama tunaweza kufanya yafuatayo:
ReplyDelete1. Hii kero inabidi imfikie Mwema, Michuzi hakuna asiyejua kuwa watu wengi wanasoma hii blog yako na pia pilisi wamo, ni juu ya kila mmoja wetu hapa kutuma ujumbe kwa wahusika na connection pia tulizonazo zitusaidie kufikisha ujumbe huu.Tanzania hii ni yetu wote!!!
2. Kero ya soko la Tegeta barabarani, jamani hili ni tatizo sasa. Unaweza tumia hata masaa mawili kutoka kilimani njiapanda ya IPTL hadi kibaoni na tatizo ni soko barabarani. Hivi jamani haya malori yasiyo na break yakipitiliza pale sokoni wanakopanga vitu itakuwaje, tusisubiri ili litokee ndo tuchukue hatua.
3. Mara nyingine huwa nashangaa unamkuta polisi na yule trafic pale Tegeta sokoni kituoni, hivi huwa wanafanya nini pale..nisaidieni maana mimi sioni haja ya wao kuwepo pale wakati hali haibadiliki.
Naunga mkono hii hoja,kibaoni panatisha,tena ajiali ya 2 weeks ago ilimkosakosa mke wa mwenye hilo duka,alitoka alipokuwa amekaa anauza duka akaenda kunawa mikono chumba cha pili,kafika tu kule lori limeingia ndani na kuharibu vibaya pale alipokuwa amekaa.Bahati yake maana lingemuua.
ReplyDeleteUkikutana na magari hayo (hasa FIAT) usiku kuanzia saa nne mengi yana taa moja kama pikipiki na yanatembea katikati ya barabara, vile vile hayana nguvu ya kupanda mlima mdogo kama ule wa tegeta darajani kuelekea mjini kwa hiyo huenda taratibu sana au kusimama barabarani na kusababisha foreni ndefu. Nina hakika polisi wa patrol huwa wanayaona.
ReplyDeleteNaungana na hoja yako mdau ila la msingi sio kwamba wahamishwe hao ma OCD na team zao za hapo tegeta na wazo bali wawajibishwe kwa ajali hizi.
ReplyDeleteNashukuru kwa mdau kuliona na kulizungumzia, ila tu, kusema kuwa Raisi atasababishiwa ajali hilo mh... gumu maana they always pave a way for him, ila pressing point inakuwa usalama wa raia na mali zao in general + unnecessary traffic jam.
ReplyDeleteKuna Maford fulani ya someone Kassam yalikuwa yanacheza sana bandarini....
It is shame utakuta gari zima limekamatwa na hilo bovu linapeta meaning halionekani....
it is time for change, every one should enjoy Tanzania...
let me be honestly with you hii ndiyo sababu inanifanya nisirudi bongo. wao wakitaka kuingia barabarani wana weka vigora magari mabovu yanawekwa pembeni ukiuliza unaambia v.i.p huu ni upumbavu kabisa roho ya mtu ina v.i.p mbona ktk nchi za watu wanaojari wengine hakuna kitu kama hicho? tunapishana nao tu mitaani ila hawa mafisadi wetu ndiyo hivyo tena mimi naogopa kweli tena ila sina namna nangojea watoto wangu wakue kidogo nije maana ni kama unaenda afganistaan kurudi ni majariwa naipenda nchi yangu ila viongozi wake nawavulia kofia
ReplyDeleteTWIGA CEMENT ndio wanaolea ujinga huu! katika karne hii ya mambo ya "ISO STANDARDS" na "SHE" ina maana hawalijui hili!? wao wakikataa magari mabovu yasiingie kwenye eneo lao, hao Polisi watakulaje hiyo rushwa!?.......panaonyesha pale bado kuna watu wana akili za ki-SU!
ReplyDelete