JK na daktari wake Profesa Mohamed Janabi
wakiwa na kinamama wa kijijini Msoga alipowatembelea.


JK ameendelea kuongoza katika matokeo rasmi ya urais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambapo hadi sasa anaongoza katika majimbo 145.

Hadi jana jioni NEC ilikuwa imetangaza matokeo ya urais katika majimbo 171 kati ya 239 yaliyopo.

Matokeo hayo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Lewis Makame kwa kushirikiana na Makamu wake, Jaji Omar Makungu, yanaonesha aliyeshika nafasi ya pili ni mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amenyakua majimbo 19.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa kwa siku tatu mfululizo mgombea wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anafuatia akiwa anaongoza katika majimbo saba ambayo yote ni ya Tanzania Bara.
Habari Kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kinachoshanza na kwa nini NEC inatumia almost a week kutangaza matokeo? Kura zilihesabiwa siku ile ya uchaguzi kwenye vitu vya kupigia kura. Kila kituo kilijua nani kashinda na kilichobaki ni kujumlisha tu Tanzania nzima.

    I don't know why inachukua almost a week kujumlisha kura zote. Hii sio haki kwa wananchi.

    I hope NEC Chief will be fired.

    ReplyDelete
  2. Ila CCM mjifunze, ushindi wa wapinzani utazidi kukua kila mwaka wa uchaguzi kama hamtafanya kazi vizuri.

    Wabunge na mawaziri kama kina Makongoro Mahanga mmepita kwa bahati kwa kuwa chadema iliweka bomu, lakini hebu tuambie katika miaka mitano iliyopita ulilifanyia nini jimbo lako? ahadi gani uliitimiza? sasa kazi kwako kama unataka kura mwaka 2015 chapa kazi ahadi za uongo hatuzitaki.

    ReplyDelete
  3. Wengine walidhani kuwa makelel ndani ya Intenet ndio yanapigakura!

    Mosi, kura zinapigwa sana vijijini.

    Pili, kura nyingi zinatokana na wingi wa akina mama.

    Tatu, ingawa vijana wetu ni wengi (wenye miaka chini ya miaka 30, ukweli ni kwamba wenye haki ya kupiga kura sio lazima waipigie Chadema! Wana vyama vyao vya siasa, pia!

    ReplyDelete
  4. makongoro mahanga hakupita! wamechakachua!

    ReplyDelete
  5. This photo is a masterpiece and shows my president is a man of the people.Kikwete juu juu zaidi.

    ReplyDelete
  6. Sijui kwa nini kuwa 'mtu wa watu' inadaiwa ni sifa ya kuwa rais wa nchi. Marehemu mchonga alisema kama vipi mpe mwaliko mnywe naye chai.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...