JK akutana na Maalim Seif,
ahudhuria mnuso wa kuwapongeza wabunge

JK akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Maalim Seif Shariff Hamad katika ikulu ndogo ya mjini Dodoma ambapo viongozi hao wawili walifanya mazungomzo.Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana rasmi tangu kuchaguliwa Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa SMZ.
JK akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi(CHADEMA) Mh.John Shibuda wakati wa mnuso wa kuwapongeza wabunge iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. huyu bwana Shibuda anamtambua Raisi au??

    ReplyDelete
  2. hivi nikweli wabunge wote wa chadema hawamtambui jk ama wanapewa shindikizo toka kwa wakubwa wao?

    ReplyDelete
  3. Mbona kwenye minuso wanatokea. Hiki ni kituko . Hapo wanamtambuaJK ama walikuwa na njaaa!

    ReplyDelete
  4. watani zetu CHADEMA kumbe ilikuwa njaa hotuba mlitoka ukumbini mnuso mjaa tele na picha na JK sasa ndio waliowapigia kura wamewatuma hivyo...aibu wazee...CCM woyee

    ReplyDelete
  5. Wanatambua kama Kikwete mtu waliyemzoea na wamekutana naye mara nyingi na siyo kama Rais aliyetangazwa na Tume, na kama umesikia speech ya Dr. Slaa amesema binafsi hawana chuki na Kikwete kama Kikwete ila system iliyomwoka kinyemela. Njaa kwani hizo pesa zimetoka mfukoni mwake au ni pesa zetu wananchi

    ReplyDelete
  6. Kweli hawa wabunge wa CHADEMA siwaelewi kabisa. Na sijui wapo kwa maslahi ya nani.
    Waache utoto waendelee na siasa za kweli.

    ReplyDelete
  7. KUWENI WAELEVU HIYO NI SHEREHE YA KUWAPONGEZA WABUNGE YEYE SIO MBUNGE ILA KAALIKWA HIVO KUSALIMIANA SIO KOSA

    ReplyDelete
  8. wengine hawajui siasa na uwasama si kama hata kusalimiana kibinadamu kupo na kwenye sherehe ni ya bunge kuwapongeza wabunge wote na sio ya JK pale hata yeye JK amekaribishwa tu wanasalimiana kama binadamu mwingine.

    ReplyDelete
  9. MBOWE SASA UNAKIPELEKA CHAMA PABAYA..UMEANZA KUTOA SHINIKIZO KWA VIONGOZI WENZAKO UNAOWAONGOZA KUFUATA UNAVYOTAKA WEWE.
    SWALI....KAMA HAMNA UGOMVI NA JK.MNA UGOMVI NA TUME.JE ITAKUWAJE USEME HAMNA UGOMVI NA MTU AMBAYE KAWEKWA NA TUME MSIYOIKUBALI.UTAPENDAJE BOGA WAKATI UA LAKE HULIPENDI???
    MSIANZE KUTICHANGANYA WANACHADEMA- TUMEWATUMA HUKO KUTUWAKILISHA.
    JE KWA NINI HAMKUHUDHURIA WABUNGE WOTE THEN MKASIMAMA NA KUTOKA NJE?HII INAONYESHA KUNA TOFAUTI TAYARI NDANI YENU MNABURUTANA WATU KUFUATA ODA ZA WAKUBWA.
    kwa style hii soon kutatokea CHADEMA HALISI NA CHADEMA TMK

    ReplyDelete
  10. HII KALI KWELI. CHADEMA HAMTAKI KUSIKILIZA HUTBA LAKINI MPUNGA MWAENDA KULA!!! TUWAELEWEJE? WOTE NJAA KALI TU! SHAME ON YOU!

    ReplyDelete
  11. jamani kushiriki kwenye mnuso kwa hao wabunge wa chadema ni sawa kwani hiyo sherehe ya kuwapongeza wabunge imeandaliwa na Rais? kama ingeandaliwa naye labda tungetafuta muongozo. and yanayotokea ndio siasa zenyewe.
    mdau

    ReplyDelete
  12. jamani kushiriki kwenye mnuso kwa hao wabunge wa chadema ni sawa kwani hiyo sherehe ya kuwapongeza wabunge imeandaliwa na Rais? kama ingeandaliwa naye labda tungetafuta muongozo. and yanayotokea ndio siasa zenyewe.
    mdau

    ReplyDelete
  13. Aibu eeh imewapata x2

    Na nyie mnaotetea mnachekesha kweli kwani JK alikuwa anazindua serikali yake au Bunge? Sasa kama walisusa uzinduzi wa Bunge kwenye mnuso wamekwenda kufanya nini? UROHO TU WA MALI NA MADARAKA HAWANA LOLOTE! UKISUSA SUSA VYOTE! Sio kuchagua huku mnachungulia hotuba kwenye luninga na kwenda kwenye mahanjumati!

    Hivi sijui waliingiaje kwenye ukumbi wa sherehe hata picha sipati! Sijui walikuwa wananyata kama mtoto aliyemkosea babake anaogopa kuadhibiwa au sijui waliingia kwa fujo kama mtoto nunda asiyesikia wala kujali, yaani picha hainiingii akilini kabisa!

    Mwee makubwa tutayaona mwaka huu!!

    ReplyDelete
  14. huu ni umbumbumbu na upumbavu kabisa...bia wanataka hotuba hawataki duh kazi ipoi Tanzania

    ReplyDelete
  15. huo mnuso umeandaliwa na mh jk kuwapongeza wabunge kama wameudhulia inamaana wana mkubali maana yeye ndiye muandaaji

    ReplyDelete
  16. Sherehe ni ya kupongeza wabunge sio RAIS. JK ameenda kama mwalikwa sasa wabunge wa CHADEMA wasimsalimie? Hawana ugomvi nae ila system ilomweka kinyemela ndio tatizo. Halfu mjue kwamba kijana yeyote anayetetea CCM ni mchawi!!! Sasa hivi tunataka mapindizi ya kiuchumi na sio Uhuru kutoka kwa wakolini. Hiyo kazi walifanya wazazi wetu kama kijana unafanya nini? Au ndio akili zimeganda huwezi kufikiria na kuamua kwa hiyo unataka kuendeleza ya zamani wakati hayana tija tena?

    ReplyDelete
  17. Mimi nawashangaa ninyi watu mnaoshindwa kuelewa hapo. Mnuso ulikuwa wa kuwapongeza wabunge Kikwete kazamia tuu kwenye mnuso, sasa wao wangefanyaje?.

    ReplyDelete
  18. ......Aiseeh! kumbe kujua kufungua BLOG sio kuwa unajua mambo!! yaani mtu kusema hakubaliani na matokeo pamoja na taratibu zilizomueka kiongozi madarakani na ameamua kuchukua msimamo kuonyesha msisitizo....watu hawaelewi! DUUUUUh makubwa!

    ReplyDelete
  19. Maoni ya watu wengi hapo juu yanaonyesha jinsi ambavyo darasa au elimu ilivyo ndogo Tanzania. Watu hawajui hatua za ki katiba za kupinga jambo fulani. Chadema wanatuelimisha wa afrika kuwa tunaweza kupingana ki hoja na kisheria siyo kupigana hovyo!

    Nyerere alipigania uhuru kwa mtindo huu huu alikwenda UNO na kupinga utawala wa wakoloni pasipo kuingia msituni. Kumwagiana maji ya upupu imepitwa na wakati. Huo mpunga ni kodi yetu watanzania.

    ReplyDelete
  20. Mimi nafikiri Tanzania bado tuna kazi kubwa ya kumuelewesha Mtanzania haki yake mnaposema mbona hawakususa sherehe JK sio aliyefanya hiyo sherehe hiyo ni kodi yako wewe ambaye huna maji wala barabara unapoishi. CHADEMA hawachukii Tanzania wanajaribu kukufungulia wewe mlango wa maisha bora jiulizeni miaka mingapi tumepata Uhuru na maendeleo makubwa uliyayaona ni yapi kuna mikoa mingine bado wanatumia barabara na vitu vingine vilivyoachwa na Mkoloni, Jamani mkiwa mnaandika Comments jaribu kuweka comments zitakazo msaidia Mtanzania sio kumrudisha nyuma hata kama ccm imeshinda ni sawa lakini muamko wa siasa aliyouleta Dr. Slaa utamsaidia Mtanzania kujua haki yake na kuwa hao viongozi waliochaguliwa wanapaswa kukusaidia wewe na pia una haki ya kuwaondoa kama hawafai.

    ReplyDelete
  21. Nimekuwa nikisoma comments tangu mda mrefu sana kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Kitu nilichojifunza ni kiwango cha udini uliotawala ktk mioyo ya watanzania wengi sana hapa nchini. Hii imetokana na mbinu chafu za CCM ili kujipatia ushindi. Na kwa hilo kwakweli pasipo kuangalia side effect yake CCM wamefanikiwa. Jana wakati CUF ilipokuwa na nguvu CCM waliupenyeza huu mchezo kwa kujenga hisia kwa wananchi kuwa CUF ni chama cha kidini na kinafadhiliwa na nchi za kiarabu kupitia Organization of the Islamic Conference (OIC) na wakatumia kigenzo cha CUF kukubalika zaidi ukanda wenye waislam wengi (hasa ukanda wa mwambao wa bahari na visiwani kwa ujumla huku asilimia 100 ya viongozi wake wakiwa ni waislam, hapa nawapa hongera wamefanikiwa.
    Baada ya kuwanunua viongozi wa CUF suala la udini kwa CUF halizungumziwi tena sasa leo wamehamia kwa CHADEMA wamepenyeza uwongo CHADEMA ni chama cha wachaga, ni chama cha wakristo na kinapata misaada kutoka VATCAN na asasi mbalimbali za kimataifa kutoka nchi za ulaya.wakitumia mbinu ileile kwa sababu CHADEMA kinakubalika zaidi bara na maeneo machache ya ukanda wa pwani. Sumu hii imeisha enea kwa watanzania wengi sana na imeanza kufanya kazi na kwa kiasi Fulani kwenye uchaguzi wa mwaka huu imefanya kazi, mfano ukizisoma comments mbalimbali za wote wanaoipinga CHADEMA woote wametawaliwa na chuki za kidini hadi wengine wamefikia steji wanajiita majina ya kikristo na wengine wakijifanya CHADEMA damu na hapo hapo kukikiponda ktk misingi ya kiimani.
    Baada ya kufurahia ushindi sumu hii imeanza kuwarudia CCM wenyewe… leo hii mashehe na viongozi wa kikristo wameanza kulalamika juu ya udini…. Rais Kikwete anachanganyikiwa na udini jinsi unavyoshamiri na kuchanua.
    Kesho wananchi tutaanza kujiuliza ;-
    1) je, ni viongozi wangapi wanaoteuliwa na raisi ni wakristo na wangapi ni waislam- wakuu wa mikoa, wakurugenzi, mabalozi, etc.?
    2) je, kwanini anapokuwa rais mkristo makamu wake anakuwa muislam?
    3) je, kwanini anapokuwa rais muislam makamu wake anakuwa muislam?
    4) je, kwanini ktka serikali wizara zote nyeti na muhimu wanachaguliwa watu wa dini flani
    5) je, Tanzania kwa ujumla ina waislam wangapi na wakristo wangapi na wanawakilishwaje, kwa nusu kwa nusu au kwa uwiaro (ratio)ya uwingi wao?
    6) je, ktk mgawanyo wa vyeo ndani ya CCM vyeo vyote vya juu vimeshikiliwa na nani?
    7) n.k.?
    KIKWETE! KAZI KWENU MOTO MMEUWASHA JOTO MPEPATA NA BARIDI IMEONDOKA SASA KAZI KWENU KUUZIMA

    NONDO

    ReplyDelete
  22. wengi wa watanzania wanakera kweli,uwezo wa kufikiri ni mdogo ndio maana hata wakidhulumiwa haki yao hawajui kudai, wapo wapo tuu kama mbumbumbu,ipo siku mtakuja kuelewa wanachokifanya CHADEMA kwamba kina manufaa kwa watanzania

    ReplyDelete
  23. kweli watanzania viazi...samahani nadhani ukijumlisha watanzania utakosea.
    wengi wa watoa maoni (sina hakika kama ni wa-tz) ni viazi!

    Why? Chadema wametumia haki yao ku-protest, badala ya kuwasifu mnawadhihaki.
    Ni nani asiekili udhaifu wa mfumo wetu wa uchaguzi?? asimame
    Nani asiekili udhaifu wa katiba yetu? nashukuru baba wa taifa aliliona hili na kukiri wazi.

    Watanzania kama tunataka maendeleo, tuwe wakweli na tujenge tabia ya kusimamia ukweli. hii habari ya mtu anakukanyaga mguu unagugumie eti ataacha ife mara moja.

    heko chadema, tuko pamoja

    Mungu ibariki TZ

    ReplyDelete
  24. Mimi ni Mkenya na wala si Mtanzania lakini nilikuwa macho kuangalia matokeo ya uchaguzi pamoja na utaratibu mzima.

    Ukiangalia mawazo ya wengi wanaojaribu kupinga mawazo ya chama kama CHADEMA ni watu ambao mawazo yao ni ya duni pia ni watu kuishi kwao ni kwa kubabaisha. Lakini hii si ajabu kwani wakati Mandela anapigania haki ya watu weusi walikuwepo weusi ambao walishirikiana na Makaburu kutaka kumuangusha! Sasa hawa watu wameisha anza kujikomba ili waonekane kama walikuwa upande wa Mandela! Si ajabu hata kwa TZ itakuwa hivyo kwa miaka ijayo. CCM haitakuwa mabadarakini milele! Hiyo inabidi ieleweke.

    Pili swala la CUF linaeleweka. CUF imeingia mkataba na CCM ktk kuunda serikali ya mapinduzi Zanzibar! sasa itakuwaje wawe wapinzani tena wa serikali hiyo! There is no logic at all!

    Kwa maana hiyo CHADEMA msikubali kuwahusisha CUF ktk shughuli zenu kwani hawa jamaa ni sehemu ya serikali!

    Mwisho nafikiri swala la udini LImeletwa na baadhi ya viongozi ambao sisi sote tunawajua. Huu moto atakaye uzima anajua mwenyewe alipo. IKUMBUKWE KUWA WATANZANIA PAMOJA NA SISI WAKANYE HATUDANGANYIKI. ANGALIA KWENYE INTERNET MANENO YA MPGANAJI WA ANT CORRUPTION SQUARD WA KENYA BWANA LUMUMBA '' UTAFAHAMU KUWA WATU WAMECHAOKA NA HAWADANGANYIKI TENA''

    ReplyDelete
  25. wee unayetetea chadema akili zako haziko sawasawa hapa swala ni kumtambua na kutambua madaraka ya JK alipokuwa bungeni hawakutaka kwenye msosi wamekuja...kwanini wasingelisusa mojakwamoja...wananjaaa hao. Ok JK kaalikwa kaalika si ni madarakani kwake si wangekitoa tuuu. Siasa hizo bado jamani TZ we need Unity hata kama wengi wenu Love ni adimu. Mmeanza vibaya sio ukumbi wa disco ule ni mahala pateule

    ReplyDelete
  26. Chadema walitamka kuwa hawamtambui JK kama Rais wa Tz.

    JK ndiye kiongozi wa serikali iliyopewa mandate na wa-Tanzania; ndiye kiongozi wa mihimili yote ya serlaki: Executive, Sheria na Bunge!

    Basi Chadema susieni mihimili hiyo yote! Mtaeleweka kwa wananchi. La sivyo, acheni upuuzi wenu! Muwe kama Al Gore wa Amerika alivyoona masilahi ya taifa ni makubwa kuliko ya chama!

    Acheni utoto wenu! Ingieni Bungeni mchape kazi! Mlichaguliwa kuchapa kazi sio kususia chochote.

    ReplyDelete
  27. Chadema wamechemka hapa na wewe unayejiita mkenya kwanza nenda kwenu mkamalize ukabila sana sana mnaombea na sisi tuingie kwenye machafuko kama kwenu wewe fanya kilichokuleta usjiingize katika mambo yasiyokuhusu

    ReplyDelete
  28. Kwa kweli Watanzania itatuchukua muda kuelimika. Kama huyo mdau Tarehe Fri Nov 19, 10:30:00 PM, aliyemjibu Mkenya "wewe unayejiita mkenya kwanza nenda kwenu mkamalize ukabila sana sana mnaombea na sisi tuingie kwenye machafuko kama kwenu wewe fanya kilichokuleta usjiingize katika mambo yasiyokuhusu."

    Hii tuu inaashiria ni jinsi gani sisi watanzania tulivyo mbumbumbu. Wenzetu Kenya wamefight mpaka wamepata katiba mpya, sisi bado ndio kwanza hatujui kinachoendelea.

    ReplyDelete
  29. du kumbe uyu kijana amechangia wa mbunge eti wapite web.tembelea uone.www.drmanyaunyau.blogspot.com

    ReplyDelete
  30. uchaguzi umekwisha tuacha mambo ya vyama kama haukubali kushindwa wewe si mshindani na katika hali ya kawaida bila hata kuchakachua matokeo ya urais chadema isingeweza kuashinda hivyo wanoapinga ni ujinga tuu wakutokufikiri

    mdau ark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...