PONGEZI KWA MAAFISA UTAMADUNI
KWA SIKUKUU YA EID EL HAJI TULIVU
Baraza la Sanaa la Taifa kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo (WHUM) linapenda kuwapongeza Maafisa Utamaduni wote kushamirisha sikukuu ya Eid El Haji kusherehekewa kwa utulivu na amani.
Itakumbukwa tarehe 20/09/2010, Serikali kupitia Katibu Mkuu wa WHUM Bw. Seth Kamuhanda ilitoa tamko Kwa maafisa utamaduni kutotoa vibali vya kuendesha Disco Toto kwa kumbi ambazo si salama na zisizo na vibali.
Tamko hilo liliweka msisitizo kwa kumbi zote za sanaa na burudani kuhakikisha zinafanyiwa marekebisho ya kiusalama na kusajiliwa kabla ya tarehe 31/12/2010. Serikali inasisitiza kwamba, yeyote atakayekiuka agizo hilo ukumbi wake utafungiwa.

Hadi sasa hatujapokea taarifa yoyote
mbaya kutokana na Sherehe za Eid El Hajj.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI – BASATA
19/11/2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...