JK akiongea na wapangaji katika nyumba
aliyokulia huko Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani


JK anaendelea kuongoza kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano akiwaacha mbali wapinzani wake wakuu, Prof Ibrahim Lipumba na Dk Willibrod Slaa ambaye ametangaza nia ya kupinga matokeo.

JK amepeta katika majimbo 51 kati ya 56 yaliyotangazwa jana jioni na Tume ya Uchaguzi (Nec). Hadi leo jioni matokeo ya majimbo 180 yaliyokusanywa kutoka NEC na wasimamizi wa mikoani jumla ya kura zote kwa urais ni 5,608,303 na zilizoharibika ni kura 144,501.


Katika kura hizo JK kalamba kura 3,544,673 sawa na asilimia 63 akifuatiwa na Dk Slaa kura 1,234,245 asilimia 22 na Profesa Lipumba 589,451 asilimia 11.

Wengine ni Peter Kuga Mziray aliyepata kura 65,276 asilimia 0.1, Hashim Rungwe kura 13,809 asilimia 0.1, Mutamwega Mugahywa kura 9,740 asilimia 0.1 na Fahmi Dovutwa kura 6,607 asilimia 0.1.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

 1. JK anastahili!
  Ni Mtu wa Watu anaependa wenziwe, habagui watu na ameonyesha upendo mkubwa kwa wale wenye matatizo hasa vilema,wagonjwa,nk, kwa kujionyesha dhahiri yuko pamoja nao!
  Yeye ni Kiongozi bora kwa Nchi yetu!
  Yeye amerithi vyema na kudumisha yale yaliyoanzishwa na Mwalimu Nyerere, kuendelezwa na Mwinyi na kupelekwa juu zaidi na Mkapa.
  JK amempa uhuru kila Mtanzania kufanya anachokitaka bila bugudha.
  Lakini hawa wenzetu wasiotaka kukubali matokeo wana yao!
  Waende jirani tu, wamuulize Maalim!
  JK na Chama chake kinapendwa na wengi tangu enzi na enzi na ni Chama thabiti chenye msimamo kisichobagua yeyote!
  Hivi hujiulizi kura Mamilioni nani ataziiba?
  Hivi wewe ni kipofu na kiziwi usieona Watanzania wanamtaka nani?
  Hivi wewe unataka nini?

  ReplyDelete
 2. Mmmeiba kura.

  Tanzania sasa haina tofauti na Kenya au Zimbabwe. Yaliyotokea Kenya na Zimbabwe yakitokea Tanzania sintashangaa; JK bure kabisa. Hana moral authority yoyote ya kuwa kiongozi wa taifa la Tanzania. NEC na UWT wamewaona watanzania kama watu wasiokuwa na uwezo wa kujiamulia destination yao, badala yake wakatusimikia mtu wao........."we gonna fight........."

  Umaskini wa Tanzania utaongezeka sana katika kipindi kijacho cha utawala haramu wa Kikwete, na ninaapa kuwa hata kabla ya mwaka mmoja tu, Tanzania haitapata hata senti moja ya pesa ya msaada. Watakaoumia sijui ila laana yote itakwenda kwa Kikwete na watu wake., Historia yake katika tifa hili itakuwa mbovu sana kulinganisha ya ya mwenzie Kaunda aliyekubali matokeao bila kinyongo na leo hii bado anaheshimiwa hata na wazambia waliompigia kura ya hapana wakati huo. Kikwete will have a zero place in our history.

  ReplyDelete
 3. Matokeo ya uchaguzi tuliofanya Jumapili yataanza kutoka lini?

  ReplyDelete
 4. .....Nyie vp!!? .... hamjanilipa hela yangu mwaka mzima! na mnaona kabisa kampeni zimenikalia vibaya!.......au nyie CHADEMA NINI!?

  ReplyDelete
 5. Twende mbele turudi nyuma...JK ni rais wa watu na yupo sana na watu habagui mtu yoyote.Tumuachie kipindi hiki pia kwani ameshinda kwa kishindo.Mungu akulinde na akuzidishie uwaongoze tena watz kwenye kipindi cha miaka 5.Inshallah.
  Mdau wa UK.

  ReplyDelete
 6. JK,umewaunganisha wanzanaibar wamekuwa wamoja lakini jamii ya kitanzania imejawa na chuki haikupi hiyo sifa waz waz aliekiri hilo ni mmoja tu dk ali mohammed shein,pili uliwasaidia wakenya kupatana.kama unasoma maneno haya me nakwambia jitahid Mwenyezi Mungu atakulipa ila wanaadam watakuchukia hasa wasiokutakia mema.wewe ni muungwana hata mkapa anajua hilo kwan yeye alishindwa kuwapatanisha wazanzibar.

  mdau wa tbc

  ReplyDelete
 7. Baba mwenye nyumba kafuata kodi yake...

  ReplyDelete
 8. Mdau wa tbc umesema kweli, mie nafikiri JK yanamkuta ya Mzee Mwinyi alitutoa kwenye dona jeusi na unga wa yanga, sukari mpaka ununue na unga wa muhogo mbaya wenye michanga tena baada ya kupanga foleni, nguo na vitu kama dawa ya mswaki vilikuwa luxury. List ni ndefu kuanzia kuogea sabuni ya pundamilia, mpaka kuvaa makaunguza. Lakini tulivyolia mbwata basi tukaanza kumtukana matusi ya nguoni Mzee wa watu na kumzulia kila la kumzulia, lakini Mzee wa watu alikaa kimya, na Mungu ndiye anamlipia.

  Na JK naye aliingia madarakani wazanzibari wanaikimbia nchi yao, hawaulizani hali wala hawazikani. Uhasama na misukosuko kila siku isiyokwisha na aliweka ahadi kuwa hali hiyo inamkera na ataifanyia kazi. Na kweli matunda yake yameonekana, ndani ya miaka mitano ya utawala wake hakuna aliyefukuzwa darajani wala kupigwa mabomu ya machozi huko Pemba. Hakuna aliyebakwa wala kuuwawa kwa sababu za kisiasa, Zanzibar imerudisha hadhi yake iliyopotea tangu 1995. Umewaunganisha wazanzibari ingawa wako wahafidhina ambao walikuwa wananufaika na mgogoro huo watajaribu kutaka kuharibu kwa namna moja au nyingine. Hilo lisikupe taabu midamu ulibeba dhamana kama Kiongozi wa nchi na utakuwa massuuli siku ya hukumu wewe tenda haki, muachie Mungu ndiye atakayehukumu na kukulipa mema yako, sie binadamu hatuna wema wala fadhila wala shukrani. Na tanu yetu tukiwa hatuna shida na njaa sauti zinatoka! Kwani kamwe mwenye njaa hana nguvu ya kutoa sauti, sasa kama mzazi ukiona watoto wanazidi kibri na mdomo juu ujue wameshiba hao wala wasikupe tabu, wavumilie tu!

  ReplyDelete
 9. Kwani kuna ajabu kufuata kodi ya nyumba iliyojenga na wazee wake? Ni haki yake yeye na ndugu zake, ikiwa kodi anachukua yeye au ndugu zake sie hayatuhusu kwa sababu hajamuibia mtu hiyo nyumba wala hajamuomba mtu amjengee!

  Jenga yako na wewe au uwende ukarithi ya wazee wako!

  ReplyDelete
 10. Mpangaji.mzee bado natafuta nitakulipa baada ya wiki moja.

  Mzee. Mbona mwenzio kanipa 15 elfu
  tasilimu wewe sasa inakuwaje?

  Mpangaji.mzee mwanangu ndo
  tumemcheza juzi walahi
  tumebaki weupe.
  Mzee.teh teh teh teh.yaani
  hakiyanani sina kitu kampeni
  zimeniacha mweupe basi
  jumapili mapema sana nitakuwa
  naelekea kuapishwa dodoma
  nikukutepale kwenye nguzo za tanesko ukisindwa hama kwenye nyumba yangu. OK

  MPANGAJI.USHINDI MWEMA MZEE

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...