Kocha wa Twiga Stars Charles Boniface
Mkwassa na wachezaji wake


Timu ya taifa ya Tanzania Wanawake Twiga Stars imefungwa magoli 3-2 na timu ya taifa ya Mali katika mchezo wao uliofanyika nchini Afrika Kusini jioni ya leo.

Mchezo huo ulikuwa ni wa pili katika mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika kwa wanawake, ambapo mchezo wa kwanza Twiga Stars ilifungwa magoli 2-1 na timu ya wanawake ya Afrika Kusini BanyanaBanyana.

Hivi sasa timu hiyo inakabiliwa na mtihani mwingine wakati itakapocheza na timu ya taifa ya Nigeria na kutokana na vipigo hivyo viwili timu hiyo itacheza mchezo huu kama kukamilisha ratiba tu kwani kwa kufungwa mara mbili tayari imeshapoteza matumaini ya kusonga mbele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Twiga imelala 2-3 na sio 1-3. Kipa wa Twiga Fatuma kafanya uzembe sana goli la tatu.

    Bado kuna mechi moja ya kundi dhidi ya Nigeria

    ReplyDelete
  2. watalii aka wauza sura rudini mji si mumeuona

    ReplyDelete
  3. Wamejitahidi sana, tuwatie moyo. Ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa na walicheza kama washindani, has mechi na Banyanabanyana. Magoli mawili ya jana ni uzembe wa kipa. Kwangu mimi ni mwanzo mzuri!

    ReplyDelete
  4. Muache kuanza hamtafika mbali mukianza kutupiana lawama. Uzembe wa kipa uzembe wa kipa. kama ni team mukubali mumfengwa iishe. Sio kusema kwangu mimi ni mwanzo muzuri wakati mumefungwa. Chukueni somo mjifunze mukija siku tena mujue nini cha kufanya. Hizo kutupiana lawama ndio maana hatuendi popote. Cheseni as a team mkifungwa munafungwa as a team sio kutupa lawama kwa mutu mumoja.

    ReplyDelete
  5. Makocha hawana uwezo,timu apewe kocha Rogatian Kaijage.

    ReplyDelete
  6. Kocha wa 'braza braza'November 05, 2010

    Wapi 'braza braza' mwanadada mcheza wa kutumainiwa toka Serengeti? Je bado unasukuma gemu au umetundika njumu siku hizi?

    Nawatakieni nyote na Waalimu wenu kila la kheri. Ni imani yangu kuwa siku hadi siku soka kwa akina dada inakuwa na siku za usoni tutafanya maajabu. Ngoja turudi nasi tuwaunge mkono!

    ReplyDelete
  7. wewe kaijage acha kujishaua! si lolote si chochote!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...