K-Mondo Sound yaachia video mbili kali kwenye TV

Mangustino Richard (kulia) na Mhina Panduka 'Toto Tundu'

WAKATI ikiendelea na maandalizi ya uzinduzi wa albamu yake ya kwanza, bendi ya muziki wa dansi K-Mondo Sound imeachia video mbili ambazo zitaanza kuonekana wakati wowote kwenye vituo vya televesheni.

Richard Mangustino, kiongozi wa bendi hiyo, alisema video hizo ni za nyimbo za Njiwa na Your Still mine ambao umeimbwa na Mhina Panduka.

“Tayari tumekamilisha video mbili, Njiwa na Your Still mine ambazo zimefanywa na H.K Vision, kwa sasa tunafanya mpango wa kuzipeleka kwa vituo vya televisheni ili mashabiki na wapenzi wa burudani waweze kujua nini kinaendelea katika bendi yao,” alisema.

Mangustino alisema wimbo wa Njiwa uko kwenye mahadhi ya rhumba na kwamba ulikwishaanza kusikika kwenye vituo vya redio wakati Your still mine haujawahi kupigwa kwenye redio tumetengeneza video yake kwanza.
Alisema Your Still mine ni mchanganyiko wa rhumba na salsa ambapo Panduka ameimba kiingereza, kinyakyusa, kiwemba, kiswahili na Kinyarwanda.

Bendi hiyo inatarajia kuzindulia albamu yake ya kwanza mapema mwakani. Albamu hiyo itakuwa na nyimbo nane ambazo ni Njiwa, Magambo, Magambo, Sharufa na Maimuna.

Zingine ni Your Still Mine, Pendo, Uko mbali na Nitoe Out. Albamu hiyo imerekodiwa na studio ya Metro chini ya mtayarishaji Alain Mapigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...