Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya mbio za KILIMANJARO MARATHON ulifanyika jioni hii katika hotel ya New Afrika jijini Dar. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. David Minja (pili kulia) na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,Leonard Thadeo pamoja na warembo walioshika tepe hiyo.
Mkurugenzi wa Wild Frontier Bw. John Addison (kulia) akiwa katika meza moja na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, Bw. Suleiman Nyambui (kushoto) pamoja na Mwanariadha wa nyota wa kimataifa wa zamani, afande Juma Ikangaa.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa KILIMANJARO MARATHON,Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko akiwa Mkurugenzi wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Mareallle mara baada ya kumaliza kuhutubia.
Meneja Matukio na Miradi Maalum wa Executive Solutions, Bi. Angela Damas akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhulia katika hafla hii ya uzinduzi wa KILIMANJARO MARATHON iliofanyika jioni hii katika hoteli ya New Afika jijini Dar.Mbio za tisa za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Moshi tarehe 27 Februari 2011 zimezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam leo.
Akiongea katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, wadhamini wakuu wa mbio hizo Bw. George Kavishe alisema, “sasa tumeingia mwaka wa tisa wa udhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon. Tunaona fahari kudhamini tukio kubwa zaidi la riadha hapa Tanzania ambalo limevutia ushiriki wa wadhamini mbalimbali, serikali, jamii ya Kilimanjaro na wanariadha mashuhuri kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kavishe amesema bia ya Kilimanjaro imedhamiria kuendeleza riadha nchini Tanzania kwa kupitia mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zimeendelea kuwa kisima cha kuzalisha vipaji na kuwapa wanariadha wanaochipukia fursa ya kujipima kwa kushindana na wanariadha mashuhuri. Hili linawapa changamoto wanariadha kuboresha viwango vyao na hatimaye kupata sifa za kushiriki katika mbio kubwa zaidi za kimataifa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko amesema “Tangu Mbio hizi zilipoanzishwa mwaka 2003 zimekua chungu cha kupika vipaji katika riadha hapa Tanzania na kwakua zinaendelea kuwa kubwa zaidi kila mwaka ni matarajio yetu sote kuwa nchi yetu itaendelea kuwa na wanariadha wazuri katika mbio ndefu. Serikali inatambua mchango wa wadhamini na waandaaji wa Kilimanjaro Marathon katika kuendeleza mchezo huu na kuitangaza Tanzania maana mbio hizi huvutia sana watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.”
Profesa Mwansoko alisema amefurahishwa na azma ya wadhamini kuendelea kudhamini Kilimanjaro Marathon na kuwapa wanariadha Watanzania fursa ya kuonyesha uwezo wao katika ushindani na wanariadha mashuhuri kutoka nchi mbalimbali.
Wadhamini wengine katika mashindano hayo ni Vodacom, Tanzania Tourist Board, Tanga Cement, DT Dobie, Tanzanite One, KK Security, Keys Hotel na Maji ya Kilimanjaro.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...